Michezo Maarufu Vikoba inalostisha

Shindu Namwaka

JF-Expert Member
Sep 22, 2014
4,911
3,082
Leo nimeona nilete uzi huu.

Sikuhizi kumekuwa na michezo fulani ya kuweka pesa na kukopa kisha kulipa kwa riba mchezo maarufu kwa jina #vikoba#.

Lakini mchezo huu umekua sababu kubwa ya watu kurudi nyuma kimaendeleo pale inapotokea umekopa pesa na umeshindwa kulipa kwa wakati mpaka kufikia muda wa kuvunja kikoba hicho.

Kumekua na sheria ambazo kama ulikopa na ukashindwa kurejesha mpaka mwisho wa kuvunja kikoba hicho na kugawana pesa mulizokua munaweka basi watu kutathimini mali ambazo wanaweza wakauza na kuzirejesha pesa hizo kwenye kikoba sasa nilichokiona leo kimegusa binafsi yangu nimesoneka sana moyoni mwangu ni pale lilipouzwa banda la chumba kimoja na ukumbi kwa sh.3,60000/=.

Ok sawa lakini mbaya zaidi ile nyumba iliyouzwa kuna bibi ambae anaishi mzazi wa huyo kijana mwenye hilo banda banda limeuzwa na bibi inatakiwa aame yule jamaa aliomba wampe siku moja afanye mipango ya kukopa tena sehemu fulani ili siku ya pili ailipe watu wamepaniki na kusema haiwezekani basi wameshauza tayali kinachofata ni bibi kuhamishwa du ni shida.

Tuwe makini na hii kitu
 
Mkuu sasa hapo shida ni vikoba au ni huyo jamaa yako kushindwa kurejesha mkopo??
Hata ingekuwa amekopa benki bado wangeliuza Hilo banda ambalo ni collateral ya huo mkopo!!
 
Je ukikopa bank na ukishindwa kulipa wanakufanya nini? Kopa kwa mipango. Usiende kunywea bia pesa ya mkopo.
 
Imefkia kipindi watu hawawezi kuishi bila mikopo...
tena wengine ndo kama huyo kijana, Anakopa huku ndo akalipe kule...,
 
Mtoa mada hujafanya utafiti wa kutosha

Vicoba vinasaidia sana kina mama na walimu sana hapa town vipo vicoba vingi imara kupitia hiyo michango,mikopo,riba na jamii akinamama wamejijengea vinyumba vyao inshaalah ila peke yao wasingeweza!
 
Leo nimeona nilete uzi huu.

Sikuhizi kumekuwa na michezo fulani ya kuweka pesa na kukopa kisha kulipa kwa riba mchezo maarufu kwa jina #vikoba#.

Lakini mchezo huu umekua sababu kubwa ya watu kurudi nyuma kimaendeleo pale inapotokea umekopa pesa na umeshindwa kulipa kwa wakati mpaka kufikia muda wa kuvunja kikoba hicho.

Kumekua na sheria ambazo kama ulikopa na ukashindwa kurejesha mpaka mwisho wa kuvunja kikoba hicho na kugawana pesa mulizokua munaweka basi watu kutathimini mali ambazo wanaweza wakauza na kuzirejesha pesa hizo kwenye kikoba sasa nilichokiona leo kimegusa binafsi yangu nimesoneka sana moyoni mwangu ni pale lilipouzwa banda la chumba kimoja na ukumbi kwa sh.3,60000/=.

Ok sawa lakini mbaya zaidi ile nyumba iliyouzwa kuna bibi ambae anaishi mzazi wa huyo kijana mwenye hilo banda banda limeuzwa na bibi inatakiwa aame yule jamaa aliomba wampe siku moja afanye mipango ya kukopa tena sehemu fulani ili siku ya pili ailipe watu wamepaniki na kusema haiwezekani basi wameshauza tayali kinachofata ni bibi kuhamishwa du ni shida.

Tuwe makini na hii kitu
mimi sioni tatizo ikiwa wamefanikiwa kurejesha pesa aliyoshindwa kuirejesha, sasa mtu kama ameshindwa kurejesha deni kwa muda wote aliopewa ndio angeweza vipi ndani ya siku chache?
unajua ukiona watu wameamua kuja kuuza vitu kufidia madeni lazima huyo jamaa kazingua na avumiliki
 
Kwa Tanzania yetu Vicoba ndio mkombozi,msaada na uti wa mgongo wa mlala hoi,
Hizi taasisi nyingine za fedha na mabenki ni jini kwa wananchi.
Labda ikija hiyo bank ya waalimu inawezakua na unafuu.
 
Kuunda vikundi ni kudhirilisha uoga sawa vikundi vimewasaidia wengi na vimewafirisi wengi lakini mimi kwenye maisha yangu nitofauti sana na sijawahi kufikiria kujiunga na kikundi chochote.

Sijui kucheza michango mara vyama vya kufa na kuzikana never miaka 150.
 
Back
Top Bottom