*Bingwa kupatikana Jumapili
*Majimaji, Toto zashikilia ubingwa
Na Zahoro Mlanzi
TIMU ya Yanga jana imewapiga kumbo kileleni mabingwa wa Tanzania Bara, Simba baada ya kuifunga African Lyon Mabao 3-1 katika
mechi ya Ligi Kuu iliyopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na hivyo kuifanya kuongoza kwa tifauti bao moja.
Kwa matokeo hayo Yanga sasa inaongoza ikiwa na pointi 46, sawa na Simba isipokuwa vinara hao wamefungwa mabao saba na kufunga 26 wakati wapinzani wao wamefunga mabao 36 na kufungwa 15 hivyo kuifanya Yanga kuongoza kwa tofauti ya bao moja.
Katika mechi ya jana Yanga iliingia kwa uchu wa kufunga mabao ambapo katika dakika 11, Fred Mbuna aliunganisha kwa kichwa krosi iliyopigwa na Davies Mwape ambayo kipa Ivo Mapunda wa African Lyon aliipangua lakini hata hivyo mpira huo ulitoka nje ya lango.
Yanga ilirudi tena langoni mwa African Lyon ambapo dakika ya 18, Mwape aliachia kombroa kali akiwa nje ya 18 ambalo hata hivyo kipa Mapunda alilipangua na kupata maumivu yaliyomsababishia maumivu na mpira kusimama kwa dakika kadhaa.
Juhudi za Yanga kusaka bao lilizaa matunda dakika ya 32 baada ya Idd Mbaga kufunga baada ya kupokea pasi ya Mwape na kuwazidi ujanja mabeki wa Lyon na kuutumbikiza mpira wavuni.
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kuingia kwa nguvu na kufanikiwa kupata baoa la pili dakika ya 46 kupitia kwa Mwape ambaye alipiga shuti kali lililomshinda kipa Mapunda ambaye alijaribu kupangua lakini kutokana na kasi ya mpira ya alijikuta akiusindikiza wavuniu.
Dakika ya 61 Yanga ilifunga bao la tatu kupitia kwa Mbaga tena ambaye baada ya kupokea pasi ya Nurdin Bakari alikimbia na mpira na kukutana kipa Mapunda ambaye alimhadaa na kufunga bao kirahisi.
African Lyon ilipata bao lake la kufutia machozi dakika ya 78 baada ya beki Chacha Marwa, kujifunga wakati akiwa katika harakati za kuokoa mpira baada ya Benedicto Ngassa kuachia shuti kali lililokuwa likienda wavuni.
Dakika ya 88, Mbaga alipata dhoruba kali na kuzimia na kutolewa uwanjani kwa machela, baada ya kugongana na Zuberi Makame ambao walikuwa wakiwania mpira wa juu na nafasi yake kuchukuliwa na Razakh Khalfan.
1 Maoni:
Anonymous said... Yanga kuukaribia ubingwa itakuwa ni fundisho kubwa kwa wachezaji wa Simba kwani naona baada ya kutolewa na TP Mazembe wao walijiona kama ni bora sana kwa kucheza kwa bidii na walipoingia uwanjani kucheza na JKT Ruvu waliingia kwa zarau ya kwamba hawa JKT si kitu tuwafunga tu,Na JKT waliingia uwanjani kwa ari na nguvu ili waitoe nishai timu kubwa.Hili ni tatizo kubwa tu kwa simba
na wachezaji wetu wa kitanzania.Wanaposifiwa basi vichwa huwa vikubwa na kujisahau kwa sifa na matokeo yake wapoingia uwanjani wanashindwa kufanya walichotakiwa kufanya. April 8, 2011 1:40 PM
WASHIRIKI 23 kutoka sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam, wamejitokeza kushiriki katika mashindano ya kumtafuta 'Malkia wa Tabata, 'Miss Tabata 2011', ambalo
limepangwa kufanyika mwezi ujao.
Mratibu wa mashindano hayo, Joseph Kapinga alisema kuwa warembo hao walianza mazoezi tangu Jumapili kwenye Ukumbi wa Da West Park Tabata, Dar es Salaam.
"Warembo wetu tayari wameshaanza kufanya mazoezi pale pale Da' West Park kila siku kuanzia saa nane mchana hadi saa moja jioni," alisema mratibu huyo.
Aliongeza kuwa bado Kamati ya Mashindano hayo inawaomba warembo wenye sifa kujitokeza kwa wingi, ili hatimaye waweze kupata wawakilishi bora katika mashindano ya Kanda ya Ilala.
"Bado milango iko wazi, mrembo yeyote anayejiamini kwamba ana vigezo anakaribishwa. Tunataka mashindano ya mwaka huu yawe na ushindani zaidi," Kapinga alisema.
Kapinga alisema kuwa Kampuni yake ya Bob Entertainment, ambayo ndiyo inaandaa mashindano hayo imepanga kuandaa sherehe maalumu ya kuwatambulisha washiriki wote kabla ya kupanda ulingoni kuwania taji hilo.
