Miembe ya kisasa..

Kwetu uswahili mwembe wa namna hiyo utakuwa mtunzaji tu walaji watakuwa ni wapita njia.Afadhali hii mirefu mtu akirusha jiwe mbwa atampa fundisho.
 
special for short ppl...lol........aisee hata home tuna mwembe kama huo ila maembe yake siyo matamu kivile
 
kama walivyosema wenzangu hii miembe iko mingi hapa Tz. mimi kwa mara ya kwanza niliiona pale SUA morogoro hapa DAR kaulizie sehemu ya Kinondoni barabara ya kwenda leaders kutokea makaburini
 
Wajameni seriously natafuta hii mbegu mwenye uhakika na upatikanaji wake anijuze.

Ipo mbona sehemu nyingi nimenunua nimepanda kwenye kiwanja changu bei m1 ni sh 3000 kuna dodo bolibo bei ni moja tu nenda wanapouza miti sehemu yeyote unapata wao wanaitoa sua kwa sababu kule ndo kuna wataalamu wanafanya budding
 
Ngoja na mimi nichangie kidogo hapa, kwa wanaohitaji serious naweza kuwasaidia cha kufanya, kwanza kuna aina tano za embe za jinsi hii zinazozaa vizuri ukanda wa mkoa wa Pwani/Dar/Moro, hizi ni kent, Red indian,Alfonso, Apple mango, ya tano nimesahau kidogo. Kwa hiyo ni muhimu kujua unataka aina ipi.

Kwa walioko Dsm mitaa ya mikocheni, kipo kitalu cha uhakika,kwa maana ya no chakachua, ukihitaji ni-PM nikupe maelezo. Pale SUA yupo rafiki yangu ambaye mimi nimechukua kwake mara kadhaa, naweza kukusaidia. Bagamoyo pia kipo kitalu cha kuaminika. Hawa wa mitaani kama pale Yenu Bar Ubungo, wanaweza kukuuzia aina moja tu, na yenyewe ikawa feki.

Tahadhali,miche hii ni dhaifu sana siku za mwanzo,inahitaji uangalizi sana,tumia mbolea ya kutosha,sio ya kuku. Naomba niishie hapa niwahi lunch.
 
Malila ni kweli aina ya maembe yapo mengi inategemea unahitaji aina gani.Kama kuna mdau anataka aniPM ninazo aina zote.

Ngoja na mimi nichangie kidogo hapa, kwa wanaohitaji serious naweza kuwasaidia cha kufanya, kwanza kuna aina tano za embe za jinsi hii zinazozaa vizuri ukanda wa mkoa wa Pwani/Dar/Moro, hizi ni kent, Red indian,Alfonso, Apple mango, ya tano nimesahau kidogo. Kwa hiyo ni muhimu kujua unataka aina ipi.

Kwa walioko Dsm mitaa ya mikocheni, kipo kitalu cha uhakika,kwa maana ya no chakachua, ukihitaji ni-PM nikupe maelezo. Pale SUA yupo rafiki yangu ambaye mimi nimechukua kwake mara kadhaa, naweza kukusaidia. Bagamoyo pia kipo kitalu cha kuaminika. Hawa wa mitaani kama pale Yenu Bar Ubungo, wanaweza kukuuzia aina moja tu, na yenyewe ikawa feki.

Tahadhali,miche hii ni dhaifu sana siku za mwanzo,inahitaji uangalizi sana,tumia mbolea ya kutosha,sio ya kuku. Naomba niishie hapa niwahi lunch.
 
Huchukua takibrani miaka 3 ndio uanze kula maembe ila inategemea na utunzaji kwani yahitaji maji kipindi cha mwanzo.mimi nilinunua miche miwili sabasaba mwaka 2009 banda la mali asili,ikaanza kutoa maua 2011 ila siku bahatika kula embe yalipukutika na vidaka kuanguka,mwaka jana yalitoa pia ila nikabahatika kupata embe 2 kabla hayajaiva wapita njia wakaiba moja nikaamua lililobaki kulichuma na kula bichi!nilichogundua juu ya miche hii inashambuliwa sana na wadudu hasa nzi ambao hufyonza embe zikiwa ndogo na kufanya kuanguka kabla ya wakati wake.Hivyo elimu juu ya utunzaji inahitajika sana wakati umeanza kuweka maua!
 
Ngoja na mimi nichangie kidogo hapa, kwa wanaohitaji serious naweza kuwasaidia cha kufanya, kwanza kuna aina tano za embe za jinsi hii zinazozaa vizuri ukanda wa mkoa wa Pwani/Dar/Moro, hizi ni kent, Red indian,Alfonso, Apple mango, ya tano nimesahau kidogo. Kwa hiyo ni muhimu kujua unataka aina ipi.

Kwa walioko Dsm mitaa ya mikocheni, kipo kitalu cha uhakika,kwa maana ya no chakachua, ukihitaji ni-PM nikupe maelezo. Pale SUA yupo rafiki yangu ambaye mimi nimechukua kwake mara kadhaa, naweza kukusaidia. Bagamoyo pia kipo kitalu cha kuaminika. Hawa wa mitaani kama pale Yenu Bar Ubungo, wanaweza kukuuzia aina moja tu, na yenyewe ikawa feki.

Tahadhali,miche hii ni dhaifu sana siku za mwanzo,inahitaji uangalizi sana,tumia mbolea ya kutosha,sio ya kuku. Naomba niishie hapa niwahi lunch.

Mkuu,ninahitaji mbegu hii mkuu ingawa sina mapana sana ya aina ya mbegu stahiki,naomba unitumie details kwa huruma_david@yahoo.com tafadhali
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom