Midege ya jeshi inayozunguka angani

Midege ya jeshi inayozunguka angani

Mshobaa

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2013
Posts
1,716
Reaction score
680
Heshima kwenu waungwana,
kwa mliopo dar wengi wenu mtakua mmeshuhudia ndege tatu za jeshi zikiwa zinarushwa kwa kufuatana kwa kasi sana angani, mimi swali langu ni je gharama zake zina faida au tija kwa taifa? Je mafuta yanayotumika sio kodi ya jasho la watanzania? Hebu tupia maoni yako hapa
 
Kuna vitu vingine ni lazima vifanyike pasi kuhitaji ridhaa ya mtu mmoja mmoja...
 
Hahaaa umefikiria nini mkuu? Mi tangu mwanzo wa mwezi wa 11 naziona tu zinapiga misele angani, hasa tangu yule askariiwa mwisho Mtz kuuawa na M23...aagh watajua wenyewe bhana
 
kwa hiyo hutaki ziruke? Tutajuaje km nzima.
 
Sio kila jambo linalofanywa na Serikali basi lazima upinge. Mbona hukuuliza kwanini zimenunuliwa kwa Kodi zetu???
Embu ulizia Nchi zilizoendelea harafu watakwambia wao ndege wanarusha lini hadi lini, mimi ninavyojua wenzetu kila siku wanafanya haya mazoezi tofauti na sisi mpaka sikukuu.
Kumbuka hili ni Jeshi la Ulinzi la Watanzania ambao wamekufanya wewe uwe huru muda huu kwenye Simu/PC yako unaandika vitu kama hivi.
 
Heshima kwenu waungwana,
kwa mliopo dar wengi wenu mtakua mmeshuhudia ndege tatu za jeshi zikiwa zinarushwa kwa kufuatana kwa kasi sana angani, mimi swali langu ni je gharama zake zina faida au tija kwa taifa? Je mafuta yanayotumika sio kodi ya jasho la watanzania? Hebu tupia maoni yako hapa
mbona timu za mpira zikifanya zoezi amuulizi au kushangaa kwa nini zinafanya,,,?? Ndugu vita is like a game no practice U will always loose let them practice I order to be fit 4 the battle viva jwtz viva air defences
 
Jwtz wakifanya vizuri Congo,Darfur tunawasifia. Unadhani jeshi bila mafunzo/mazoezi wanaweza kushinda vita?

kabisa Mkuu, naona kasumba ya kupondea kila kitu inazidi kukomaa, hata mabunduki huwa yanatestiwa huko Police Posts kwa kuweka risasi halisi na kufyatua angani........ wacha wazee wazima wale tizi.
 
kwa hiyo ulitaka zivundikwe ndani?kumbuka izi jet ni kama mashine yoyote ile usipoiwasha na kuitesti mara kwa mara unategemea nini?
 
Marekani ilikua imefunga baadhi ya idara kwa kusubiria bajeti .sisi wafanyakazi wengine hawajapewa chao tare 33 sasa tunarusha ndege ahahahahah BRN
 
Back
Top Bottom