Aliwataja warembo ambao tayari wameshajitokeza kuwa ni Marion Augustino (18), Neema Marwa (18), Esther Simon (18), Sweetylily Suleiman (21), Malaika Abdallah (18) na Theckler Benedict (19).
Wengine ni Happiness Emmanuel (18), Irene Jafari (19), Janeth Marandu (21), Shadya Ally (21), Victoria Amon (20) na Mgayo Salehe (21).
Pia wamo Sarah Hangaya (20), Neema Stanford (21), Upole Athumani (19), Asia Amiri (22), Lucy Paulo (21), Johanita Kanyika (22), Mariamu Lameck (19), Blandina Paul (18),
Catherine George (19), Lilian Brayson (24) na Lucia Joseph (20).
Imeandikwa na Na Mwandishi Wetu; Tarehe: 8th April 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 183; Jumla ya maoni: 0
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limezionya klabu za Simba na Yanga kujiepusha na mambo yoyote yanayoweza kutia aibu mchezo wa mpira wa miguu.
Miamba hiyo ya soka inakabana koo katika kuwania ubingwa wa Tanzania Bara zote zikiwa na pointi 46, lakini zinatofautiana uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Kila timu imebakisha mechi moja, ambapo Yanga itamaliza ligi Jumamosi kwa kucheza na Toto African Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na Simba itamaliza pia Jumamosi kwa kucheza na Majimaji ya Songea Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga katika uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa ambao ndio kanuni zinazotumika kwenye ligi hiyo ikitokea timu kulingana pointi, ina faida ya mabao 22, wakati Simba ina faida ya mabao 21.
Akizungumza Ijumaa, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema ana amini timu zote zitazingatia taratibu za mpira na hakuna ambayo itafanya mambo kinyume na taratibu.
Alionya vitendo vyovyote vitakavyofanywa kwa nia ya kuaibisha mpira wa miguu hatua kali zitachukuliwa kwa wahusika.
Pia Wambura alitolea ufafanuzi wa kanuni za ligi kwamba kinachoangaliwa kama timu zikifungana pointi ni uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa na kama hilo pia zikiwa sawa basi timu yenye idadi kubwa ya mabao ya kufunga ndiyo inakuwa ipo juu.
Yanga imefunga mabao 29 na imefungwa saba, wakati Simba yenyewe imefunga mabao 36 na imefungwa 15, hivyo kama ikitokea Simba ikaifunga Majimaji na Yanga pia ikaifunga Toto African, lakini zikalingana uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa, basi bingwa ataamuliwa kwa mwenye idadi kubwa ya mabao ya kufunga.
MIAMBA ya soka ya Hispania, Barcelona juzi ilifanya kweli katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kuichapa Shakhtar mabao 5-1, huku ikiwachukua dakika
mbili kuhesabu bao la kwanza.
Ushindi huo umewaweka Barcelona katika nafasi nzuri ya kuweza kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.
Barca iliwachukua dakika mbili kuweza kuhesabu bao la kwanza dhidi ya wapinzani wao kutoka Ukraine.
Andres Iniesta alimpasia mpirea Lionel Messi, ambaye aliunasa mpira na kumchungulia kipa Andriy Pyatov na kufunga shuti la chini ambalo lilijaa wavuni.
Kisha Iniesta naye alitengeneza nafasi ya kufunga kwa kumpasia beki Daniel Alves, aliyekuwa peke yake na kufunga bao la pili dakika ya 34.
Barca ilipata bao la tatu dakika ya 53 wakati mlinzi Gerard Pique, alipounganisha mpira wa kona na kufunga goli la tatu likiwa pia goli lake la pili msimu huu.
Yaroslav Rakitskiy aliipa matumaini timu ya Ukraine kwa kupata bao la ugenini alipomfunga kipa wa Barcelona, Victor Valdes katika dakika ya 60.
Lakini Seydou Keita, akaifungia Barcelona bao jingine dakika moja baadaye.
Kiungo Xavi alikuja kufunga bao jingine zikiwa zimesalia dakika nne kabla ya mpira kuisha.
Ushindi huyo wa Barcelona umeifanya, Shakhtar iwe na mlima wa kupanda katika mechi ya marudiano ambapo italazimika kushinda mabao 4-0 ili kusonga mbele.
Ushindi huo umeweka dalili za kukutana Barcelona na Real Madria katika hatua ya nusu fainali baada ya Real, nayo kushinda mechi yake ya kwanza dhidi Tottenham mabao 4-0 Jumanne.
Lakini kocha wa Barca, Pep Guardiola amewaonya wachezaji wake kutoidharau timu ya Shakhtar, ambayo iliwahi kushinda mabao 3-2 katika Uwanja wao wa Nou Camp mwaka 2008.
Alisema: "Matokeo si ya mwisho. Wana timu nzuri sana."
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.