It is good that shes coming back lakini. Ni dhahiri kwamba katupatia heshima kubwa sana, lakini jamani, lets not hype up this thing, huyu mama ni mwanasiasa mchanga sana, but ofcourse she is very articulate, lakini hana cha ajabu kutuletea. Kuna watu aidha sawa na yeey na wengine wengi zaidi bora kuliko yeye. Kwa mfano, Migiro hawezi kusimama na Prof Tibaijuka pamoja na kumpiga sana majungu alipokuwa huko UN, na analijua hilo wazi. Lakini muhimu hapa ni kwamba tuna hazina nzuri ya kina mama kuliko huko nyuma, migiro, tibaijuka, ni wawili tu in the recent past, wengine ni siasa za kulala na wakubwa tu;
Nafasi za naibu katibu mkuu UN huwa ni ya miaka mitano tu, kwahiyo hakuwa na jinsi; na alikubali nafasi hiyo akijua hilo - yani kwamba atarudi nyumbani kabla ya 2015; kuna nafasi wazi pale New York ubalozi, inawezekana kabisa mabadiliko ya mawaziri yakatokea to accomodate her esp kwasababu ni mwanamke, na waziri mmoja akatupwa huko NY ubalozi, ili kumpisha mama migiro uwaziri, au hata pengine tunaweza shangaa anapewa nafasi kubwa ya chama. Nje ya hapo, migiro ni kiongozi wa kawaida tu, hana cha ziada zaidi ya kuwa mmoja ya kina mama wachache wenye nyota katika siasa.