Miaka miwili ya Dr. Shein na hatma ya CUF, Je jumuiya ya kimataifa imeitupa mkono Zanzibar ?

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Tokea kufanyika kile kilichoitwa uchaguzi wa marudio mwezi Machi, 2016, sasa ni takribani miaka miwili na miezi miwili ya uongozi wa DR Shein kule Zanzibar. Muda unaenda kwa kasi sana.
Kuna masuali mengi ya kujiuliza hapa.

IPI HATMA YA CUF ?

Kwanza ipi hatma ya CUF ambayo baada ya kumaliza uchaguzi ule waliousisia waliwaaminisha wazanzibari kwamba haki yao ya uchaguzi wa 2015 uliofutwa na Jecha itapatikana na wenyewe walielekeza nguvu zao kupitia jumuiya ya kimataifa hasa kwa kujiweka karibu na taasisi za kimarekani na Uengereza. Jee kwa kile kinachoendelea kuna uwezekano wa kutokea mabadiliko yoyote ya kurejheshwa haki hiyo ? na jee ikiwa hilo halikufanikiwa na mazingira ya uchaguzi ya 2020 yakafanyika bila kutokea mabadiliko ya kimfumo kwenye ZEC na Serikali nini itakuwa hatma ya CUF ?

JEE JUMUIYA YA KIMATAIFA IMEITUPA MKONO ZANZIBAR NA CUF ?
Hili ni suali muhimu, wadau wa uchaguzi wa kimataifa ni UN, kupitia taasisi yake ya UNDP, mataifa makubwa na mashirika yao ya kutetea demokrasia na haki, nchi moja moja na washirika wa maendeleo na marafiki. Zanzibar imekumbwa na tufani ya kisiasa kwa muda mrefu na hakujawa na usawa wa mazingira ya ushindani ya uchaguzi huru na haki kwa wadau , kiasi kwamba kumetokezea mitafaruku na hata mauaji na uvunjifu wa haki za binadamu.

Tuliona jitihada za awali za jumuiya ya Madola baada ya uchaguzi wa 1995 kupitia msuluhishi Chief Ameka Anyauku, ikifuatiwa na miafaka iliyofeli ya 1995, 2000 n.k. Miafaka hii bila shaka ilitiliwa nguvu na Jumuiya za kimataifa mbali mbali.

Hata hivyo, wadau wa demokrasia walidhani SULUHU ya kuingiza maridhiano Kwenye KATIBA YA ZANZIBAR, kupitia mabadiliko ya katiba ya mwaka 2009 chini ya Utawala wa Dr Karume itakuwa Muarubaini wa Matatizo ya Zanzibar kwa washindani kushirikiana kuongoza nchi kwa ulingano wa kuchaguliwa jambo ambalo lilifanya kazi kwa miaka mitano tu 2010 - 2015.

Kinachoshuhudiwa ni kurudi kwa migogoro kama awali huku kukiwa na malalamiko ya chama Dola (CCM ) kutokubali kufuata misingi ya umoja wa kitaifa kwenye Chaguzi na hatimae migogoro kuendelea licha ya JITIHADA KUBWA ZA NDANI NA KIMATAIFA.

Kwa sasa ni zaidi ya miaka miwili ya uongozi wa Dr Shein, Hatusikii masindikizo wala hatuoni jitihada za wazi za jumuiya ya kimataifa kuhusu hali ya Zanzibar. Muda umekwenda kuna ukimya . Jee kwa muhtasari huo tunaweza kusema Jumuiya ya Kimataifa imeshindwa na kuamua kuitupa mkono Zanzibar ?

Tunahitaji wataalamu na wajuzi wa siasa na diplomasia watusaidie maana ikiwa hali itakuwa hivi ilivyo nini itakuwa hatma ya Zanzibar huko mbele ?

Kishada.
 
Tafadhali ingia kwenye mada kwa faida ya wengine.
Kumbe niingie! Haya sikia CUF hasa ile isiyotambuliwa na msajili ni kikundi chenye nia ya kumrudisha sultan tuliyempindua 1964.
Haita kuja itokea chama hicho kushinda uchaguzi
 
Tuweke sawa kwa faida ya wana JF. Hapa unazungumzia CUF kushinda au Kutopewa nchi kutawala ?
 
Kumbe niingie! Haya sikia CUF hasa ile isiyotambuliwa na msajili ni kikundi chenye nia ya kumrudisha sultan tuliyempindua 1964.
Haita kuja itokea chama hicho kushinda uchaguzi

Ukishajibu hapo juu. Sasa njoo kwenye mada. Nini hatma ya CUf na nini hatma ya Zanzibar hapo mbele huko ndiko tunakotaka mawazo yako sio ishu ya Sultani.
 
Tokea kufanyika kile kilichoitwa uchaguzi wa marudio mwezi Machi, 2016, sasa ni takribani miaka miwili na miezi miwili ya uongozi wa DR Shein kule Zanzibar. Muda unaenda kwa kasi sana.
Kuna masuali mengi ya kujiuliza hapa.

IPI HATMA YA CUF ?

