Michirizi ya Damu

Michirizi ya Damu

SEHEMU YA 14

Dar es Salaam, Tanzania *
*
“Theresa! Huu ni mwaka wetu wa pili katika ndoa yetu, ungependa tufanye nini?” aliuliza mwanaume mmoja aliyeitwa kwa jina la Godfrey Kidatu, alikuwa kijana wa miaka thelathini na mbili, alikuwa na mwili uliojazia kidogo, kwenye kidevu chake kilikuwa na ndevu chache kidogo.

Alikuwa amekaa katika meza ya chakula pamoja na familia yake katika Ufukwe wa Miladiva. Mkewe, Theresa alikuwa pembeni huku wakiwa na mtoto wao aliyekuwa na miaka miwili. Kwa jinsi walivyokaa kimahaba, kila mtu aliyekuwa katika ufukwe huo uliokuwa jijini Dar es Salaam alikuwa akiwaangalia kwani walionekana kupendeza na kumvutia kila mtu.

“Tuna mengi ya kufanya ila kwanza haka katoto kaanze shule ya chekechea,” alijibu Theresa huku akimwangalia mume wake.
Godfrey Kidatu alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa na maisha mazuri jijini Dar es Salaam, alikuwa mmoja wa wafanyabiashara wakubwa waliokuwa na mafanikio makubwa katika umri mdogo.
Alikuwa kijana mcheshi, mwenye biashara nyingi zilizomuingizia kiasi kikubwa cha pesa kila siku. Maishani mwake, alikuwa na kila kitu, alikuwa na uwezo wa kufanya kitu chochote kile kwa sababu tu alikuwa na fedha.

Alijenga jumba kubwa Masaki, alikuwa na boti mbili zilizokuwa zikifanya safari kwenda katika Visiwa vya Zanzibar, alikuwa na mabasi makubwa yaliyokuwa yakienda mikoani, kwa kifupi, maishani mwake hakuwa na shida na kila kitu alichokifanya kilimaanisha pesa.
Aliamua kutoka na mkewe kwenda katika ufukwe huo, hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza ndani ya mwaka mmoja.

Alitamani sana kuwa na familia yake karibu lakini kutokana na majukumu aliyokuwa nayo, hakuwa akipata nafasi hiyo hata kidogo.
Siku hiyo alipata nafasi na kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kutoka na familia yake hiyo ambayo ilikuwa kila kitu.

Walikaa na kuzungumza huku kila mmoja akionekana kuwa na furaha tele, walitaniana na kufanya mambo mengi ya kimahaba, wakapanga mipango yao mengi, kwa kifupi, kila mmoja alitamani kumfurahisha mwenzake siku hiyo.
SEHEMU YA 18

Baada ya kupita miezi sita tena huku akiwa barani Asia ndipo akatumiwa meseji katika akaunti yake ya WhatsApp, harakaharaka akaifungua na kuisoma, alitumiwa kupitia namba ngeni na ujumbe aliotumiwa ulikuwa mfupi tu uliosomeka ‘Miladiva’.

Kitu cha kwanza kabisa kumjia kichwani mwake kilikuwa ni kukumbuka kitu kilichotokea kwenye ufukwe huo. Alikumbuka kwamba mara ya mwisho kwenda katika ufukwe huo ni miezi kadhaa iliyopita ambapo alikwenda pamoja na familia yake.

Hakujua ujumbe huo ulimaanisha nini lakini alipouliza, akatumiwa ujumbe mwingine mfupi uliosomeka ‘Nipigie’, hapo ndipo akakumbuka, picha ya mwanaume tata yule aliyemwambia ampigie ikamjia kichwani mwake, hakutaka kuchelewa, akamtumia meseji ya kulalamika kwamba ilichukua muda mrefu mpaka kumtafuta.

“Nilikuwa bize sana. Ila nimekumiss baba watoto,” aliusoma ujumbe huo, mwili ukamsisimka.
“Kweli?” aliuliza.
“Ndiyo! Naomba nikuone jamani!” aliusoma ujumbe huo ambao uliambatanishwa na sauti iliyorekodiwa, alipoifungua, ilikuwa sauti ya mwanaume huyo iliyokuwa ikilalamika kimahaba, tena mbali na hiyo, alimwambia kwamba alihitaji mpenzi wa kudumu kwani wapenzi wote aliokuwa nao waliishia kumtenda tu, hawakuwa na mapenzi ya dhati.

“Nipo kwa ajili yako! Nitakulinda mpenzi! Naomba kuonana nawe nikifika Tanzania,” alimwambia.
“Kwani upo wapi?”
“Nipo Kuwait, kuna kitu nimefuata.”
“Basi sawa baba watoto! Nakupenda!”
“Nakupenda pia. Mwaaaaah!”
“Mwaaaah!”

Wakaagana, Godfrey hakuamini kama aliwasiliana na mwanaume tata huyo, alibaki hotelini huku akiwa amechanganyikiwa kwa furaha, aliinuka na kuanza kurukaruka, alikuwa na hamu ya kupata mawasiliano na mwanaume huyo na mwisho wa siku alipigiwa na hivyo kuwa na namba yake.

Wakati akiwa anafurahia akasikia simu yake ikilia na alipoifungua akakutana na picha za kihasarahasara alizotumiwa katika akaunti yake ya WhatsApp ambazo zilimuonyesha mwanaume huyo akiwa katika mikao ya hatarihatari.

Japokuwa alikwenda Kuwait kukaa kwa wiki moja na kutakiwa kwenda nchini Uingereza lakini wiki moja akaiona kuwa kama mwaka, kila siku kazi yake ilikuwa ni kuangalia kalenda, hakukuwa na kipindi alichokiona siku kwenda taratibu kama kipindi hicho.
shunii mbona sehem ya 14-18 siioni
Mkuu ebu fatilia vizuri episode zote zipooo mwisho 20
 
".....piramidi moja lililokuwa katika Mji wa Giza uliokuwa nchini Misri..."

Kipande hiki kimefanya niache kuisoma hii story.

Ina maana sasa hivi hilo piramidi halipo tena Giza na mji wa Giza haupo tena Misri au?
 
".....piramidi moja lililokuwa katika Mji wa Giza uliokuwa nchini Misri..."

Kipande hiki kimefanya niache kuisoma hii story.

Ina maana sasa hivi hilo piramidi halipo tena Giza na mji wa Giza haupo tena Misri au?
Kamuulize Nyemo sasa mkuu
 
Back
Top Bottom