Miaka miwili ya Dr. Shein na hatma ya CUF, Je jumuiya ya kimataifa imeitupa mkono Zanzibar ?

Kishada ni alijojo, subiri 2019 utupe karata yako kwenye polling box using'ang'anie hayo maelezo yako ya hoja za nguvu!
 
Wewe Kishada jiongeleshe tu hapa hamna mtu anaetazama CUF kama mtazamo wako ulivo, Cuf imelala Lipumba tu mmoja amewakalisha watawezaje mziki wa CCM chama dola. Kuhusu hatma ya Zanizbar i believe you know the drill.
 
Wewe Kishada jiongeleshe tu hapa hamna mtu anaetazama CUF kama mtazamo wako ulivo, Cuf imelala Lipumba tu mmoja amewakalisha watawezaje mziki wa CCM chama dola. Kuhusu hatma ya Zanizbar i believe you know the drill.

Sasa mbona inaonesha kama hii mada inakuchoma. Tunajadili tu, nini mtazamo wako na hatma ya Zanzibar ? Hapa unasifia chama dola mwenyewe unauita mziki. Usisusie mada hiyo drill ieleze kwa faida yawana JF
 
KISHADA SIJAELEWA UNATAKA NINI NAKUONA UNATAKA KUTU-REMOTE TUFUATE UNACHOAMINI WEWE

Sasa si leta mawazo mbadala kama unayo. Kwani kishada umemuelewa vipi wewe ?
Mada inajaribu kuangalia mustakbali wa Zanzibar kuelekea huko mbele na sintofahamu ya uchaguzi, na aidha kujadili hatma ya CUF kama chama cha siasa jee kitakuwaje ikiwa hakukutokea mabadiliko yoyote kwenye ZEC na kwenye serikali iliohali walishawaaminisha wanachama waKE KUWA HAKI YAO ITAPATIKANA hapa hujaelewa nini ?
 
Kwanza ukiangalia historia ya chama cha cuf mara nyingi utaona ni watu wanaosimamia na wasiotetereka katika misimamo yao. Juhudi unazoziita za kimataifa zipo na hazikuanzia leo ingawa mara hii zimekuwa na kasi ya ajabu na athari kubwa kwa pande zote za muungano kwa sababu aliyoyafanya babu jecha ilikuwa ni ujambazi wa wazi kabisa. Angalia tu kidogo wala sio sana athari yake utaikuta hata Tanganyika kwenyewe. Nikuhakikishie Juhudi hizi za Mataifa zitazaa matunda. Hilo halina shaka kabisa. Diplomasia maamuzi yake huwa yanachelewa sana lakini huwa ni uhakika na jamaa wanaonekana kushinda.

Unajaribu sana kwenda kwenye mada asante. Hata hivyo unadhani CUF itahimili tena wimbi la 2020 ikiwa mazingira ya kisiasa na uchaguzi hayatabadilika kule Zanzibar ? CCM na dr Shein wao hawana habari wanasema wakutane 2020 na CCM inakwenda kushinda kwa urahisi. Na wanasema hizo kauli eti sijui jumuiya gani eti itawapa dola hizo ni za kuwafariji wanachama tu . Nini kinasapa jeuri hii hawa viongozi ambao wenyewe ni watuhumiwa wa kupora haki za watu, unafikiri hii trends ni ya bure ?
 
Binafsi sioni njia nyepesi kwa CUF na uhai wa chama ikiwa juhudi zao hazitabadilisha mazingira kabla ya 2020, Kilicho wazi ni kitu kimoja watawala wa CCM kadiri siku zinavyiokwenda ndio wanajianika kimatyaifa kuhusu suala la Zanzibar. ikiwa walifika mahala walifuta uchaguzi wote na kufanya wa kwao wanaoutaka mbele ya macho ya ulimwengu na kushindwa kuthibitisha mantiki ya kufuta uchaguzi ule , si hayo kuthubutu kufanya uchaguzi ule wa marejeo na kuanika vifaa vya kijeshi ili kuingia kwenye utawala basi si bure, Huku ni wazi ni kuishiwa mikakati ya kidiplomasia na sasa wanadiplomasia wote wanaitazama Dunia kuelekea hio 2020. Tunatazama nini kitafuata baada ya kila upande kushikilia msimamo wake ?
 
Jee hapa hakuna muunganiko wa Diplomasia yetu kuibeba CCM na watawala kulipuuzia suala la Zanzibar ? Kwa mfano Role ya Wizara ya mambo ya nje ya Tanzania kule UN na Balozi mbali mbali, hazijatumika kufunika kombe na kulainisha jumuiya za kimataifa kwa Maslahi ya CCM labda ?
Balozi Mahiga?

Link http://www.mwananchi.co.tz/Wagombea-urais-11-CCM-wapewa-kazi-Serikalini-/-/1596774/3165442/-/mtl8lk/-/tzwebmail.tz.nationmedia.com%3A9090owa

Wewe unaauliza kama India wanapenda na kutumia mbaazi?

Hiyo kitu haitaki darubini kuiona.
 
unazungumza dunia ipi wewe ? Point yako ni nini ?
Ninahofahamu sizungumzii "Alternate Universe" yako wewe ndiyo maana unashindwa kuniafahamu.. my point is clear nobody care kama znz kuna mgogoro sipokuwa nyinyi tu na kila leo mnapiga picha na wazungu kuwadanga watu eti mko mbioni kutafuta haki yenu na karibu mtapewa wakati hao mnaopiga piha nao hawana umuhimu wowote. subiri 2020 na jiandae kisaikolojia kwani kipigo chaja
 
Ninahofahamu sizungumzii "Alternate Universe" yako wewe ndiyo maana unashindwa kuniafahamu.. my point is clear nobody care kama znz kuna mgogoro sipokuwa nyinyi tu na kila leo mnapiga picha na wazungu kuwadanga watu eti mko mbioni kutafuta haki yenu na karibu mtapewa wakati hao mnaopiga piha nao hawana umuhimu wowote. subiri 2020 na jiandae kisaikolojia kwani kipigo chaja

Hapo ndipo ninaposhangaa. yaani ulitaka uone watu wanapambana na kufukuzana, kususiana na kuuana ndio uamini kuwa kuna mgogoro Zanzibar ? Nimekuuliza uko dunia gani wewe ina maana hujuwi kuwa Tanzania ilisusiwa kupewa misaada na baadhi ya nchi wakitaka mgogoro wa uchaguzi uwekwe sawa kwa suala la Zanzibar.
 
Umesema juhudi zinaendelea sawa. Nadhani hili ni kuhusu jumuiya ya kimataifa. sasa mkuu ikitokezea juhudi hazikuzaa matunda ipi itakuwa hatma ya CUF kule Zanzibar na Tanzania wategemee miujiza gani ?

Kwanini utegemee juhudi hazikuzaa matunda na usitegemee juhudi zizae matunda.

Nadhan tusubiri mkuu usiwe na pupa 2020 si mbali na maalim seif huwa anatamka mara kwa mara akishindwa atarudi kwa wananchi kuwaeleza na bila shaka kutakuwa na hatua nyengine CUF wanaweza kuchukua badala yake.
 
Back
Top Bottom