Mie nilidhani Mbowe tu ndio halipi kodi, kumbe hata Manji

Mie nilidhani Mbowe tu ndio halipi kodi, kumbe hata Manji

mwembemdogo

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2016
Posts
2,282
Reaction score
1,253
Nimeshtushwa na taarifa kuwa mfanyabiashara mkubwa na Diwani wa Mbagala CCM na Mwenyekiti wa Klabu bingwa ya soka Tanzania na mmliki wa Quality Group Mh. Yusuf Manji nae halipi kodi. Tunakuomba Diwani Manji hebu lipa hiyo Trilioni 1 unayodaiwa ili nchi ipige hatua kimaendeleo.
====================
Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi Dar Es Salaam imemuru kampuni ya Quality Group inayomilikiwa na mfanyabiashara maarufu Yusuph Manji na wenzake kuondoka kwenye jengo la Quality Plaza na kulipa kodi ya pango wanayodaiwa tangu mwaka 2007 hadi sasa
Fedha hizo zitalipwa kwa mlalamikiwa wa kwanza kwenye kesi hiyo, kampuni ya Image Properties and Estate ambayo ni wakala wa mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) unaomiliki jengo hilo
Uamuzi huo ulitolewa jana na msajili wa mahakama hiyo Frank Mahimbali kwa niaba ya jaji John Mgetta katika kesi mbalimbali zilizofunguliwa na Kampuni ya Quality Group kupinga kulipa kodi ya jengo hilo
Kesi hizo zilitokana na mdai Quality Group kukimbilia mahakamani kila alipokuwa akipelekewa notisin ya kuhama katika jengo hilo na na mlalamikiwa wake, Kampuni ya Image Properties and Estate
Msajili wa hizo amesema kesi ya iliyotolewa hukumu ni ya mwaka pamoja na kutaja kesi ya msingi ya mwaka 2009 ambayo ilitolewa hukumu
Aidha mahakama iliamuru PSPF kulipa mlalamikaji namba moja , Quality Group shilingi milioni 100 kama hasara ya jumla iliyopata kampuni hiyo baada ya kuzuiliwa kuhamisha vitu vyake ndani ya ofisi hizo
 
Na bado ataambiwa alipe kidogo kidogo,
 
Mbele kwa mbele haka kawimbo katamu sana aisee
 
Hakuna wa kumgusa manji kwenye Suala Hilo

OVA
 
Yanga wamlipe hela zake ili akalipe kodi, maana Yanga ndo imemfilisi
 
Trillion 1 subiri nipate maelezo kwanza hiyo Pesa ndefu aiseeee
 
Hakuna wa kumgusa manji kwenye Suala Hilo

OVA

Katulizwa kwenye Coco beach aliponunua kihalali, kapigwa mpka kaamua kununua gazeti la Jambo leo kupingana na serikali wewe unasema nini, na bado atashughulikiwa kwa mujibu wa sharia, washirika wake kibiashara akiwepo rais mstaafu mmoja wanafahamu hili. Ngoja uone, kama ana madhambi na manyangunyangu yake yote yatashughulikiwa. Hivi rais anaaposema watu wanaficha hela na kuwaahidi kuwashughulikia wewe unafikiri anawazungumzi akina nani?
 
Alipoona agizo la Lukuvi kunyang'anya viwanja visivyoendelezwa, akaitumia Yanga ionekane kama ameigawia eneo kubwa kule Kigamboni, kumbe amejigawia kwa kuwa anaikodi miaka kumi. Yanga wenyewe hawajui!
 
CCM isiyolipa kodi ndiyo inalifilisi taifa hili. MaCCM ni zaidi ya magaidi.
 
Back
Top Bottom