Miamba ya mitihani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miamba ya mitihani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sweke34, Jul 2, 2011.

 1. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Walipasua daraja la kwanza kidato cha sita
  [​IMG] Wazawadiwa kitita cha fedha, kompyuta
  [​IMG] Watambulishwa bungeni, Bunge larindima
  [​IMG]
  Wanafunzi 20 waliofanya vizuri katika mtihani wa Taifa wa kidato cha sita mwaka jana wakiwa Bungeni ambapo walizawadiwa jana bungeni mjini Dodoma na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.


  Katika jitihada za kutaka kufufua ari ya wanafunzi kusoma kwa bidii na kujenga utamaduni mpya wa kutambua juhudi za kuendeleza elimu ya taifa, Serikali jana iliweka historia kwa kuwapongeza na kuwazawadia wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa Taifa wa kidato cha sita mwaka jana.
  Wanafunzi hao walizawadiwa jana bungeni mjini Dodoma na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

  Pinda alisema serikali ina lengo la kuanzisha mfuko maalum kwa ajili ya kuwasomesha wanafunzi wanaofanya vizuri katika mitihani yao ya sekondari kwenye vyuo vya elimu ya juu vya nje ya nchi.

  Waziri Mkuu aliyasema hayo wakati Bunge lilipowapongeza wanafunzi hao 20 waliofanya vizuri katika mitihani yao mwaka huu.

  Alisema ameiagiza Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), kukaa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kuangalia utaratibu huo wa kupongeza kuwa wa kudumu.

  “Nimeiagiza Tamisemi kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu kuhakikisha unakuwepo utaratibu huu uwe wa kudumu na ikiwezekana hata wale wa vyuo vikuu nao wanaofanya vizuri waweze kutambuliwa kama hawa.

  “Nia yetu ni kufanya mfuko maalum ambao utawawezesha wanafunzi hawa kusoma katika vyuo vikuu vya nje ya nchi,” alisema.

  Aidha, Pinda alisema wanafunzi saba wamethibitisha kuwa uamuzi wa Serikali wa kujenga shule za kata ulikuwa ni uamuzi na utabaki kuwa uamuzi sahihi.

  Alisema kama shule hizi zisingekuwepo huenda vijana hao wasingeweza kuonyesha uwezo wao kitaaluma kama walivyofanya katika mitihani yao hiyo ya kidato cha sita hususan wasichana.

  Alisema pia kufanya vizuri kwa wanafunzi hao kumeonyesha kuwa changamoto zilizopo zikitatuliwa wanaweza kufanya vizuri zaidi.

  Alisema ni jukumu la Serikali kuendelea kuziboresha shule hizo na kuwatia moyo walimu na wanafunzi wao ili waendelee kufundisha na kujifunza kwa bidii.

  Katika hafla hiyo, Pinda alitangaza zawadi kwa wanafunzi hao 20 kuwa ni kompyuta aina ya Lap Top na Sh. 150,000 pamoja na Cheti cha Ubora kwa kila mwanafunzi aliyealikwa jana.

  Pia zimetolewa Sh. 500,000 pamoja na Cheti kwa Walimu 31 wa A-level waliowafundisha wanafunzi hao.
  Pinda alisema Serikali imetoa Sh. milioni moja pamoja na cheti kwa kila shule walikosoma wanafunzi hao na meza ya maabara yenye thamani ya Sh. milioni tano.

  Kadhalika, shule zote za kata saba ambazo wamesoma wanafunzi hao walikabidhiwa cheti.
  Awali, waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, alisema wanafunzi sita kati ya 10 kwa upande wa wasichana walifanya vizuri katika masomo ya sayansi. Alisema pia, wavulana wanane walifanya vizuri katika masomo ya sayansi.

  Aliongeza kuwa wasichana sita kati ya 10 wanatoka shule za serikali, wanne wanatoka shule binafsi.
  Kwa upande wa wavulana, wanafunzi sita nao wametoka shule za serikali na wanne shule binafsi.

  Kati ya vijana hao, vijana saba walitajwa kuwa walimaliza kidato cha sita katika shule za kata ambazo nazo zilipewa zawadi kutokana na kuonyesha mfano mzuri.

