Mifuko ya hifadhi ya jamii yaanza kujenga viwanda

Mifuko ya hifadhi ya jamii yaanza kujenga viwanda

Well, basi tunaweza kusema 95% ya watanzania wameajiriwa kwa sababu kila mmoja anaingiza kipato japo kinakuwa sio direct kutoka kwa mwajiri, Ndivyo unataka kusema mkuu!?
Nimeongelea kuhusu value chain inayohusiana na sekta inayohusika kwa maana wale wadau wa kiwanda ambao wanahusika na na kuhakikisha product ya muwa inaingia kiwandani..Mkulima, transporter wa product na wengineo...Nakupa mfano mimi naweza kuanzisha kiwanda cha mafuta ya alizeti.. Kile kiwanda kitahitaji supply ya alizeti. Ile alizeti mpaka ifike kiwandani kunaweza kukawa kuna watu wengine wapo involved ambao ajira zao hazihusiani na kiwanda....Ni mtazamo tu mkuu
 
Bavicha wakisikia kauli ya hivi wanaugua kabisa,sijui kwanini wanaombea serikali hii ishindwe" kwa rafudhi ya kanda ya ziwa" Nimesema hakuna atakayekwamisha serikali yangu zaidi ya kukwama yy mwenyewe"
 
wanaongozwa na wanasiasa badala ya kufanya tathmini ya kina

Pesa wanazokusanya hawa taasisi za Pension funds [ mifuko ya jamii] sio fedha zao bali ni za wafanyakazi; utaratibu huu ulianzishwa ili kuwasaidia wafanyakazi wasipate taabu pale wanapostaafu/ kuacha kazi!! Hizi fedha ni akiba yao wanayotakiwa kupewa mara wanapoacha kazi!!

Serikail kuamua kuwalazimisha hawa waendesha hizi taasisi kuwa hizi fedha za wafanyakazi zitumke kuanzisha viwanda sio sahihi kwasababu mifuko ya jamii sio kazi yao kuanzisha na kuendesha viwanda hizo ni kazi za wawekezaji [ entrepreneurs] ambao ndio shuhuri yao kutafuta mitaji na kuwekeza pale ambapo pana faida!!!

Kulazimisha mifuko ya jamii kujenga viwanda ni kurudia makosa yale yale tuliyofanya huko nyuma ya kuwa na mashirika ya umma katika uzalishaji bidhaa ambapo nchi ilipoteza rasilimali nyingi kwa uendeshaji wa hayo mashirka kwa hasara !!!

Let the private sector take the risks in investing in the industrial sector; they can source the funding and run the businesses because they have the expertise!! The government should only concentrate on formulating policies that will enable the industrial sector to thrive.

Acheni kufanya mambo kwa pupa mkidhani mkifanya hivyo mtafanikiwa; kaeni kitako na kufanya tathmini ya kina ya mambo bila kuogopana huku mkishauriana bila vitisho!!
 
Huu ni upuuzi,mifuko ya jamii mwisho wa siku itafilisika kabisa kwasababu ya kugeuzwa shamba la bibi na hawa wanasiasa.Kwanza inaidai serikali billions of money na bado wanaikwangua tu humu kuna watu wanashabikia.
 
Nimeongelea kuhusu value chain inayohusiana na sekta inayohusika kwa maana wale wadau wa kiwanda ambao wanahusika na na kuhakikisha product ya muwa inaingia kiwandani..Mkulima, transporter wa product na wengineo...Nakupa mfano mimi naweza kuanzisha kiwanda cha mafuta ya alizeti.. Kile kiwanda kitahitaji supply ya alizeti. Ile alizeti mpaka ifike kiwandani kunaweza kukawa kuna watu wengine wapo involved ambao ajira zao hazihusiani na kiwanda....Ni mtazamo tu mkuu
Ndio, na hicho kiwanda chako cha mafuta labda kimeajiri direct watu 600, mjasiliamali mwingine jirani anaona fursa kuwa baada ya kazi hawa wafanyakazi sababu ya kuwa na kipato na uchovu anafungua kagrosari jirani ambapo tuseme 150 kati ya hao wanapitia na kupata wastani wa bia 7 kwa week (bia 7 x 150). Kwa hiyo katika mchanganuo wako utasema kuwa mmiliki wa baa na wahadumu umewaajiri wewe!?
Yaweza kuwa ndio au hapana na ndio maana taasisi ikitaka kuanzisha kiwanda lazima iangalie direct employments kwanza kama MeTL wanavyotaja watu 30,000 wakati tunajua kuna retailers hata mara mia ya hao. Ina maana wanajenga kiwanda cha sukari bila mashamba yao ya miwa ukitegemea wakulima ndio walete hiyo miwa yote!
Hatupingi lakini kauli kama hizi zinatupa mashaka maana tumezaliwa katika nchi hii na tunaijua, tunawajua waliokuwa wakipiga kelele za 'ujamaa oyee' jinsi walivyolibadilia Azimio la Arusha na kujigeuza majizi makubwa!
 
Naona hatujaelewana.. Maana ulivyotoa tu mfano wa glocery nimeona hatupo on the same page kuhusu understanding ya value chain..All the best..
 
Sekta ya hifadhi ya jamii ndio inaelekea kibla hivyo!! Poleni sana mliodhani itainua migongo yenu baada ya kuwa imesulubiwa na mwajiri.
Naomba kujua kama kuna mfanyabiashara mkubwa au mwekezaji aliyefanikiwa kibiashara hapa Bongo kwa kutekeleza maagizo ya serikali.
 
Katika kuweka kumbukumbu sawa:
1. Kuna watu waliambiwa KILIMO KWANZA wakalima kwa kumaanisha, je kimewakuta nini?
2. Kuna watu waliambiwa KILIMO NI BIASHARA, wakalima nyanya ekari, je wamepata nini?
3. Kuna walioambiwa wajenge vuo vikuu ili kukabiliana na uhaba wa waalimu wa sekondari, je kwa sasa waalimu wameajiriwa? Je serikali inaonyesha hari ya kutaka waalimu?
4. Kuna walioaminishwa ya kuwa Mtwara itapaa kiuchumi, hivyo wakawekeze. Ardhi ikapanda bei hatari, je nini kimewakuta?
"Za kupewa na 'mbayuwayu' changanya na zako".
 
Warudishe na fao la kujitoa ili na sisi wajasiriamali tupate mitaji ya kuanzisha biashara na shughuli zetu wenyewe
umeona enhee kaka wanatumia pesa zetu kujengea miradi that is not fair mwisho wa siku hatunufaiki na chochote
 
Mifuko ya hifadhi ya jamii imeanza mikakati ya kujenga viwanda ambapo kiwanda cha sukari kitajengwa Morogoro chenye uwezo wa kuzalisha tani 200,000 kwa mwaka na kuajiri watu 100,000.

Pia kuna viwanda vya kutengeneza mafuta ya alizeti na usindikaji wa nafaka mahindi ambavyo vitajengwa Dodoma na Iringa

Mimi ninaajua kuwa mifuko ya hifadhi ya jamii kutumia michango ya watu kujenga viwanda sio sahihi, na kwa uhakika ni kosa kubwa. Mifuko ya hifadhi ya jamii inatakiwa kuwekeza kwenye miradi ambayo ni (risk free), na mahali pekee pa kuwekeza ni kwenye hati fungane za serikali. Ni serikali chache zinaweza kufilisika, kwa umri wangu wa miaka 60 nimeona serikali 3 tu zilizowahi kuwa mfilisi ( Serikali ya Somalia iliyokuwa na rais Siad Bare, serikali ya kisovieti ya Urusi- ya Michail Gobachov na serikali ya Ujerumani mashariki ya Honeka).

Kuwekeza katika viwanda ni jambo jema lakini sio salama kwa wanachama wa mifuko hii. Sasa kutokana na tabia aliyoianzisha rais wa awamu ya nne ya kukopa bila kulipa wataafu wengi hawajalipwa mafao yao. Imefikia mahali watu waliostaafu kuanzia mwezi wa nne mwaka huu hawajalipwa mafao yao hadi sasa. Mifuko imefikia hatua ya kuwaomba wawalipe pensheni ya kila mwezi hata kabla ya kulipa kile kiasi cha mkupuo-lumpsum.

Kwanini serikali hii haijifunzi kutokana na makosa ya serikali iliyopita? Haki hii ya serikali kupora haki za msingi za wataafu inatokana na katiba, sheria au ni kiburi? Ninajua Magufuli hajafikisha miaka 60 na vivyo hivyo waziri wake mkuu kwa hiyo sio wazee, na matatizo ya wazee hayawahusu! Rais atatunzwa hadi kufa hata akiishi miaka 200 na waziri wake mkuu hivyo hivyo. Haki za wazee wanyonge zinaangaliwa na nani? Rais anawawekea dhamana gani kuwa viongozi watakaofuata wataheshimu taratibu za kulipa madeni ya viwanda hivyo. Nani msimamizi wa viwanda hivi? Au ni mkopo kwa serikali na serikali ndiyo itasimamia uendeshaji wa viwanda na mapato itakayoyapata italipa mifuko ?

Hii sio haki na ninawaona wataalamu wa mifuko wamejifanya hamnazo wanaanza kuwekeza. Hii ni hatari.
 
Huwezi kutumia pesa za mifuko ya jamii kujenga viwanda.

Hakuna short-term return na hata hiyo long-term return ni very risky.

Kuweka rekodi sawa si watanzania wote wanashangilia haya makosa ya makusudi yanayofanywa kwa kukiuka miongozo ya BOT na SSRA.

Hili suala la viwanda linageuka kuwa obsession itakoangusha uchumi kwa serikali kuweka nguvu kwa kitu ambacho hakilipi.

Muda utaongea.
Kwa maoni kama haya inakuwaje ujiita "introvet"? Nimeyapenda
 
Mimi ninaajua kuwa mifuko ya hifadhi ya jamii kutumia michango ya watu kujenga viwanda sio sahihi, na kwa uhakika ni kosa kubwa. Mifuko ya hifadhi ya jamii inatakiwa kuwekeza kwenye miradi ambayo ni (risk free), na mahali pekee pa kuwekeza ni kwenye hati fungane za serikali. Ni serikali chache zinaweza kufilisika, kwa umri wangu wa miaka 60 nimeona serikali 3 tu zilizowahi kuwa mfilisi ( Serikali ya Somalia iliyokuwa na rais Siad Bare, serikali ya kisovieti ya Urusi- ya Michail Gobachov na serikali ya Ujerumani mashariki ya Honeka).

Kuwekeza katika viwanda ni jambo jema lakini sio salama kwa wanachama wa mifuko hii. Sasa kutokana na tabia aliyoianzisha rais wa awamu ya nne ya kukopa bila kulipa wataafu wengi hawajalipwa mafao yao. Imefikia mahali watu waliostaafu kuanzia mwezi wa nne mwaka huu hawajalipwa mafao yao hadi sasa. Mifuko imefikia hatua ya kuwaomba wawalipe pensheni ya kila mwezi hata kabla ya kulipa kile kiasi cha mkupuo-lumpsum.

Kwanini serikali hii haijifunzi kutokana na makosa ya serikali iliyopita? Haki hii ya serikali kupora haki za msingi za wataafu inatokana na katiba, sheria au ni kiburi? Ninajua Magufuli hajafikisha miaka 60 na vivyo hivyo waziri wake mkuu kwa hiyo sio wazee, na matatizo ya wazee hayawahusu! Rais atatunzwa hadi kufa hata akiishi miaka 200 na waziri wake mkuu hivyo hivyo. Haki za wazee wanyonge zinaangaliwa na nani? Rais anawawekea dhamana gani kuwa viongozi watakaofuata wataheshimu taratibu za kulipa madeni ya viwanda hivyo. Nani msimamizi wa viwanda hivi? Au ni mkopo kwa serikali na serikali ndiyo itasimamia uendeshaji wa viwanda na mapato itakayoyapata italipa mifuko ?

Hii sio haki na ninawaona wataalamu wa mifuko wamejifanya hamnazo wanaanza kuwekeza. Hii ni hatari.
Jamani mbona kinachofanyika na mifuko ya jamii ni sahihi. Wanachokifanya wao wanajenga then wanaipa taasisi ama kampuni ndo inacontrol business.

Mfano mzuri. Ni chuo kikuu cha dodoma chote kimejengwa na mifuko ya hifadhi ya jamii na chuo kama taasisi kimepewa dhamana ya kurudisha mapatao kwa miaka 50.

Mfano mwingine daraja la kigamboni mbona ni wao wamejenga na wameipa kampuni binafsi kwa ajili ya ukusanyaji wa mapato. Na watapokea mapato kwa muda wa miaka 30.

Watanzania tuache ulalamishi. Kwa upande wangu mifuko ya jamii ina haki zote za kutumia fedha hizo kwa ajili ya kuwekeza na kuinua sekta ya viwanda nchini. Tutakua taifa la majuha kama mifuko yetu itakua na mabilioni ya pesa kwenye mabenki lakini hizo pesa hazizunguki. Au ndugu zangu bado tupo kwenye zama za kutegemea wawekezaji kutoka nje..? Tuwe wazalendo na tuiunge mkonk serikali katika kuwekeza kwa pesa zetu wenyewe.

Kule marekani wenzetu kipindi cha new deal waliamua kutumia mifuko ya hifadhi ya jamii kuinua uchumi wao chini ya rais Franklin Rooselvelt. Watanzania naona tunarudi kwenye zama za ukabila na ukanda. Kuna tatizo gani kiwanda kikiwa Dodoma. .?
 
Afu watu wa singida povu linawatoka sasa nimeamini kumbe zile akili za kina wema sepetu sio makosa yao ni tatizo la watu wa singida wote.
 
Kagera Sugar au Mtibwa wanazalisha tani ngapi na wameajiri wafanyakazi wangapi?
Nilisoma sehemu (stand to be corrected) kuwa MeTL ndio mwajiri mkubwa na ameajiri wafanyakazi wasiozidi 30,000 kwenye kampuni zake zote. Sasa hawa jamaa wataajiri vipi watu 100,000 (laki moja)!?
Power Mabula anaendelea na Matangazo ya maonyesho yake. Nyote mnakaribishwa.
Atavuta pikipiki tisa kwa nywele zake, scania itapita juu ya kifua chake, atageuza mtu kuwa chura.
Shime akina baba na akina mama, vijana kwa wazee fikeni bila ya kukosa
 
1477057441650.jpg
1477057521300.jpg
 
Kiwanda cha kuzalisha tani 200000 kwa mwaka kuajili watu 100000 tunarudia makosa yaleyale. Lazima kife kama vingine. Maana running cost ni kubwa due to over employment
 
Hapo juu nimechomoa sehemu ya kabrasha ya mpango wa mifuko ya jamii kujenga viwanda. Baadhi ya mambo yameshatekelezwa tayari hata wajumbe tumekosa la kuhoji.
 
Back
Top Bottom