AL SHARPTON
JF-Expert Member
- Feb 6, 2014
- 2,797
- 953
Marehemu mwenyewe alitakaje?
Mke anaweza kuwa anataka kuwapa ndugu majivu ya mtu ambaye hakutaka hilo.
Na huko nyumbani unaweza kuambiwa hawakubali kwa sababu habari nzima ya kumchoma mtu moto kimila ni laana.
Ndiyo maana nauliza kuna will?
Mia mia mkuu.
Kiranga wakati mwingine unakera sana....
Unapenda kuandika unachojua kuliko ulichoulizwa au kujibu hoja husika....
Ni tabia ya watanzania wengi tofauti na waafrika wengine kudharau kwao...asili yao...utu wao na ndigu zao....
Inatia aibu na fedheha mtu kujifanya mzungu zaidi ya wazungu wenyewe...
Mimi si mgeni wa maisha ya watanzania wengi waliopo US hupenda kujiona wako juu kiasi cha kudharau hata ndugu zao lakini wanapofikwa na mauti ndipo pilika pilika huanza za kuchangishana kusafirisha mwili...
Ingekua ni will yake kuwa hataki ndugu angelimwambia hilo mkewe but kitendo cha mkewe kuhangaika kutafuta ndugu kinaashiria huenda marehemu alikwepa ndugu kwa kuwa alijisikia sana na hakutaka majukumu yoyote juu ya ndugu zake nyumbani...
Pilika za kusaka ndugu alizianza tangu anaumwa kama unataka uthibitisho nenda pale embassy kaulize jamaa alivyohangaika na matangazo kwakuwa hakuwa na mawasiliano na jamaa yeyote wa karibu...
Maisha ni safari ndefu kuna kuugua...kuzeeka....kulemaa.....kudhoofu na kufa tusijisahau namna hiyo....
Huyo jamaa anapenda mizaha sana
Wewe unaleta ligi tu......
Ndugu za marehemu wanatafutwa kama unawajua mtafute mkewe au peleka taarifa ubalozini....
Hii iwe fundisho kwa wengine......
Wanatutia aibu.....
Fundisho kwa wengine kuhusu nini?
Mtu kajiishia maisha yake yote humjui hakujui, amekutia aibu kivipi?
Kiranga habari ya mjini ni ndugu wa marehemu wanatafutwa kama unawajua saidia si muda wa mzaha huu....
Aibu ni hii ya mkewe kuangaika kutafuta ndugu wakati wamezaa watoto wanne kwa mda wote huo bila kuwajua ndugu zake...
Haiwezekani mtu ugombane na kila ndugu hiyo ni tabia tu ya kujiona bora...
Naongea haya kwakuwa nipo hapa foreign affairs mda kidogo na tunakumbana na matatizo mengi sana ya diasporas hususan kama haya....
Habari za will kamuulize mkewe kama zitakusaidia....
Stop being imbecilic all the time kiranga!!!!!
Ndugu za marehemu hata wewe unaweza kuanzia kwenye mitandao ya jamii kuwatafuta, kuna Lukindos kibao.
Kukuonesha jinsi gani hili jina lilivyokuwa na network kubwa hapo Wizara ya Mambo ya Nje kwenyewe tu palikuwa na Balozi amefariki miaka michache iliyopita, akitwa Balozi Raphael Lukindo.
Unajuaje kwamba aibu ni ya mkewe kutafuta ndugu leo? Kwa nini ni aibu?
Unajuaje kwamba mkewe hakutaka kuwajua ndugu zake tangu kabla na akakatazwa na mume? Na unajuaje kwamba hakuna sababu valid zisizoipa familia hii aibu kutafuta ndugu leo?
Na unajua mkewe anawatafutia nini ndugu? Unajua sababu za ndani kabisa za familia hii kuishi ilivyoishi na kufanya ilivyofanya kiasi cha kusema hii ni aibu?
Au kama kawaida ya baadhi yetu tunarukia ku label mambo "aibu" bila hata ya kuwa na taarifa za mambo yalivyokuwa?
Ukimpata ndugu usisite kutoa taarifa....
Tunatanguliza shukrani...
