Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,501
- 911,251
- Thread starter
- #15,321
Schalke, Real Madrid zakandamiza Ulaya Send to a friend Wednesday, 06 April 2011 21:24
LONDON, England
SCHALKE 04 ya Ujerumani na Real Madrid ya Hispania zimefanya kile kisichotarajiwa baada ya kufunga idadi kubwa ya mabao katika mechi za robo fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya na kujihakikishia kucheza nusu fainali.
Schalke iliwatandika mabingwa watetezi, Inter Milan mabao 5-2 wakati Madrid iliilowesha Tottenham 4-0. Mechi za marudiano zimepangwa kupigwa Aprili 13.Timu hiyo inaoshiriki Ligi ya Bundesliga, ambayo haijaonyesha makali kwenye ligi hiyo, ilipata bao la kuongoza kupitia kwa Raul Gonzalez na kufanya idadi ya mabao yake kwa mashindano yote kufikia 70.
Madrid nayo kwa upande wake, ilitawala hasa baada ya kutolewa kwa mshambuliaji wa Tottenham, Peter Crouch katika dakika ya 15. Emmanuel Adebayor alifunga mawili wakati Angel Di Maria na Cristiano Ronaldo waliongeza kwa kila moja.
Kwa timu yenye wachezaji 10 kwa muda mrefu, huwezi kuweka mikakati na malengo vikatimia, alisema kocha wa Madrid, Jose Mourinho. Lakini kwa England, huo si mwisho.
Mechi nyingine zilikuwa jana usiku, Manchester United ilikuwa stanford Bridge kucheza na Chelsea na Shakhtar Donetsk dhidi ya Barcelona.Inter, ilikuwa inaonekana kutaka kuweka rekodi ya kutetea ubingwa mara mbili, ilianza kupata bao sekunde ya 29 kupitia kwa Dejan Stankovic, aliyeukwamisha mpira wavuni umbali wa mita 50 baada ya kipa wa Schalke, Manuel Neuer kutoka kwenye eneo lake.
Mabingwa hao watetezi walipata bao la pili kupitia kwa mshambuliaji wa Argentina, Diego Milito katika dakika ya 34, lakini Schalke walizinduka baadaye. Inter, waliokuwa bila beki wao Lucio, iliwamaliza kadi nyekundu ya Cristian Chivu aliyetolewa nje dakika ya 62 wakati huo matokeo yakisomeka 4-2.
Tulianza vizuri, lakini mambo yalibadilika kipindi cha pili, alisema nahodha wa Inter, Javier Zanetti. Joel Matip aliisawazishia Schalke dakika ya 17 kabla ya Edu kufunga lingine dakika ya 40.
Mchezaji wa zamani wa Real Madrid na Hispania, Raul alifunga bao la kuongoza katika dakika ya 53, kabla ya Andrea Ranocchia kujifunga na Edu kuongeza lingine na kujiwekea matumaini ya kucheza na Chelsea au United.
Ilikuwa siku njema kwetu, kufunga mabao matano si mchezo, tena dhidi ya mabingwa watetezi, Raul alisema. Baada ya kuanza vibaya, timu yangu ilionyesha ukomavu.
Mourinho anajipa matumaini ya kutwaa ubingwa mara tatu na klabu tatu tofauti, aliiongoza Madrid kufunga mabao matatu ya harakaharaka kipindi cha pili dhidi ya Spurs.
Ni moja ya siku ambazo mambo yamekwenda kombo...mambo yaliharibika kabisa, alisema kocha wa Tottenham, Harry Redknapp, ambaye alimpoteza Aaron Lennon dakika za mwisho mwisho.
Ilikuwa ngumu kuja hapa na watu 11, na mbaya zaidi tukacheza 10.Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Adebayor alifunga bao lake la 10 katika mechi dhidi ya Spurs katika dakika ya nne na dakika ya 57, huku mabao yote akiyafunga kwa kichwa.
Kwa wakati huo, Crouch alikuwa amekwishapigwa kadi nyekundu kutokana na kucheza ovyo. Hata hivyo, Spurs ambao wanacheza kwa mara ya kwanza, walishambulia na kuonyesha uhai.
Di Maria alifunga kwa shuti la mbali katika dakika ya 72 na Ronaldo alifunga bao lake la 38 kwa kumtungua kipa wa Spurs, Heurelho Gomes ambaye alibabatizwa na shuti hulo na kujifunga.
Kitu ambacho hakikuwa cha kawaida kwa Madrid ilikuwa kadi ya Pepe kwa kumchezea vibaya Gareth Bale dakika ya 36 na kumfanya Bale ashindwe kuendelea na mchezo huo na pengine hata wa marudiano utakaofanyika White Hart Lane.
Real Madrid inaweza kukutana na Barcelona katika nusu fainali kwani timu hiyo ya Catalan inapewa nafasi kubwa ya kuifunga Shakhtar.

PRINT