Moja ya vyuo hivyo mifano yake hai ipo hapa hapa Dar,kuna baadhi ya vyuo vya Hoteli na uhazini vipo Parking ya Avalon na mitaa ya Mansfield,Nkrumah na vitongoji vya K'koo,Sinza,K'nyama... Sijui ila ni bomu la muda litalipuka siku moja...
Kwa maoni yangu, Suala ubora wa chuo na credibility yake ni jambo moja, na michuzi kupokea tangazo ni jambo jingine. Kwenye tangazo, sio jukumu la mpokeaji kufanya vetting ya chuo, hilo ni jukumu la mtumiaji huduma hiyo. Ni kawaida kukuta matangazo ya hivi vyuo feki na non accredited kwenye magazeti na vyombo vya habari vya home na sio jukumu la chombo husika kuulizwa.
Hivyo ni sawa kwa michuzi kupokea tangazo lolote.
Ni makosa kusema Michuzi hahusiki kwa tangazo..Kupokea tu matangazo bila kujua undani wake na kuyabandika bila kujiridhisha ni dalili ya u-robot.
WoS amesema vizuri 'buyer be ware' kosa la Michuzi lipi?. Hivi kweli ni jukumu la mtangazaji kufanya vetting?. Kuna sheria ya liability kwenye matangazo mipaka ya sheria hii inaishia kwenye vyakula na madawa, mtu akithirika ndipo mpaka aliyetangaza atawajibika ndio maana huwezi kuona matangazo ya madawa ama mahospitali.Kwa tangazo la chuo, hakuna liability yoyote kwa media inayotangaza hata kama hicho chuo ni non existance, fake ama un accredited.Kwenye hili la matangazo, nasimama na Michuzi sio kwamba he is doing the right thing, bali he is making his good clean money huku akiisaidia jamii kuihabarisha, kulikoni wengine wetu mimi nikiwemo, tunajisikitikia na umasikini wetu tukishindwa kufanya yatupasayo kufanya, tuishia kuwalaumu wengine wafanyao vitu vyao.Naomba kudeclare conflict of interest. Mimi ni fan mkubwa wa globu ya jamii.
Ntamwambia Invisible asikubali kuitwa Robot,,,,, hii imekaa vibayaNo wonder nchi yetu kila kitu kinaenda shaghalabaghala kwa sababu ya watu kama wewe mnaoukubali u-robot. Robot hatumii akili kuchuja kitu kinachokuja mbele yake, yeye anapokea tu instructions na kuzitekeleza ..thats why..
Ntamwambia Invisible asikubali kuitwa Robot,,,,, hii imekaa vibaya
Sio kila kitu unahitaji kutumia akili, mambo mengine kweli ni kirobt robot na hata watu wenye mtindio, nao pia wana uwezo wa kuchuja mema na mabaya kwa jamii kutegemeana na mtindio wao umeathiri idara gani.Yaani unarejea tena kuuliza kosa la Michuzi ni lipi? No wonder nchi yetu kila kitu kinaenda shaghalabaghala kwa sababu ya watu kama wewe mnaoukubali u-robot. Robot hatumii akili kuchuja kitu kinachokuja mbele yake, yeye anapokea tu instructions na kuzitekeleza ..thats why..
Huo ni mfano wa kutosha kuwa chuo hicho hakifai kusoma,huwezi kuwa na chuo kina intake sita kwa mwaka na digrii unapata within two years.ukitizama website ya chuo unajua kuna something ..... kwenye hicho chuo.fanyeni utafiti kabla ya kulipa au kujisali na vi college kama hivi.hata ukitaka kwenda vyuo vikuu pata ushauri wa vyanzo mbalimbali kama www,timesonline.co.uk au tizama universities ranking etc.
chuo kama kiko serius kisingepita kwa michuzi blog kinakwepa kodi ya kujitangaza. unajua gazeti kama la ulaya gharama za matangazo ni kubwa hivyo wanavamia kwa michuzi.
Michuzi anatakiwa awe makini kwenye matangazo kwani anaowapoteza ni watanzania wenzake.
huko mbele tutakuwa na wasomi wenye MBA ambazo hazina misingi mizuri kama hizi za vyuo hivi.
TATIZO SIYO HIVYO VYUO.Hivi vyuo sidhani viko zaidi ya kufanya biashara.Wenye kusoma huko wanasafari ndefu ya kuelimika/kupata taaluma stahiki.BUYER BEWARE!
Vyuo hivyo si vina Mamlaka zilizo juu yake zenye kutakiwa kuregulate na kuhakikisha vinaperform 2 the required standards?Vyuo vingi vimeanzishwa siku hizi lakini yet wanataaluma hafifu.