Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Bilbao draws 2-2 at Getafe in Spanish league


storypage_APlogo_01.png




PRINT RSS



Updated Mar 14, 2011 6:14 PM ET
MADRID (AP)

Substitute Urko Vera's 93rd-minute header gave Athletic Bilbao a 2-2 draw at Getafe on Monday in the Spanish league.

Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats Scores | Fixtures | Table | Stats

The Bilbao midfielder headed in a corner in the final seconds to earn a point at Alfonso Perez coliseum after Manuel del Moral had scored a brace and an own goal.
Del Moral put the Madrid club ahead in the 53rd, but he headed a Bilbao free kick into his own net in the 69th to level the score.
The Getafe captain then perfectly placed a left-footed shot from outside the area into the right corner for what looked like the winner in the 84th.
Bilbao is one point behind fifth-place Espanyol, while Getafe has not won a game in six weeks.
 
Machaku, Yondani chali, Dihile, Kazimoto waula Send to a friend Tuesday, 15 March 2011 21:13

kocha%20poulsen21.jpg
kocha wa timu ya taifa,Taifa Stars, Jan Poulsen

Sosthenes NyoniKOCHA wa timu ya taifa,Taifa Stars, Jan Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kitakachojiandaa kwa mchezo dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na kuwaacha Salum Machaku na Kelvin Yondani.

Mbali ya kuwaacha nyota hao Poulsen amewaita kwa mara ya kwanza nyota wa JKT Ruvu kiungo Mwinyi Kazimoto na kipa Shaaban Dihile waliokuwa nje ya kikosi hicho kwa zaidi ya miezi 8 tangu kuoondoka Mbrazil Marcio Maximo.

Akitangaza kikosi hicho kwenye ofisi za Shirikisho la Soka nchini TFF, Poulsen alitetea uamuzi wake wa kumuita mshambuliaji mkongwe Athuman Machupa kwa kusema uzoefu wake una umuhimu katika kujenga ari ya kikosi kwa kuwa anajua nini anachokifanya.

"Tunahitaji kuchanganya wachezaji ili kuwapa uzoefu wale chipukizi ili waweze kujifunza kwa wale wachezaji wazoefu,"alisema Poulsen.

Mdenmark huyo amemwacha beki wa Simba, Kelvin Yondan, kipa wa Majimaji, Said Mohamed na mshambuaji wa Mtibwa Sugar, Salum Machaku aliyekuwa moja ya nguzo muhimu kwenye kikosi cha Kilimanjaro Stars kilichotwaa ubingwa wa Kombe la Chalenji mwishoni mwaka jana.

Pia, amewachagua Shaban Kado na Mbwana Samata katika kikosi chake ili hali anajua wazi wachezaji hao wamo katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 23, Ngorongoro Heroes kinachojiandaa na mechi dhidi ya Cameroon.Poulsen alisema kuwa timu zote hizo ni muhimu, lakini duniani kote timu ya taifa ya wakubwa ni muhimu zaidi.

Kwa mara ya kwanza Mdenmark huyo amewaita Kazimato na Dihile ambao waliwahi kuichezea Taifa Stars ilipokuwa ikinolewa na Marcio Maximo.Akizungumzia uamuzi wa Poulsen, kocha wa JKT Ruvu, Charles Kilinda alisema amefurahishwa na uteuzi wa wachezaji wake wawili Dihile na Kazimoto na kumtaka kuongeza idadi ya wachezaji kutoka kikosi cha maafande hao.

"Nimefurahi, kwanza nasema alikuwa hatutendei haki, alichelewa sana kuwaita, lakini Poulsen aangalie uwezekano wa kuongeza wengine kwani nina wachezaji wengi mahiri,"alisema Kilinda.

Naye Dihile aliyeiongoza Stars kucheza hatua ya mtoano ya michuano ya CHAN mwaka 2009 alisema; "Nimefurahi kwa sababu mwalimu ameona nafaa na mimi naahidi sitamuangusha nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kwa kushirikiana na wenzangu kuhakikisha tunaisaidia timu ifikie malengo yake.’’

‘’Kwa sababu Mungu ndiye muweza wa yote na kila kitu ni juu yake hata hilo suala zima la ushindani wa makipa katika timu ya taifa yeye mwenyewe ndiye atafanikisha,’’alieleza Dhile.Akizungumzia mchezo wa Machi 26, Poulsen alisema ni dhahiri utakuwa mgumu ukizingatia uzuri wa wapinzani wao Jamhuri ya Afrika ya Kati ambao wanaongoza kundi hilo na walipata ushindi ugenini dhidi ya Algeria.

"Tunahitaji pointi nne ili tujiweke katika nafasi nzuri ya kufuzu,tunafahamu wazi kwamba Jamhuri ya Afrika ya Kati si timu rahisi, waliifunga Algeria kwao, lakini na sisi tunataka ushindi pia, hivyo tutahakikisha tunashinda mechi hiyo,"alisema Poulsen.

