Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,501
- 911,251
- Thread starter
- #15,381
Wachezaji 26 waitwa kuunda Twiga Stars
Imeandikwa na Na Mwandishi Wetu; Tarehe: 8th April 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 31; Jumla ya maoni: 0
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars), Charles Boniface ametangaza majina ya wachezaji 26 watakaoanza mazoezi Jumatatu kwa ajili ya mechi yao ya mchujo ya michezo ya Afrika dhidi ya Sudan.
Kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Ijumaa na Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura timu hiyo itaanza mazoezi Jumatatu kwenye
Uwanja wa Karume Dar es Salaam kwa wachezaji kutokea makwao na itaingia rasmi kambini Aprili 20.
Aliwataja wachezaji walioitwa na timu zao katika mabano kuwa ni Asha Rashid (Mburahati Queens), Neema Jacob (Simba Queens), Sophia Mwasikili (Sayari), Fadhila Hamad (Uzuri), Irene Matowo (Mburahati Queens), Hellen Tolla (JKT), Mwanahamisi Shurua (Mburahati Queens) na Fatuma Jawadu (Sayari).
Wengine ni Fatuma Swalehe (Simba Queens), Maimuna Mkane (JKT), Pulkelia Charaji (Sayari), Fatuma Makusanya (Simba Queens) na Mwanaidi Tamba (Mburahati Queens).
Pia wapo Fridiana Daudi (JKT), Fatuma Salum (Mburahati Queens), Mwajuma Abdillah (Tanzanite), Mariam Fakil (Tanzanite), Mwasiti Selemani (Tanzanite), Aziza Lugendo
(Mburahati Queens), Suzana Komba (TMK), Rukia Hamisi (Evergreen), Pendo Juma (Evergreen), Zena Khamis (Mburahati Queens), Tatu Said (Umonga Sekondari, Dodoma),
Mwanaidi Khamis (Uzuri Queens) na Zena Said (Uzuri Queens).
"Kwa siku kumi za kwanza, Twiga Stars itafanya mazoezi Uwanja wa Karume kwa wachezaji kutokea nyumbani (off camp) na baada ya hapo itaingia rasmi kambini Aprili 20, 2011.
"Twiga Stars itacheza mechi yake ya kwanza ugenini Aprili 30, 2011, wakati ya marudiano itachezwa Mei 15, 2011 jijini Dar es Salaam. Twiga Stars ikiitoa Sudan itakuwa imefuzu kwa michezo ya All Africa Games ambayo itafanyika Septemba 2011 jijini Maputo,
Msumbiji," alisema Wambura.
Wakati huo huo, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imefanya marekebisho mbalimbali ya kanuni za uchaguzi ikiwemo kuainisha viwango vya ada za fomu za kuomba uongozi na za rufaa
kwa ngazi zote.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Deogratius Lyato alisema kwa wanaotaka urais wa TFF watalipa Sh 500,000, wakati Makamu wa Kwanza wa Rais na Makamu wa Pili wa Rais wa TFF ada itakuwa Sh300,000 huku wajumbe wa Kamati ya Utendaji ada ikiwa ni Sh 200,000.

PRINT