UDOM yaanza kwa kishindo mashindano ya Mei Mosi

University of Dodoma (UDOM)

Public Institution
Joined
Feb 24, 2024
Posts
48
Reaction score
52
IMG_2334.jpeg

Timu ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) imeanza kwa mafanikio makubwa ushiriki wake katika mashindano ya michezo ya watumishi wa umma nchini Tanzania (Mei Mosi 2026), kwa kuibuka na ushindi wa kishindo katika mchezo wa kwanza.

Katika pambano la mpira wa wavu kwa wanaume lililochezwa leo, timu ya UDOM iliibuka na ushindi wa seti 2–0 dhidi ya timu ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), matokeo yaliyoonyesha uimara na maandalizi thabiti ya kikosi hicho.

IMG_2335.jpeg

Akizungumza mara baada ya ushindi huo, Mkufunzi Mwandamizi wa Michezo wa UDOM, Bw. Patrick Mwani. alisema mafanikio hayo yametokana na maandalizi ya kina pamoja na nidhamu ya hali ya juu ya wachezaji.

“Tumefanya maandalizi ya kutosha na wachezaji wameonyesha nidhamu kubwa uwanjani. Huu ni mwanzo mzuri, na tumejipanga kuendeleza kiwango hiki katika michezo inayofuata,” alisema Bw. Mwani.

IMG_2333.jpeg

Mashindano hayo ya kitaifa yanayofanyika mkoani Njombe yanaleta pamoja watumishi wa umma kutoka taasisi mbalimbali nchini, yakilenga kuimarisha afya, mshikamano na ushirikiano kazini kupitia michezo.

Mbali na mpira wa wavu kwa wanaume na wanawake, timu ya UDOM pia inashiriki katika michezo mingine ikiwemo bao, riadha, karata na draft, ikiwa na matumaini ya kufanya vizuri katika mashindano yote.

Ushindi huu wa awali unaweka msingi imara kwa UDOM katika harakati zake za kuwania nafasi za juu kwenye mashindano hayo ya Mei Mosi 2026.

IMG_2332.jpeg
 
Halafu mjibu malalamiko ya wanafunzi wenu. Siyo mnakuja kujisifia kwenye michezo, huku kwenye taaluma mkipuyanga.
 
View attachment 3574998
Timu ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) imeanza kwa mafanikio makubwa ushiriki wake katika mashindano ya michezo ya watumishi wa umma nchini Tanzania (Mei Mosi 2026), kwa kuibuka na ushindi wa kishindo katika mchezo wa kwanza.

Katika pambano la mpira wa wavu kwa wanaume lililochezwa leo, timu ya UDOM iliibuka na ushindi wa seti 2–0 dhidi ya timu ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), matokeo yaliyoonyesha uimara na maandalizi thabiti ya kikosi hicho.

View attachment 3575000

Akizungumza mara baada ya ushindi huo, Mkufunzi Mwandamizi wa Michezo wa UDOM, Bw. Patrick Mwani. alisema mafanikio hayo yametokana na maandalizi ya kina pamoja na nidhamu ya hali ya juu ya wachezaji.

“Tumefanya maandalizi ya kutosha na wachezaji wameonyesha nidhamu kubwa uwanjani. Huu ni mwanzo mzuri, na tumejipanga kuendeleza kiwango hiki katika michezo inayofuata,” alisema Bw. Mwani.

View attachment 3575002

Mashindano hayo ya kitaifa yanayofanyika mkoani Njombe yanaleta pamoja watumishi wa umma kutoka taasisi mbalimbali nchini, yakilenga kuimarisha afya, mshikamano na ushirikiano kazini kupitia michezo.

Mbali na mpira wa wavu kwa wanaume na wanawake, timu ya UDOM pia inashiriki katika michezo mingine ikiwemo bao, riadha, karata na draft, ikiwa na matumaini ya kufanya vizuri katika mashindano yote.

Ushindi huu wa awali unaweka msingi imara kwa UDOM katika harakati zake za kuwania nafasi za juu kwenye mashindano hayo ya Mei Mosi 2026.

View attachment 3575003
Kwanini hamja publish wafanyakazi bora wa Taasisi na Colleges kama wenzenu wote wa Taasisi za Umma na Vyuo?
 
Back
Top Bottom