Michirizi ya Damu

Gud axee
 
SEHEMU YA 104

Wakafanikiwa kuona kila kitu, tangu alipoingia na mwanaume huyo lakini kilichowashangaza ni kwamba wakati wa kuondoka, aliondoka na mwanaume mwingine, walitamani kumfahamu lakini walishindwa kwa kuwa alivalia kofia kubwa ya Marlboro.

“Ni nani huyu?” aliuliza polisi mmoja.
“Hatujui!”
“Kitu cha kwanza ni kumtafuta huyu mwanamke tutajua tu!” alisema polisi mmoja.

Hakukuwa na muda wa kupoteza, wakaanza kumtafuta katika hoteli mbalimbali. Walijua kwamba kama hilo lilikuwa jina lake basi ni lazima angekuwa ameliandikisha katika hoteli aliyokuwa amefikia hapo Cairo.

Baada ya saa kadhaa, wakagundua kwamba mwanamke huyo alikuwa katika hoteli moja hapo Cairo, wakaanza kufuatilia huko kutaka kujua kama alikuwepo. Walipofika, wakaelekea mpaka mapokezini ambapo wakaulizia na kuambiwa kwamba alikuwepo ndani na mwanaume mwingine hivyo kwenda huko.

“Cha kwanza ni kuwakamata wote wawili, ikishindikana basi tuwapigeni risasi,” alisema polisi mmoja kwani kwa kile kilichotokea, kilikuwa aibu kubwa.

**** Wote walichoka hoi, Fareed alimwangalia Maria, hakummaliza. Hakuwahi kukutana na mwanamke kimwili, huyo ndiye alikuwa mwanamke wake wa kwanza. Alijisikia kuwa na nguvu kubwa, alijua kucheza na mwanamke, alijua maeneo ambayo yangemtetemesha mwanamke yeyote yule.

Maeneo hayohayo ndiyo aliyoshughulika nayo, alifanikiwa kwa kiasi kikubwa, Maria alipagawa, alikuwa hoi huku akidiriki kusema kwamba kwa kile alichokuwa amekifanya Fareed, hakuwa amefanyiwa na mwanaume yeyote yule.

Fareed akasimama na kwenda kuoga, bafuni, alikuwa na wasiwasi, alihisi kabisa kwamba inawezekana polisi wangefika katika hoteli hiyo kwani alipokuwa ameingia ndani ya hoteli ile, kamera zilimuona na kumgundua kwamba alikuwa nani.

Alifikiria kutoroka siku hiyohiyo, hakutaka kulala mahali hapo, ili maisha yake yaendelee kuwa salama na akamilishe kazi zake zote ilikuwa ni lazima kutoroka hapo hotelini haraka iwezekanavyo kabla mambo hayajaharibika.

Alioga harakaharaka, alipomaliza, akatoka na kuelekea kitandani. Akamshika kiuno Maria na kuanza kukipapasa, hakuishia hapo, akaupeleka mdomo wake katika kiuno kile na kuanza kukifanyia utundu.
 
SEHEMU YA 105

Maria akaanza kutoa miguno ya kimahaba, Fareed alifanya hivyo kwa lengo la kumpagawisha halafu amuache, akamvutia kwake, akaupeleka ulimi wake katika kitovu cha msichana huyo na kuendelea kumfanyia utundu huku mikono yake ikitalii katika kifua chake.

Maria alichanganyikiwa, alijiona akiwehuka, akaondoka katika ulimwengu halisi na kuingia katika ulimwengu ambao haukuwepo kabisa ulimwenguni. Fareed hakuacha, aliendelea kwa dakika tatu kisha akamuacha Maria na kumwangalia machoni.

“Endeleaaaaaaa…” alisema Maria huku akimvuta Fareed juu yake.
“Nenda kaoge kwanza!”
“Jamaniiiiiii!”

“Leo mimi ni wako! Yaani hapa huchomoki,” alisema Fareed huku akiupitisha mkono wake shingoni mwa msichana huyo, akakichukua kidole chake cha mwisho na kukiingiza sikioni mwa Maria.

“Ishiiiiii..aagghhuu..” alilalamika Maria kimahaba.
“Nenda bafuni kwanza!” alisema Fareed.
Japokuwa alikuwa amezidiwa lakini hakutaka kupingana na Fareed, hapohapo akasimama na kwenda bafuni kuoga.

Huku nyuma Fareed akavaa nguo harakaharaka, alipomaliza, akachukua kibegi chake, akaufungua mlango na kutoka.

Alitaka kushuka kwa kutumia ngazi lakini aliona kama angechelewa, hivyo alichokifanya ni kupanda lifti. Wakati yeye akishuka kwenda chini ndiyo muda ambao polisi walipanda kwenda juu, yaani kwa kifupi, walikuwa ndani ya lifti mbili tofauti na walikuwa wakipishana kwa wakati mmoja.

**** Lifti ikashuka mpaka chini, Fareed hakutaka kubaki mahali hapo, kile kilichomfanya kujenga urafiki na Maria alikikamilisha na hivyo alitaka kuondoka hapo haraka iwezekanavyo.

Alipofika chini, akaanza kutembea kwa mwendo wa kawaida, hakutaka kuonekana kuwa na wasiwasi kwa kuamini kwamba kama angekuwa katika hali hiyo ingekuwa rahisi kwake kukamatwa hata na walinzi waliokuwa katika hoteli hiyo.

Hakukuwa na polisi mapokezini kitu kilichomfanya kutembea kwa uhuru mpaka nje ambapo akachukua teksi na kuondoka mahali hapo.

Moyo wake ulikuwa na furaha tele, alifanikiwa kwa kile alichokuwa amekipanga na kitu alichokifikiria kwa kipindi hicho ni kumuua bilionea Belleck ambaye hakujua alikuwa wapi ila kama angekwenda katika ofisi yake moja iliyokuwa nchini Marekani, angejua mahali alipokuwa kipindi hicho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…