Mifuko ya hifadhi ya jamii yaanza kujenga viwanda

Mifuko ya hifadhi ya jamii yaanza kujenga viwanda

Ilishatabiliwa tokea mwanzo kuwa kwa Magufuli kila goti litapigwa
 
Kagera Sugar au Mtibwa wanazalisha tani ngapi na wameajiri wafanyakazi wangapi?
Nilisoma sehemu (stand to be corrected) kuwa MeTL ndio mwajiri mkubwa na ameajiri wafanyakazi wasiozidi 30,000 kwenye kampuni zake zote. Sasa hawa jamaa wataajiri vipi watu 100,000 (laki moja)!?
Watoto wa wajomba ni wengi lazima tugawane keki ya nchi. Hujiulizi kwa nini TTCL haiwezi kushindana? angalia waajiriwa wake.
 
Hizi pesa zetu hatujapeleka zijenge viwanda ni akiba yetu na mambo ya kuzitumia kujenga viwanda si sahihi hata kidogo nafuu wamkopeshe Mengi na Manji ndio wajenge viwanda.
Mkuu leo nimesikia kwenye magazeti wakisema serikali imerejesha fedha ilizokopa kwenye mifuko ya jamii kiasi cha bilioni 700+ japo haijamaliza zote ina maana wemerejesha na kuchukua tena wakajengee viwanda??serikali inaandaa mazingira mazuri kwa wawekezaji mara inataka kujenga yenyewe??au wanataka kujikumbusha Enzi hizoo serikali ilimiliki viwanda vikafa vyote kifo cha mende.???
 
Ni specialization. Kila mkoa unatakiwa ku specialize kwenye eneo moja au mbili tu. Kwa mfano mikoa ya Mwanza, Simiyu, Shinyanga na Geita wata specialize kwenye viwanda vya bidhaa zitokanazo na pamba na ng'ombe. Tabora tumbaku, Kigoma mawese, Kagera bitoke & kahawa, Pwani magari & trekta nk nk. Kila mkoa na wilaya zitakuwa na viwanda vya aina yake. Nchi ya viwanda ifikapo 2025.
Na mkoa wa katavi?
 
KWA SABABU NDIO WANAO WAAJIRI.

Hivyo viwanda vitaishia kununuliwa na akina Manji kwa bei za kutupa kabisa
kweli kabisa....serikali ingebaki kama regulator,wawaachie akina bakhresa

kkununua bahasha mpaka bajeti ya bunge,full urasimu
 
Mifuko ya hifadhi ya jamii imeanza mikakati ya kujenga viwanda ambapo kiwanda cha sukari kitajengwa Morogoro chenye uwezo wa kuzalisha tani 200,000 kwa mwaka na kuajiri watu 100,000.

Pia kuna viwanda vya kutengeneza mafuta ya alizeti na usindikaji wa nafaka mahindi ambavyo vitajengwa Dodoma na Iringa




Hongera. Magufuri na timu yako. hakika uongozi wako ni wa kutimiza ahadi. Hii ndivyo inatakiwa kwamba Rais anataka nini na exactly ASAP maagizo yanatekelezwa. Big up!!
 
Sidhani kama haya ni majukumu yao kwani kulipa tu mafao ya wastaafu na kuyaboresha ni shida tupu! Wao wangetoa mikopo ya ujenzi wa viwanda kwa kupitia benki zao , mfani benki ya Azania ambayo inamilikiwa na Nssf na Ppf wakopaji waende kule wao wabaki na kazi yao KUU. tatizo wanakimbilia maeneo ambayo ni ya 'kimaslahi' binafsi ie ....%
 
Iki cha Alzeti kwann kisijengwe Singda?
Dodoma ni center ya alizeti saiv kati ya singida na manyara.maana mkoa wa manyara hasa kiteto wamekuwa wakulima wazuri kuzid wa singida kiasi cha alizet kuuzwa bei chini zaidi na pia watu wa singida wamekuwa wakienda kibaigwa kununua alizeti kipeleka singida kwa wingi
 
Ni muhimu sana sana mifuko ya hifadhi ya jamii iwekeze kwa makini sana sababu wengi wanategemea hapo - isiwekeze kisiasa bali bale penye mafanikio na kukuza mfuko muhimu uchumi uwe mbele.
 
Kagera Sugar au Mtibwa wanazalisha tani ngapi na wameajiri wafanyakazi wangapi?
Nilisoma sehemu (stand to be corrected) kuwa MeTL ndio mwajiri mkubwa na ameajiri wafanyakazi wasiozidi 30,000 kwenye kampuni zake zote. Sasa hawa jamaa wataajiri vipi watu 100,000 (laki moja)!?
Kuzaliasha ajira laki moja inamaanisha watakaojairiwa kiwandani na wale waliopo kwenye mnyororo wa thamani ya uzalishaji sukari ambao hawapo likked na kiwanda moja kwa moja
 
Kuzaliasha ajira laki moja inamaanisha watakaojairiwa kiwandani na wale waliopo kwenye mnyororo wa thamani ya uzalishaji sukari ambao hawapo likked na kiwanda moja kwa moja
Well, basi tunaweza kusema 95% ya watanzania wameajiriwa kwa sababu kila mmoja anaingiza kipato japo kinakuwa sio direct kutoka kwa mwajiri, Ndivyo unataka kusema mkuu!?
 
Ni jambo jema kama hawa jamaa wamejiandaa kuviendesha. Kwa uzoefu wangu hawa mifuko ya kijamii hawana hata uwezo wa kuendesha majengo yao na badala yake wanayakabidhi kwa makampuni binafsi kama knightfrank ili wayaendeshe. Sijui kwanini wanawaachia wengine na si wao. Sasa kama kuendesha majengo kwa wapangaji hawawezi, sijui viwanda watafanyaje. Viwanda ni sehemu iliyokaa kiufundi zaidi na ndiko teknolojia zinakobadilika kila mara. Tusije kujenga majengo tukashindwa kuviendesha. Na kama ni uwekezaji wa viwanda, wasiwaze kujenga tu bila kuwaza watakavyoviendesha.
 
Huyo Yehodaya ni moja ya wanaccm wanaoamini serikali iko sawa kwa 100%.Hivi anafahamu kwamba mpaka sasa alizeti tumeweka stoo kwa kukosa soko? Watu wameuzia wakenye na wachina bado alizeti imefurika.Tunahitaji kiwanda kikubwa chenye uwezo wa kupandisha bei ya zao la alizeti.Eti unaweka ramani, unajua mafuta tunauza Nairobi na Rwanda.Acha siasa ongea ukweli.
 
Huwezi kufikia uchumi wa kati kwa kulundika kila kitu sehemu moja.Kosa lililofanywa la kuweka kila kitu Dar,linaenda kujirudia.Tunaona UDOM ilivyochochea maendeleo Dom.Hivyo vitu kama hivyo vinapaswa kufanyika Nchi nzima ili uchumi usitegemee sehemu moja.
 
Back
Top Bottom