Kikosi kamili kilichotangazwa jana mbele wa Wanahabari ni makipa Shaaban Kado, Juma Kaseja na Shaaban Dihile wakati mabeki ni Shadrack Nsajingwa, Aggrey Morris, Nadir Haroub'Canavaro', Stephano Mwasika,Haruna Shamte, Juma Nyoso na Idrisa Rashid.

Viungo ni Nurdin Bakari, Shaaban Nditi, Jabir Aziz, Henry Joseph, Abdi Kassim na Mwinyi Kazimoto huku washambuliaji ni Dan Mrwanda, Nizar Khalfan, Mrisho Ngassa, Mohamed Banka, Athumam Machupa, John Boko na Mbwana Samata.

Wakati huo huo; Salome Millinga anaripoti kuwa timu ya soka ya vijana U-23, Ngorongoro Heros leo itashuka dimbani uwanja wa Uhuru kucheza mechi yake ya kirafiki dhidi ya Azam FC kabla ya kuifuata Mtibwa Sugar, Machi 18 mjini Morogoro.

Akizungumza na Mwananchi, kocha Ngorongoro Heroes, Jamhuri Kihwelu alisema anategemea mechi hizo mbili zitamsaidia kujua mapungufu ya kikosi chake kabla ya safari ya Cameroon."Pia, tunasubiri majibu kutoka Shirikisho la soka Uganda kama timu yao itakuja huku kwa ajili ya mechi ya kirafiki au tutaenda kwao kucheza na timu ya U23 ya kwao," alisema Kihwelu.
 
Azam itatoa jibu' Send to a friend Tuesday, 15 March 2011 21:04

Sweetbert Lukonge

KOCHA wa Yanga, Sam Timbe amesema mechi yake dhidi ya Azam itakayofanyika Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Uhuru ndiyo itakayotoa majibu sahihi ya wapi atakapomalizia msimu huu.

Akizungumza na Mwananchi, Timbe alisema timu yake bado ina nafasi ya kunyakuwa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu kutokana tofauti ndogo ya pointi iliyopo baina ya wapinzani wao wa jadi Simba.

"Nafasi ya kufanya vizuri na kunyakuwa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu bado tunayo kwa sababu Simba wanaongoza kwa pointi nne tu.

"Endapo tutafanya vizuri katika mechi zetu zilizobakia ukiwemo mchezo wa Jumapili dhidi ya Azam na kuomba wapinzani wetu wapoteze mechi zao basi tunaweza kunyakuwa ubingwa huo," alisema Timbe.

Alisema ligi ya Tanzania kwa sasa ni ngumu na kila timu inaweza kufanya maajabu hivyo ni mapema sana kwa watu kuanza kusema kuwa timu fulani ni bingwa wakati mikikimiki hiyo haijafikia ukingoni.

Alisema vijana wake kwa sasa wako vizuri na wanaendelea kujifua ili kuhakikisha wanaibuka na pointi tatu dhidi ya Azam na kupunguza tofauti ya pointi iliyopo kati yao na Simba.

Simba inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 44 na Yanga inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 40 wakati Azam ipo nafasi ya tatu ikiwa na poiti 37 katika michezo 19.
 
Yanga, JKT zaingiza 19 m Send to a friend Tuesday, 15 March 2011 21:02

Sosthenes Nyoni
KIASI cha Sh,milioni 19,475,000 kimepatikana kupitia viingilio vya pambano la Ligi Kuu kati ya Yanga na JKT Ruvu lililofanyika Machi 12 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Afisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema mapato hayo yalipatikana baada ya watazamaji 4,028 kuingia uwanjani kwa viingilio vya kati ya Sh15,000, sh. 8,000, sh. 5,000 na sh. 3,000.

Wambura alisema kuwa baada ya kulipa asilimia 18 kwa Serikali ambayo ni sh. 2,970,763 ikiwa ni Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na gharama za awali za mchezo sh. 3,639,600 fedha zilizobaki kwa ajili ya mgawanyo ni sh. 12,864,637.

Alisema Katika mgawanyo huo kila timu ilipata mgawo wa sh. 3,859,391, gharama ya mchezo Sh. 1,286,464,TFF Sh. 1,286,464, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu- FDF Sh. 643,232), Uwanja Sh. 1,286,464, Baraza la Michezo la Taifa BMT Sh. 128,646 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam DRFA Sh. 514,585.

Aidha Wambura alisema mechi kati ya Azam na Mtibwa Sugar iliyochezwa Machi 13 mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru iliingiza kiasi cha Sh Milioni 3,718,000 baada ya kuingiza watazamaji 1,021 waliolipa viingilio vya kati ya Sh,5,000, 3,000 na 2,000.

Wambura alisema baada ya kuondoa gharama za awali za mechi kila timu ilipata Sh, 468,494, gharama ya mchezo Sh,156,165,TFF Sh, 156,165, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu- FDF Sh, 78,082, Uwanja Sh. 156,165,DRFA Sh. 62,466 na BMT sh. 15,616.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom