Miaka miwili ya Rais Samia na siasa safi

Suphian Juma

Senior Member
Apr 2, 2019
133
546
Rais Samia ameikuta Nchi imetamalaki Siasa zilizojaa uadui na chuki zilizopitiliza. Nani ambaye hakumbuki ulishajengwa utamaduni Mpya kila mwenye Chama tofauti na wewe ni adui wako? Kila apandae jukwaani ni kueneza HATE SPEECH inayoambatana na vitisho vya kuuana dhidi ya wanaopingana na misimamo ya Chama chake? Na viongozi wa Chama na Serikali wanabariki kauli hizo ovu zinazokizana na Katiba na Sheria ya vyama vya Siasa?

Nahoji nani asiyekumbuka Ulinzi na Usalama wa mwanasiasa na Mwanaharakati uliondoka kutoka kwenye mikono ya dola salama na kumilikiwa na kundi ovu mithili ya Alshabab lilioitwa "watu wasiojulikana"?

Nani asiyekumbuka Wanasiasa wenye heshima kubwa katika nchi kama akina Mzee Kikwete, Mzee Makamba, Membe, Ridhiwani Kikwete, Nape Nnauye, Tundu Lissu, Zitto, Mbowe, Maalim Seif na wengine wengi walifanyiwa "Defamation" wazi wazi bila Soni wala haya na kutweza utu wao na akina Musiba na hakuna hatua yoyote ilichukuliwa na si tu na Chama Tawala wala Serikali?

Hamkumbuki hata mimi Suphian niliandikwa nafanya mapenzi ya Jinsia moja (Shoga), kwamba eti nafanya ushenzi huo na Wanasiasa Zitto na Hayati Maalim Seif? Kisa tu napingana na Utawala uliokuwa unasigina Katiba ya nchi, Demokrasia na Haki za Binadamu!!? Mnadhani Mwanamke wangu, Wazazi wangu, rafiki na jamaa zangu walijisikiaje?

Nani ambaye hakumbuki ilikuwa dhambi kubwa ya hata kufutwa uanachama ikibainika mwanasiasa wa Upinzani na na mwanachama wa Chama Tawala kuonekana hadharani wakishiriki jambo la kijamii au hata tu kutakiana kheri ya kuzaliwa kwenye mitandao ya kijamii au hata kukutwa wanakunywa kahawa pamoja kijiweni?

Nauliza nani amesahau habari za kila uchwao za wanasiasa, Wanaharakati na Waandishi kutekwa, kubambikizia kesi, na hata kuuawa na hakuna taarifa ya watuhumiwa kufikishwa mbele ya vyombo vya Sheria? Kichaka kinabaki tu "uchunguzi unaendelea"..!!?

Nahoji nani hakumbuki vyama vya Siasa vilipigwa "stop" kufanya mikutano ya hadhara kinyume na Sheria ya vyama vya Siasa ya mwaka 1992 na marekebisho yake na Katiba ya nchi iliyopo? Nani hakumbuki huko majimboni wabunge walikuwa wanatumia hadi vyombo vya Ulinzi na Usalama kutishia, kupigana ngumi hadharani na kuwakamata wagombea au wanasiasa kutoka vyama tofauti na vyao? Mimi mwenyewe nilishawahi kufuatwa na Polisi zaidi ya mara nne kwetu Kijijini Minyughe kwa agizo la OCD aliyepewa agizo na Mbunge kisa tu nafanya Shughuli zangu halali za kisiasa... Imagine!!

Nahoji mazingaombwe yote haya ya Kutekana, kubambikiziana kesi, kumchafuana, kutwezana utu yanapatikana katika ibara gani ya Katiba yetu? Katiba gani ya Chama cha Siasa? Sheria gani ya nchi? Ilani, Sera na Miongozo gani? Kama sio roho binafsi ya Kiongozi na genge lake aliyekengeuka kufuata Katiba ya Nchi na Katiba ya Chama chake...!!? Tumsifie? Chama kimtetee? Rais Samia amtetee? Aisee HAPANA abebe tu "zigo lake la Mavi" daima.

Rais Dkt Samia amekuja. Akaenenda katika Katiba, Sheria na Ustaarabu wa Kitanzania, Miaka miwili yake Ikulu hatujasikia mwanasiasa, mwanaharakati wala Mwanahabari ametekwa, amebambikiziwa kesi, amepigwa risasi, amehojiwa uraia wala kuuawa badala yake sote tunakunywa kahawa, tunahoji, tunakosoa Serikali hatufungwi, tunafanya mikutano ya hadhara na wala hatuonani maadui kisa tuna vyama Tofauti. Sote tunalindwa sawia na vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Sio hivyo tu, Mhe. Rais Samia amekubali Sheria zote kandamizi za kisiasa kwenda kurekebishwa kama sio kufutwa kabisa, pamoja na kukubali Mchakato wa kuunda Katiba Mpya kuanzishwa ili kuruhusu mazingira ya Uhuru, Haki na aminifu ya ushindani wa kisiasa baina ya vyama vya Siasa kama ambavyo Katiba na Sheria ya vyama vya Siasa ya mwaka 1992 inavyoelekeza.

Suphian Juma Nkuwi,

Kada wa CCM,

Machi 19, 2023

Simu: +255717027973

IMG_20230120_111916.jpg
 
MIAKA MIWILI YA RAIS SAMIA NA SIASA SAFI.

Mhe. Rais Samia amekubali Sheria zote kandamizi za kisiasa kwenda kurekebishwa kama sio kufutwa kabisa, pamoja na kukubali Mchakato wa kuunda Katiba Mpya kuanzishwa ili kuruhusu mazingira ya Uhuru, Haki na aminifu ya ushindani wa kisiasa baina ya vyama vya Siasa kama ambavyo Katiba na Sheria ya vyama vya Siasa ya mwaka 1992 inavyoelekeza....
Naunga mkono hoja
P
 
Kwani Sufiani ulipojiunga CCM Toka ACT ulikuwa unasifu Nini?

Samia akiachia madaraka utakuja Tena utuambia maisha yalivyo magumu kwa wananchi?

Siasa zako sizani kama zinamwanga huko mbele.

You are too much.

Kati ya vitu Wana siasa waliikosa wakati ule ni kunyimwa mwanya wa kula keki ya taifa kizembe kizembe. Sasa hivi wanalamba asali kimya.
 
Rais Samia ameikuta Nchi imetamalaki Siasa zilizojaa uadui na chuki zilizopitiliza. Nani ambaye hakumbuki ulishajengwa utamaduni Mpya kila mwenye Chama tofauti na wewe ni adui wako? Kila apandae jukwaani ni kueneza HATE SPEECH inayoambatana na vitisho vya kuuana dhidi ya wanaopingana na misimamo ya Chama chake? Na viongozi wa Chama na Serikali wanabariki kauli hizo ovu zinazokizana na Katiba na Sheria ya vyama vya Siasa?

Nahoji nani asiyekumbuka Ulinzi na Usalama wa mwanasiasa na Mwanaharakati uliondoka kutoka kwenye mikono ya dola salama na kumilikiwa na kundi ovu mithili ya Alshabab lilioitwa "watu wasiojulikana"?
20230317_125131.jpg


Nimewakuta huko kitaa
 
Back
Top Bottom