  Wanafunzi waliozawadiwa, ni Muhagachi Chacha ( Kibaha), Samwel Katwale (Mzumbe), Amir Abdallah (Feza Boys), Aron Gerson (Tabora Boys), Shaban Omary (Tabora Boys), Kudra Baruti (Feza Boys), George Assenga (Majengo), Comman Nduru (Feza Boys), Francis Joseph (Tabora Boys), George Felix (Mzumbe) na Doreen Kabuche (Benjamin W. Mkapa).

  Wengine ni Rahabu Mwang’amba (Kilakala), Mary Mosha (Kifungilo Girls), Nuru N. Kipato (Marian Girls), Zainabu Hassan (Al-Muntazir Islamic), Catherine E. Temu (Ashira Girls), Anthonia J. Lugomo (Usongwe), Cecilia Mviile (Kifungilo Girls), Mariam Matovolwa (Kilakala) na Suzan Makoi (Tarakea).

  Wanafunzi ambao walizawadiwa na Waziri Mkuu ambao walisoma katika shule za kata katika masomo yao ya kidato cha kwanza hadi cha sita ni Samweli Katwale kutoka Sekondari ya Bukwande (Magu), Francis Josephat kutoka Sekondari ya Inchugu (Tarime), Rahabu Mwang’amba kutoka Sekondari ya Vwawa (Mbeya), Zainabu Hassan kutoka Sekondari ya Uhuru (Shinyanga), Mariam Matovolwa kutoka Sekondari ya Kikuyu (Dodoma), Suzana Makoi kutoka Sekondari ya Tarakea (Rombo) na Anthonia Lugomo wa Sekondari ya Usongwe (Mbozi).

  Wakitoa maoni yao kuhusu utaratibu huo wa Bunge na serikali kuwatambua wanafunzi waliofanya vizuri, baadhi ya wabunge walisema utaratibu huo utahamasisha wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani yao.

  Mbunge wa Vunjo, (TLP), Augustine Mrema, alisema hilo ni jambo zuri kwa vile linawapa motisha wanafunzi na wenzao wanaoendelea na masomo.

  Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Suzan Kiwanga, alisema ana wasiwasi na shule zilizotajwa kuwa si za kata kwa kuwa baadhi yake zimekuwepo kabla kuanzishwa kwa shule za kata.


  Alisema wanaendelea kufanya utafiti zaidi ili kubaini kama kweli wanafunzi hao walimaliza masomo yao ya kidato cha nne katika shule za kata.

  Mbunge wa Kibakwe (CCM), George Simbachawene, alisema tukio hilo ni zuri linachochea wengine kufanya vizuri katika mitihani yao.

  Mbunge wa Shinyanga Mjini (CCM), Stephen Masele, alisema amefurahi kwa kuwa mmoja wa wanafunzi waliofanya vizuri ametoka mkoani mwake.

  Alitoa wito kwa wananchi kuziunga mkono shule hizo ili zifanye vizuri na kwamba ni matumaini yake kuwa zikifanyiwa marekebisho zitakuwa shule bora zaidi.

  Mbunge wa Lulindi (CCM), Jerome Bwanausi, alisema kuwa ni changamoto kubwa kwa wanafunzi waliobaki katika shule hizo kufanya vizuri katika masono yao ili nao wapongezwe na kuzawadiwa kama wenzao.

  Mbunge wa Rombo, (Chadema), Joseph Selasini, alisema kuwa ni jambo zuri kwa sababu wanafunzi wanaobakia shuleni wanapata moyo wa kufanya vizuri katika masomo yao.

  Hata hivyo, alisema shule nyingi hazina vitabu, walimu na maabara na kutaka changamoto hizo zipatiwe ufumbuzi wa kina bila kubweteka.

  Meneja wa Kitengo cha Habari cha Shirika lisilo la kiserikali la Haki Elimu, Nyanda Shuli, alikipongeza kitendo cha Waziri Mkuu kuwapongeza na kuwapatia zawadi vijana waliofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha sita ya mwaka huu.

  Shuli alisema kutoa zawadi kwa mtu yeyote aliyefanya vizuri ni kitendo cha kutambua juhudi zake na kumhamasisha aendelee na juhudi zake hizo.

  Aidha, alisema kitendo hicho pia kinawapa changamoto wanafunzi wengine ya kujibidisha katika masomo yao ili wafanye vizuri na hatimaye waweze kuzawadiwa kama walivyofanyiwa wenzao hao.

  Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba, alisema:
  “Kumzawadia mtu baada ya kufanya vizuri ni jambo jema, lakini kama CWT ugomvi wetu wa muda mrefu na serikali ni kuweza kuwatafutia zawadi walimu wote kwa kuwaboreshea mazingira mazuri sehemu zao za kazi, kwani zawadi kwa kikundi kidogo sio kuboresha elimu.”

  Aliongeza kuwa ili sekta ya elimu ifanye vizuri zaidi serikali inatakiwa kuwaboreshea walimu mishahara yao, vitendea kazi, maeneo ya kuishi pamoja na vivutio vingine.

  “Ikiwa serikali itaweza kuboresha vitu hivi vitatu sekta ya elimu itafanya vizuri zaidi kinyume cha hapo kutoa zawadi kwa watu wachache huku kundi kubwa likiwa limeachwa nyuma sio kuboresha elimu,” alisema.

  Mkuu wa Kitivo cha Elimu Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Dk. Honoratha Mushi, aliunga mkono maamuzi ya kuwatunukia zawadi wanafunzi waliofanya vizuri.

  Dk. Mushi alisema zawadi hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuwahamasisha wanafunzi wengine kufanya vizuri katika masomo yao.

  “Motisha hii ni nzuri na pia itasaidia kwa wanafunzi wengine kuhamasika kufanya vizuri katika mitihani yao huku wakijua wanapatiwa zawadi,” alisema na kuongeza kuwa jambo la muhimu ambalo linatakiwa kuzingatiwa kwa wanafunzi ni kuhakikisha kuwa wanakuwa na uelewa wa elimu ili iwasaidie katika maisha yao.

  Alisema baadhi ya changamoto zinatakiwa kufanyiwa kazi ikiwemo marekebisho ya mitaala ya elimu ilenge kumsaidia mwanafunzi.

  Imeandikwa, Sharon Sauwa na Muhibu Said (Dodoma) na Raphael Kibiriti, Romana Mallya na Beatrice Shayo (Dar).  CHANZO: NIPASHE
   
 2. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  shule ya uhuru ya shinyanga ni ya miaka nenda rudi ni ya siki nyingi sana mimi binafsi nimeifahamu zaidi ya miaka 15 iliyopita na hata shule ya majengo ya moshi ni ya siku nyingi tu. Wananchi wanapaswa kufahamu hapa serikali inaleta siasa tu ku justify shule za kata zilizojengwa na LOWASSA. Ukweli ni kwamba shule nyingi zilizotajwa na pinda kuwa ni za kata ni za siku nyingi sijui ni kigezo gani kimetumika kuziita shule hizo za kata. Ni bora pinda angesema hata kama ni shule za kata basi ni zile zilizokuwepo siku nyingi na siyo zilizojengwa wakati wa LOWASSA.
   
 3. Mosachaoghoko

  Mosachaoghoko Senior Member

  #3
  Jul 2, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inchugu secondari ni ya muda murefu sana kwani sii mojawapo wa shule hizi zilizooteshwa kama uyoga hivyo haiwezekani kabisa kuiita ya kata je na ya tarafa wataiitaje sasa
   
 4. Ikumbilo

  Ikumbilo JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 455
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii habari inanipa raha sana. Yaani nimefurahi sana.
   
 5. M

  Masuke JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Ni kweli mkuu hiyo shule ya Uhuru ni ya zamani, kuna jamaa nimesoma naye A-level na tumemaliza 2001 na O-level kasoma uhuru, hata hiyo Bukandwe intake ya kwanza ni ama 97 au 98 maana imeanza mimi bado niko O-level.
  Wangetueleza shule za kata za lowasa au hata shule za kutwa nazo ni za kata bila kujali zilianzishwa lini.
   
 6. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2011
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Upuuzi mwingine wa wanasiasa na bunge lao. Haya mambo ya zawadi yanachangia sana kutuhalibia elimu yetu na miaka michache ijayo tutajadili tena juu ya uchafu wa aina hii;
  1. Walianza kutoa zawadi kwa walimu wakuu wa shule za serikali na kutoa adhabu kwa wale ambao shule zilianguka. Matokeo ikawa kila mkuu wa shule anahangaika kudanganya mitihani ili abaki kwenye u-head master
  2. Ikaja bodi ya mikopo ikisema inalipia div. 1 na 2 kwenye vyuo vikuu. Hapo tena wazazi wakaona ni safi kuiba mitihani hata kwa milioni 2 lakini mtoto akisha pata div 2 basi hatalipa chuo kikuu.

  3. Sasa wanaanza upuuzi mwingine wa ku-parade watoto bungeni na ahadi za zawadi. Subiri tu utaona maana shule za binafsi zilisha anza siku nyingi ikiwa ni sehemu ya matangazo ya biashara ya shule zao.

  Vijana kama hawa pongezi na zawadi lingebaki kuwa ni kazi ya familia zao na siyo kulifanya kama ni jambo la kitaifa. Mbona kwenye elimu ya juu hawaonekani kuwa kama wanavyoonekana huko sekondari? Kweli akili ya bunge haitoshi kiasi cha kutoona kuna tatizo.
   
 7. M

  MdogoWenu Senior Member

  #7
  Jul 2, 2011
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 173
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Kudesa ni janga la kitaifa.Miaka ya 60, 70 na hata katikati ya 80 ilikuwa vigumu kupata document yenye complete solutions za past papers.Sasa hivi kuna vitabu tele vina solutions za past paper kwa mfululizo hata wa miaka 20.Swali likirudiwa, una hakika gani kwamba aliyelifaulu aliwahi kulifanya kwa kuliona soln yake kwenye past paper.Matokeo yake huyaoni wanapofika Univesity maana huko nako ni hivyohivyo. Kudesa.Matokeo yake unayaona kazini ambako mtu hawezi kuelewa document yenye page 5. Kwa sababu huku hakuna solved past papers.Ndiyo wale tunao humu JF wanaopiga kelele eti thread ziwe fupi wakati tatizo ni poor reading speed combined with poor understanding speed.
   
 8. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #8
  Jul 2, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  mimi nakuunga mkono cose hawa tanzania one wakifika vyuoni huwa c tanzania one tena hapa sijui huwa inakuwaje. U tanzania one wao huwa unaishia kwenye matokeo ya secondary?
  Hapa kuna kusesa kwingi na kukaririshwa majibu ya mitihani.
   
 9. T

  T.K JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 345
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hata hiyo shule ya Majengo ya k'njaro ni ya muda mbona? Mwaka 2001 wakati nikiwa Moshi Tech hao wanafunzi wa Majengo tulikuwa tunakutana nao kwenye makongamano ya dini, na tulikuwa tunawashangaa sbb sisi tulikuwa tuanavaa suruali wao walikuwa wanavaa kaptula tena nakumbuka rangi ilikuwa "damu ya mzee" au labda mtu aniambie hapa ilijengwa shule nyingine ya "kata" na ikapewa jina sawa na hiyo iliyokuwepo.
   
 10. A

  ADAMSON Senior Member

  #10
  Jul 2, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umenifurahisha sana ukizingatia nimetoka kumaliza mitihani yangu leo saa tano asbh umeyasema yale niliyoya
  shuhudia
   
 11. notmar

  notmar Member

  #11
  Jul 2, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  eti majengo secondary ile shule maarufu pale moshi inayomilikiwa na RC leo ni shule ya kata! na brother P.lymo alikuwa mjengoni kuwakilisha.ama kweli wanasiasa wameshindwa kudanganya sasa wanajidanganya wenyewe...................................

  DUH!MAHELA YA KUTOSHA.......................................
   
 12. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hii ni kashfa nyingine kwa serikali ktokana na waziri wa elimu kulidanganya bunge kwa kuzitaja shule za kata ambazo sio za kata kwani zipo kwa miaka mingi na nyingine ni private kama majengo sec.

  Tulizoea kuona JK akidanganywa na wasaidizi wake mara kwa mara lkn naona awamu ni zamu ya waziri wake kudanganywa na wasaidizi wake.

  Kwanini viongozi wetu wanadanganyika kirahisi sana?
   
Loading...