Nitatoaje taarifa wakati sijui kama marehemu alitaka ndugu washirikishwe baada ya yeye kufariki?
Mimi sipo katika ku assume tu kwamba kila mtu ana values kama zangu, au zako.
Especially kama mtu mwenyewe kashajionesha wazi kwamba ni outlier tangu alivyoishi.
Tatizo lako unapenda kutoa majibu mepesi kwa maswali mazito....
Wewe unayesema kirahisi rahisi kwamba hii ni aibu bila hata kujua details za maisha ya hii familia ndiye uliye deeply steeped in research before giving your answers.
Unataka kutoa majibu ya kuanza kutafuta ndugu kabla hujajua kama marehemu alitaka hilo ama la, na kwa nini marehemu kakata mawasiliano na Tanzania miaka yote hii.
Mimi natafuta habari zaidi kujua marehemu alitaka nini kabla ya kwenda na default settings.
Kati yetu wawili hapa, nani anapenda kutoa majibu mepesi kwa maswali mazito?
Ndugu wanatafutwa baada ya miaka 30?Ndugu za marehemu wanatafutwa kama unawajua mtafute mkewe au peleka taarifa ubalozini....
Hii iwe fundisho kwa wengine......
Wanatutia aibu.....
Mimi silizungumzii hili kwa ngazi binafsi ni issue iliyokuwa raised na mkewe...
Wewe unaleta hoja kwangu wakati kinachotakiwa ni ndugu wa marehemu nakushangaa unavyomaliza nguvu kughani mashairi yasiyo na tija...
Hiyo will ukiipata itakusaidia nini? Hebu kama umeshindwa kusaidia ktk hili kaa kimya tu acha wenye msaada watoe...
Ndugu wanatafutwa baada ya miaka 30?
Wanaotia aibu ni nyie mnaotafuta ndugu zake.
"Kinachotakiwa ni ndugu wa marehemu" kinachotakiwa na nani?
My whole focus ni kujua marehemu alitaka nini, hujaweza kujibu hilo unajikita tu katika "kinachotakiwa ni ndugu wa marehemu".
Will nikiipata itanisaidia nini? Are you serious?
Will ndiyo inayotoa matakwa ya marehemu, kama vile "nyumba yangu isichukuliwe na mtu mwingine ila mke wangu" au "mke wangu asirithiwe na ndugu zangu wengine wowote kwa mujibu wa mila zetu" au "401 K yangu iende kwenye charity fulani" au "majivu yangu yasivuke bahari", au "ndugu zangu nisameheni kwa kujitenga kwa miaka yote hii".
Wewe leo unauliza will itasaidia nini?
Sie akina nani?
Hata wewe ukiwa na shida ubalozini au wizarani utasaidiwa...
Its not our private business
Ndio maana tangu awali nilikwambia unapenda kuandika unachojua kuliko ulichoulizwa...
Hili ni tatizo la kuzoea kukariri kuliko kuelewa...
Nilikuuliza will ya marehemu lukindo inakusaidia nini wewe binafsi na si will in general sense....
Unaanza ngojera na mashairi yasiyo na tija that's ridiculous!!!
Mkewe ametoa taarifa ya kutafuta ndigu sasa nakushangaa wewe umekazania matakwa ya marehemu lol.....
Kama umeshindwa kutoa msaada kaa kando....
Unawezaje kuwa na will ya marehemu Lukindo inayoelea tu juu juu bila ya kuwa will in general.
Tatizo lako umejaa collectivism in a Borg-like mindset.
Will ya marehemu Lukindo itanisaidia nini mimi binafsi, kujua majibu ya maswali ambayo hatuna majibu yake kukipata kujibiwa kwenye will hata wengine tunaouliza marehemu alitaka nini tutakuwa tushajibiwa. Na tunaweza kujisikia comfortable kuanza kuwatafuta kina Lukindo tunaowajua. Sasa hivi siwezi kuanza kufanya hivyo, then kesho nije kuambiwa marehemu hakutaka hilo.
Wengine tunaheshimu matakwa ya marehemu kabla ya kuanza kuji appoint wasaidizi wa marehemu kumtafutia ndugu zake bila hata kujua kama alitaka kusaidiwa hivyo au hakutaka.