Michirizi ya Damu

Michirizi ya Damu

SEHEMU YA 117

Meli ikakaa siku ya kwanza, Mzee Ahmed alikuwa na kazi ya kumpelekea chakula, ikakaa siku ya pili na siku ya tatu ilipoingia ndipo zamu yao ilipofika. Mzee huyo hakuwa na hofu, hakudhani kama polisi wangeweza kuingia mpaka katika chumba kile kwani haikuwa kawaida yao.

Siku hiyo, mbali na kuwatafuta watu waliokuwa wakizamia, ilikuwa ni lazima wamtafute na Fareed. Walihisi kwamba mtu huyo angeweza kutumia nafasi hiyo kutorokea nchini Cyprus ambapo hakukuwa mbali kutoka katika bandari hiyo.

“Leo ni tofauti na siku nyingine,” alisema mwanajeshi mmoja.
“Kivipi?”
“Tutapekua kila kitu katika meli yako. Mbali na watu wanaozamia, pia kuna mtu tunamtafuta. Ni mtu hatari sana,” alisema mwanajeshi huyo.

“Ni nani? Kafanya nini?”
“Amefanya mauaji ya bilionea!”
“Mauaji ya bilionea? Eeh! Ndiyo kwanza nasikia leo,” alisema Mzee Ahmed.

Moyo wake ulikuwa na hofu, hakujua kama mtu aliyempakiza kwa ajili ya kumvusha kwenda nchini Uturuki ndiye ambaye alikuwa akitafutwa.

Wanajeshi wanne wakafika mahali hapo, huku wakiwa na bunduki zao, wakaingia ndani ya meli hiyo.
 
Back
Top Bottom