Kwanza ipi hatma ya CUF ambayo baada ya kumaliza uchaguzi ule waliousisia waliwaaminisha wazanzibari kwamba haki yao ya uchaguzi wa 2015 uliofutwa na Jecha itapatikana na wenyewe walielekeza nguvu zao kupitia jumuiya ya kimataifa hasa kwa kujiweka karibu na taasisi za kimarekani na Uengereza. Jee kwa kile kinachoendelea kuna uwezekano wa kutokea mabadiliko yoyote ya kurejheshwa haki hiyo ? na jee ikiwa hilo halikufanikiwa na mazingira ya uchaguzi ya 2020 yakafanyika bila kutokea mabadiliko ya kimfumo kwenye ZEC na Serikali nini itakuwa hatma ya CUF ?

JEE JUMUIYA YA KIMATAIFA IMEITUPA MKONO ZANZIBAR NA CUF ?
Hili ni suali muhimu, wadau wa uchaguzi wa kimataifa ni UN, kupitia taasisi yake ya UNDP, mataifa makubwa na mashirika yao ya kutetea demokrasia na haki, nchi moja moja na washirika wa maendeleo na marafiki. Zanzibar imekumbwa na tufani ya kisiasa kwa muda mrefu na hakujawa na usawa wa mazingira ya ushindani ya uchaguzi huru na haki kwa wadau , kiasi kwamba kumetokezea mitafaruku na hata mauaji na uvunjifu wa haki za binadamu.

Tuliona jitihada za awali za jumuiya ya Madola baada ya uchaguzi wa 1995 kupitia msuluhishi Chief Ameka Anyauku, ikifuatiwa na miafaka iliyofeli ya 1995, 2000 n.k. Miafaka hii bila shaka ilitiliwa nguvu na Jumuiya za kimataifa mbali mbali.

Hata hivyo, wadau wa demokrasia walidhani SULUHU ya kuingiza maridhiano Kwenye KATIBA YA ZANZIBAR, kupitia mabadiliko ya katiba ya mwaka 2009 chini ya Utawala wa Dr Karume itakuwa Muarubaini wa Matatizo ya Zanzibar kwa washindani kushirikiana kuongoza nchi kwa ulingano wa kuchaguliwa jambo ambalo lilifanya kazi kwa miaka mitano tu 2010 - 2015.

Kinachoshuhudiwa ni kurudi kwa migogoro kama awali huku kukiwa na malalamiko ya chama Dola (CCM ) kutokubali kufuata misingi ya umoja wa kitaifa kwenye Chaguzi na hatimae migogoro kuendelea licha ya JITIHADA KUBWA ZA NDANI NA KIMATAIFA.

Kwa sasa ni zaidi ya miaka miwili ya uongozi wa Dr Shein, Hatusikii masindikizo wala hatuoni jitihada za wazi za jumuiya ya kimataifa kuhusu hali ya Zanzibar. Muda umekwenda kuna ukimya . Jee kwa muhtasari huo tunaweza kusema Jumuiya ya Kimataifa imeshindwa na kuamua kuitupa mkono Zanzibar ?

Tunahitaji wataalamu na wajuzi wa siasa na diplomasia watusaidie maana ikiwa hali itakuwa hivi ilivyo nini itakuwa hatma ya Zanzibar huko mbele ?

Kishada.
Hahahahaa KISHADA naona bado unaenelea kuweweseka. si ulituambia hapa mwaka haumalizi Shein ataondoshwa madarakani? Serikali ya ZNZ ni ya umoja wa kitaifa ambayo inajumuisha vyama 4 angalia baraza la mwaziri la znz..
Pole sana 2020 siyo mbali kama bado seif atakuwa yupo CUF
 
Ingependeza ukaonesha wapi nilisema mwaka haumalizi Shein ataondoshwa madarakani. Jitahidi kufahamu haya machapisho.

Hebu twambie huo Umoja wa kitaifa wa Serikali ya Shein umetumia katiba gani kuunda serikali na vyama ambavyo havina uwakilishi wowote ?

Lakini twambie hatma ya CUF na hatma ya Zanzibar na jee jumuiya ya Kimataifa imeitupa Zanzibar ? Huku ndio tunataka mawazo yako.
 
Tunahitaji mitazamo yenye hoja kwa ajili ya kuchangamsha mjadala wetu. Tusitazame mambo haya kwa jicho la kushinda na kushindwa kwa mnasaba wa kishabiki. Ipi hatma ya Zanzibar ?
 
Kwa mfano kurudi kwa mgogoro wa Zanzibar baina ya wadau wakubwa wa kisiasa wa CCM na CUF licha ya KATIBA kuweka suluhu , ni ishara mbaya na kiashiria cha uwezekano wa kutokea umwagikaji damu huko mbele HASA PALE WADAU HAO WATAKAPOTUNISHIANA MISULI. Iko wapi dhima ya jumuiya ya kimataifa. Jee Zanzibar itaweza kuepuka tena mara hii machafuko ?
 
Jumuia za kimataifa haiwezi kuwasaidia Wazanzibar, fitna za kidini zina nguvu sana.

Unanikumbusha waraka wa kinana wa kuihusisha CUf na ugaidi na kutaka wasipate uungwaji mkono kuelekea uchaguzi wa 2015. Tuseme Udini ndio umetumiwa na jumuiya ya kimataifa kupuuzia hali ya Zanzibar ?
 
Udini unatumika kila pahali duniani kuleta fitna, usiwaamini watu weupe kwenye mambo hayo.
 
Kwa hivyo tunaweza kuhitimisha hivyo kuwa Jumuiya za kimataifa zimetupa madai na kuisimamia Zanzibar kwenda kwenye mkondo unaotakiwa kwa sababu za kidini ?
 
Jee hapa hakuna muunganiko wa Diplomasia yetu kuibeba CCM na watawala kulipuuzia suala la Zanzibar ? Kwa mfano Role ya Wizara ya mambo ya nje ya Tanzania kule UN na Balozi mbali mbali, hazijatumika kufunika kombe na kulainisha jumuiya za kimataifa kwa Maslahi ya CCM labda ?
 
Kumbe niingie! Haya sikia CUF hasa ile isiyotambuliwa na msajili ni kikundi chenye nia ya kumrudisha sultan tuliyempindua 1964.
Mbina CCM ndio wanaorudisha wale masultan waliowapindua? Tatizo mnakaa kijijini nyie mnasikiliza redio za betri bado, si ajabu bado unaamini nyerer yuko hai!!! :D juzi hapa visiwani ulikuja ujumbe wa Sulatn huyo unaemchukia, Serikali ya CCM, iliifunga bandari na kukawa hakuna kazi mpaka meli ya Sultan ilivoondoka....Huyo Maalim ata hakushuhulika na ugeni uo alikuwa na yake.

Kwaio ni CCm wenyewe ndioo wanaowapaptikia masultan. Uko kwenu msi mlikuwa mkiuzana kwa kuoneshwa vioo tu
 
Lakini tuitazame Zanzibar kama sehemu ya Tanzania / nchi, kwenye muungano wetu. Jee huu muungano hauhusiki kuwazuiya wavunja demokrasia kutokushughulikiwa kule Zanzibar. Maana Zanzibar nje ya Tanzania haijulikani kama nchi na mwanachama wa UN. Hili nalo sio tatizo kwa kutobanwa kufuata Mikataba ya Kimataifa ikiwemo Haki za binadamu ?
 
Kuna mifano mingi kuonesha Suala la Zanzibar limetupwa. Marekani na uengereza baada ya kumaliza uchaguzi wa 2015 walizuiya baadhi ya misaada ya maendeleo kwa Tanzania mnakumbuka ile misaada ya MCC, na tuliona wakitoa matamko mara baada ya kufutwa ule uchaguzi na Jecha kutaka ZEC imalizie matokeo ya uchaguzi wa 2015 yaliyokuwa bado hayajatamngazwa lakini yalishajumuishwa. Leo hii msimamo ni upi ? Inasemekana nchi hizo na kupitia Jumuiya ya Ulaya zimeahidi kutoa mabilioni ya shilingi kwa ajili ya maendeleo. Hii ni mifano ya wazi kuwa Suala la Zanzibar limetupwa. Au kuna kilichojificha ?
 
Tunahitaji mitazamo yenye hoja kwa ajili ya kuchangamsha mjadala wetu. Tusitazame mambo haya kwa jicho la kushinda na kushindwa kwa mnasaba wa kishabiki. Ipi hatma ya Zanzibar ?
Kweli Mkuu,lakini umesikia kauli za kina Lukuvi kuhusu Zanzibar na dini ya Kiislam,propaganda ya kuwa ugaidi utapitia pwani za Zanzibar kama Zanzibar haitadhibitiwa ndio zinazosambazwa na wenzetu wa Tanganyika kwa jumua za kimataifa,Uislam unapigwa vita kila kona,binafsi sifikirii kama wana nia ya kuisaidia Zanzibar ili kutatua hali ya kisiasa hapa Zanzibar.,wanaenda Zanzibar ibaki kama ilivyo

Seif Sharifu amejitahidi sana kupigania maslahi ya Zanzibar na wazanzibari,mungu atamlipa,wazanzibari watamkumbuka,lakini kumbuka mkuu madhumuni ya mapinduzi ya Zanzibar yalikwa kudhibiti Uislam,huo ndio ukweli usiofichika,historia za mapinduzi ya Zanzibar imeweka wazi.,Nyerere alishawahi kusema kuwa kama angelikuwa na uwezo visiwa vya Zanzibar angelivitupa mbali sana..

Wazanzibari watawala(CCM Zanzibar) ambao ni wachache ambao wengi wao wana asili ya Tanganyika wamejazwa propaganda kuwa Sultan atarudi,humu katika huu uzi ukisoma "comments" za watu wengine utashanga kuwa mpaka hii miaka tunayoishi bado mtu anakubali kuwa warabu watarudi Zanzibar..

Chakufanya ni wazanzibari wenyewe wapiganie nchi yao kama walivyompindua mkoloni Sultan,wajipange wampindue mkoloni CCM,kila kitu kina ugumu wake lakini hakuna kisichowezekana,,
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom