MICHEZO YA VYUO VIKUU CHINA-vichekesho TAnzania

Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,067
2,197
Michezo ya Universaide inafanyika huko China. Kuna habari za kuchekesha sana kuhusu ushiriki wa timu.


Tanzania maofisa watatu, wachezaji wawili
Kenya maofisa watatu, wachezaji 19
Uganda maofisa watatu, wachezaji zaidi ya 20
Rwanda maofisa 0, wachezaji


what can we tell from these figures?
 
Mkuu haiingii akili, maofisa wengi kuliko wachezaji sijui lengo la ushiriki ni kuhudhuria na kutazama au ni kucheza.
 
Mbona hata All africa game itayoanza msumbiji karibuni kuna mchezo wanapeleka viongozi wengi kuliko wachezaji. Hiyo ndiyo bongo bana
 
Wajameni waacheni nao waende wakabarizi, wizara ya michezo hakuna posho kama za Jairo...
 
Kama kuna Wizara isyopewa kipaumbele Bongo ni wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na idara zake. Sijui tumelogwa au vipi? Kwetu michezo ni subsidiary Hakuna kiongozi wala mbunge ambaye anajali hii idara. Ila kikipatikana kikombe lazima kwanza kiende kuhiji bungeni watu wapigiwe makofi na waandaliwe lunch au dinner! Inabidi tukubali kuwekeza kwenye michezo ili tuone matunda yake.Ni aibu kwa nchi kubwa kama TZ kupeleka viongozi 3 na wachezaji 2. Na sitashangaa miongoni mwa hao viongozi nikiskia kwamba wapo waliojisafirisha au kutembeza bakuli kwa mjomba na shangazi mkubwa ili walao wakahudhurie vikao vya vyama vyao ambavyo mara nyingi hufanyika sanjari na michezo. Lazima tuamke na kuwapa sapoti ya ukweli wachezaji wetu sio maneno tu. Lakini pia viongozi nao lazima wawajibike sio kubweteka na kusubiri kugombania safari ili wapate posho na kufanya shopping za vilaptop na kamera!
 
Masikini nchi yangu Tanzania kila mahali ni uozo, tuwaache wenzetu wenye akili waje watutawale. wakati sisi tuanang'ang'ania ufisadi wenzetu kenya wamasonga mbele, kama sikosei kenya inashika nafasi ya pili katika nchi zilizowekeza Tanzania, fikirini kwa makini jambo hili. Nawakilisha
 
Back
Top Bottom