Ni kama nimemwelewa hivi...hupati kitambulisho cha Taifa kama huna barua ya mtendaji, sasa ukiwa tayari unacho kitambulisho au namba ya NIDA barua ya mtendaji ya utambulisho ni ya nini tena? Nadhani ndiyo lengo lake mifumo kutosomana
Kujua makazi yako au unapopatikana kwa wakati huo, na anae omba ni wewe kwa uthibitisho toka kwa mtendaji au mwenyekiti wa kijiji
Kwa kuwa ina aminika Hawa viongozi huko chini ndio wanaweza thibitisha ukaazi wako eneo hilo kwa muda fulani na namba ya nyumba, mtaa
Labda huko mbele kama taarifa zikiwa Sawa sawa ndipo tunaweza kuhama taratibu
Vilevile ikumbukwe Kuna wazee wetu ambao hawana vifaa vya kidigitali kuweza kutumia ili kusaidia maswala yao ya kila siku
Mifano midogo, huduma za stationery hazijaenea, gharama ni kubwa pia.
Kuna huduma za jihudumie lakini sio wengi wanaweza kuzitumia, kijana wa kidato cha Sita hawezi kuomba cheti cha kuzaliwa au kifo, mkopo, barua ya utambulisho
Msafiri hawezi omba passport, visa application online, booking ya ndege, hotel au accommodation
Mfanyabiashara hawezi kuomba TIN online, leseni ya biashara
Mfanyakazi hawezi kuomba bima ya afya mtandaoni, kujaza majukumu yake nk
Yapo mengi, muhimu yanafanyiwa kazi taratibu