Mlume Ndago
Member
- Jul 28, 2025
- 41
- 53
Habari za muda huu wakuu, ni matumaini yangu kuwa mpo na afya na nguvu tele, na kama ni hivyo basi tumshukuru na kumtukuza Mungu wa mbinguni aliye hai.
Moja kwa moja bila ya kupoteza muda niende kwenye mada yangu iliyonifanya niandike uzi huu.
Suala hili huenda wengine wanalijua na wengine hawalijui, ila kwa ufupi tu ni kwamba.
Wanachama wote ambao wamejiunga na mfuko wa mafao ya jamii yaani NSSF michango yao ya mwaka 2022 na 2024 ya Mwezi wa 12 haionekani kwenye statement ingawa mwajiri alishapeleka tayari.
Binafsi sijajua tatizo ni nini! Ila nahisi (sina uhakika) itakuwa wamejikopesha kufanyia miradi yao au zimechukuliwa kwenda kufanyia kazi maalum, maana suala hili tangu litokee ni mwezi sasa na hakuna ufafanuzi wowote uliotolewa kwa wanachama.
Najiuliza je, ikitokea mfanyakazi ameachishwa kazi leo inakuwaje kuhusu michango yake ya mwezi wa 12 mwaka 2022 na 2024?