Miaka miwili ya Dr. Shein na hatma ya CUF, Je jumuiya ya kimataifa imeitupa mkono Zanzibar ?

Endelea na ushabiki.

Unamuuliza mpika pilau eti umeweka chakula cha wapishi ? Maajabu leo Tume iliyoundwa na CCM , ikachaguliwa mwenyekiti kada wa CCM, Ifute uchaguzi wote bila ushahidi wowote wa maana kwa maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM ambaye ni rais na amir jeshi Mkuu wa JMT, Halafu ujipe matumaini eti tume imtangaze mpinzani huo ni umwehu.

Mnachokifanya CCM bara na Zanzibar mnakijuwa wenyewe hapo hatujadili maana tunajuwa kuwa mmeapa hamtoi kwa vikaratasi vya kura sisi huko hatujadili. .

Hapa tunazungumzia hizi jumuiya za kimataifa ziko wapi au ndio zimeitelekeza Zanzibar ?
Ukiona zimekaa kinywa ujue kila kitu kiko poa na wameridhika na hali iliyokuwepo hivi sasa. mlijitahidi kwenda kupiga picha umoja wa Mataifa na kuwadanganya jamaa zangu wa chokocho na Gando lakini matokeo yake ndiyo unayoyaona hivi sasa. siku zote njia ya muongo ni fupi.sijui hivi sasa anasema nini kwani kila baada ya miezi 3 maalim lazima awape drip misukule yake hahahahaa Kishada unakaribishwa ukongoroni njo unywe juice ya ukwaju
 
Mkuu mie naona suala la Zanzibar au hata mambo yanayoendelea kufukuta kwenye nchi za Kiafrika yanatakiwa kumalizwa na wananchi wa nchi husika kwa maridhiano na kuwa na utashi wa kisiasa. Haya mambo kupereka jumuhia za kimataifa hayatasaidia chochote hasa kama hakuna interest ya kiuchumi kwa hayo mataifa. Unakumbuka suala la Africa ya Kati wamechinjana mpaka wakapata akili ya kumaliza mambo yao wenyewe. Huku jumuhia hizo zipo lakini kwa kuwa hakuna interest za kiuchumi kwao hawana msaada.
Back to suala la Zanzibar, Seif alidanganyika (kudanganywa) kususia uchaguzi (hata kama ilikiwa na mushkel) akidhani jumuhia za kimataifa watakuja kumtoa Shein madarakani na kuwekwa yeye. Bora angekuwa na wabunge wake wa kuisemea kwenye baraza lao. Kwa hali hii ilivyo, Seif was the architect of his own downfall.
Seif kushiriki uchaguzi wa marudio ingekuwa sawa na kubariki uchafu wa Jecha. Uamuzi wa kutoshiriki ulibarikiwa na Wanzazibari wote.
 
Udini unatumika kila pahali duniani kuleta fitna, usiwaamini watu weupe kwenye mambo hayo.
Oooooh.... So kinana na dr shein ni watu weupe? Matatizo yenu waafrika mnashindwa kuyatatua mnawasingizia watu wengine na ndo maana miaka na miaka matatizo hayaishi sababu ya kukosa akili za kutatua na badala yake kusingizia watu wengine
 
Hoja ya kisomi sana na nzito pia. Sina cha kuongea, natafakari tu ushetani uliofanyika kule Zanzibar na kama Jecha ataingia akhera au jehanamu
 
Kishada ni mawazo yako na Kizibao ni mawazo yake, Kishada usilazimishe mawazo yako ayakumbatie Kizibao. Hata mimi nasema Jamshid au jamaa zake hawatokuja kurudisha ufalme wa kiarabu hapa visiwa vya Zanzibar sahau kabisà bwana Kishada. Jumuia ya Kimataifa haitashughulika na upuudhi wa Maalimu Seif Sharifu Hamad kama ule unaorudiwarudiwa na Radio Swahiba FM Mbweni na kujibiwa na Raisi Shein kuwa wataanzia wapi na watamalizia wapi. kwa sasa ni serikali iliyopo ya CCM mpaka 2020.
 
Kumbe niingie! Haya sikia CUF hasa ile isiyotambuliwa na msajili ni kikundi chenye nia ya kumrudisha sultan tuliyempindua 1964.
Haita kuja itokea chama hicho kushinda uchaguzi
Mbona inatokea sana mkuu lakini kwa vile mpo karibu na shetani na hamtaki haki mnabiruwa matokeo, mwaka gani mlishinda? Ndio maana viongozi wenu siku za ijumaa wakiingia msikitini mnasusiwa msali wenyewe manaki ni wanafiki tu
 
Kishada ni mawazo yako na Kizibao ni mawazo yake, Kishada usilazimishe mawazo yako ayakumbatie Kizibao. Hata mimi nasema Jamshid au jamaa zake hawatokuja kurudisha ufalme wa kiarabu hapa visiwa vya Zanzibar sahau kabisà bwana Kishada. Jumuia ya Kimataifa haitashughulika na upuudhi wa Maalimu Seif Sharifu Hamad kama ule unaorudiwarudiwa na Radio Swahiba FM Mbweni na kujibiwa na Raisi Shein kuwa wataanzia wapi na watamalizia wapi. kwa sasa ni serikali iliyopo ya CCM mpaka 2020.

Mkuu kwani mimi nimesema lipi baya ? mimi sijasema kuwa Jamsidi atarudisha ufalme ZANZIBAR, MTAFUTE ALIYESEMA HIVYO.

Hapo kwenye jumuiya ya kimataifa kutoshughulika na unaouita upuuzi wa Maalim Seif ndio tuanzie kama mada inavyojieleza.

Kwa nini wewe unauona ni upuuzi ?
 
Mada itusaidie kujadili ikiwa ndio Zanzibar imeachwa mkono ama la , na itusaIDIE KUJADILI NAFASI YA cuf KUELEKEA 2020 na hatma yake ikiwa hakutafanywa mabadiliko yoyote . Na vile vile tujadili hatma ya Zanzibar huko mbele .
 
Ukiona zimekaa kinywa ujue kila kitu kiko poa na wameridhika na hali iliyokuwepo hivi sasa. mlijitahidi kwenda kupiga picha umoja wa Mataifa na kuwadanganya jamaa zangu wa chokocho na Gando lakini matokeo yake ndiyo unayoyaona hivi sasa. siku zote njia ya muongo ni fupi.sijui hivi sasa anasema nini kwani kila baada ya miezi 3 maalim lazima awape drip misukule yake hahahahaa Kishada unakaribishwa ukongoroni njo unywe juice ya ukwaju

Ndio Mkuu. Kwa hio kama nchi hakuna tatizo lolte la kidiplomasia kwa yaliyotokea 2015 ? tuseme sawa. Ndio kusema jumuiya ya kimataifa imeshindwa na mgogoro wa Zanzibar ? na ipi hatma ya Zanzibar kwa migogoro hii ya chaguzi ?
 
Asili ya muungano ni kuidhibiti ZNZ hapa ndipo kwenye kiini cha tatizo.

Inawezekana labda.
Nilikuwa najiuliza Kimataifa Tanzania ndio inajulikana na ndio imefunga mikataba ya kimataifa na masharti ya UN, Zanzibar ina utawala wake wa ndani. Nikajiuliza kwa nini Matatizo ya Zanzibar hayapati nguvu kutatuliwa moja kwa moja kupitia jumuiya za kimataifa na inayotambuliwa ni Tanzania. Hapa Muungano unahusika kudhoofisha Haki na demoklrasia Zanzibar. Nimekufahamu Mkuu.
 
Back
Top Bottom