Matokeo mazuri yazibeba kadhaa Ligi ya Mabingwa Ulaya Send to a friend Monday, 14 March 2011 20:14
MUNICH, Ujerumani
HUKU zikikabiliwa na mechi za marudiano za Ligi ya Mabingwa Ulaya leo, timu za Bayern Munich, Olympique Marseille na Manchester United zilifanya vizuri katika mechi zao za mwisho wa wiki.
Timu hizo zinakabiliwa na mechi hizo muhimu za marudiano za Ligi ya Mabingwa Ulaya, ingawa itakuwa ni Bayern Munich ambayo inaikabili Inter iliyokuwa na matokeo mazuri zaidi katika Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga baada ya ushindi wa mabao 6-0.
Hata hivyo, Man United na Olympique Marseille ambazo zinakutana kwenye Uwanja wa Old Trafford, Manchester baada ya suluhu ya 0-0 , pia zilishinda kiaina.
ENGLAND
Ushindi wa Man United wa mabao 2-0 dhidi ya Arsenal Jumamosi kwenye Kombe la FA utaikutanisha na wapinzani wao wa jiji la Manchester, Man C ity kwenye mchezo wa nusu fainali .
Man United waliwalaza wapinzani wao wakubwa wa msimu katika mbio za kusaka ubingwa wa Ligi Kuu, Arsenal na kuwatupa nje ya michuano hiyo, wakipangiwa sasa kukutana na Man City kwenye mchezo wa nusu fainali mwezi ujao katika Uwanja wa Wembley.Hilo lilikuwa pigo la pili kwa Arsenal baada ya kutolewa na Barcelona katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kipigo cha mabao 3-1
"Ulikuwa mchezo wenye shinikizo kubwa kwa timu zote mbili," alieleza kocha Sir Alex Ferguson.
Kwa upande wao, Man City, baada ya kuiondoa Reading kwa bao 1-0 wamejikatia tiketi ya kucheza na Man United katika nusu fainali ambayo itafanyika kati ya Aprili 16 na 17.
Nusu fainali nyingine itakuwa baina ya Stoke City na Bolton Wanderers ambazo ziliziondoa West Ham na Birmingham City katika mechi nyingine za mwisho wa wiki.
UFARANSA
Lille MÈtropole imeendelea kukaa kileleni mwa Ligue 1 baada ya ushundi mgumu wa dakika za mwisho za mchezo kwa bao la Eden Hazard katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Valenciennes Jumapili. "Tulikuwa wenye bahati baada ya kipindi cha kwanza kucheza wastani," alisema kocha Rudi Garcia.
"Tulitarajia kwamba kitu maalum kingetokea kipindi cha pili na ndivyo ilivyokuwa kwa bao la Eden." Stade Rennais wanashika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi tatu baada ya kufungwa 2-0 na Marseille, ambao wao wapo nyuma kwa pointi wakishika nafasi ya nne. Nafasi ya tatu inashikwa na Olympique Lyon, walioko mbele ya Olympic Marseille kwa tofauti ya mabao baada ya ushindi wao wa mabao 2-0 dhidi ya Sochaux.
UJERUMANI
Uongozi wa Borussia Dortmund kileleni mwa Bundesliga umepunguzwa na kuwa pointi tisa baada ya kufungwa 1-0 na TSG 1899 Hoffenheim, kipigo chao cha tatu msimu huu.
"Sina wasiwasi hata kidogo," alisema J¸rgen Klopp. Mpinzani wa karibu wa Dortmund, Bayer 04 Leverkusen, walishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Mainz 05 wanaoshika nafasi ya tano.
Hannover 96, waliofungwa kwa mabao 4-0 na FC Koln wapo nyuma kwa pointi tano, huku vinara wa ligi, Bayern wakiwa nyuma kwa pointi mbili zaidi baada ya ushindi mnono wa mabao 6-0 kwa Hamburg SV, ambao walimtimua kocha wao, Armin Veh.
ITALIA
Huku AC Milan wakiongoza kwa tofauti ya pointi tano, kileleni mwa Serie A, walizuiwa na kutoka sare ya 1-1 dhidi ya klabu ya mkiani, AS Bari. Udinese walipata karamu ya mabao 7-0 dhidi ya Palermo, ambayo karibuni ilifungwa pia mabao manne na Cagliari. Kinara wa mabao wa msimu uliopita, Antonio Di Natale alifunga mawili na kufikisha idadi yake kuwa 24 , pungufu ya mabao manne kufikia idadi yake msimu uliopita.
Pia, ilikuwa siku nzuri kwa Francesco Totti, ambaye alishangilia ushindi wa klabu yake, AS Roma kwa mabao 2-0 kwa Lazio kwamba ulikuwa wa kihistoria. "Ushindi huu kwa mabao mawili, yote yangu, dhidi ya wapinzani wetu wa mjini ni jambo la kujivunia."
HISPANIA
Karim Benzema alikuwa chachu ya ushindi wa mabao 2-0 wa Real Madrid Jumamosi dhidi ya HÈrcules , hasa baada ya kubaini kuwa wapinzani wao, Barcelona walishikwa shati na kutoka sare ya bao 1-1 na Valencia, Jumapilid.
Ndoto za Barca kuendeleza ushindi zilianzishwa na bao la Bojan Krkic dakika ya 30, lakini Jes˙s Navas alisawazisha kwa Valencia, dakika ya 49. " Ushindi hapa ulikuwa wa muhiomu kwetu na pointi mbili zingesaidia, lakini zimeyeyuka," alisema kiungo Sergio Busquets. "Lakini, kitu kizuri ni kwamba bado tunaongoza kwa pointi tano mbele ya Real Madrid na hii ni dalili njema."
KWINGINEKO ULAYA
Huko Austria, SK Rapid iliishangaza Austria Wien na kuzima ndoto zao za ubingwa kwa ushindi wa bao1-0, ambao umewaacha wapinzani wao nyuma ya SK Sturm Graz kwa tofauti ya mabao. Hakukuwa na mabao katika ligi ya Bucharest baina ya majirani, Rapid Bucuresti na Dinamo Bucuresti, ambao wote wanashika nafasi za tano na sita.
Ligi ya Daraja la Kwanza Czech , Viktoria Plzen iliilaza AC Sparta Praha 1-0 na kukaa kileleni kwa tofauti ya pointi tano. Kule Uholanzi, uongozi wa ligi wa PSV Eindhoven umebakia kwa pointi moja baada ya sare ya 2-2 dhidi ya NEC Nijmegen na wapinzani wao wa karibu Twente kushinda.