Miaka miwili ya Dr. Shein na hatma ya CUF, Je jumuiya ya kimataifa imeitupa mkono Zanzibar ?

Muungano unapohusishwa na kudhoofisha Haki na demokrasia Zanzibar inafanana. Ule uchaguzi wa 2015 lilitumika jeshi letu (JWTZ) kuvamia kule kituo cha majumuisho Bwawani na Polisi kumchukua Makamo Mwenyekiti wa ZEC jaji Hamid na kumpeleka Kituoni , Hafla JECHA aliyewaambiwa wenzake kuwa alikuwa anaumwa na Tumbo siku hiyo kwa hivyo angeshindwa kuja Kazini kutangaza Matokeo ghafla akaonekana kwenye televisheni ya ZBC sehemu isiyojulikana akifuta uchaguzi peke yake.

Hata uchaguzi wa marudio kulionekana Vifaru vya JWTZ mitaani vikitisha watu.

Jeshi chombo cha muungano kilitumika kudhoofisha Haki za Watu kule Zanzibar. Huu MUUNGANO HUU .
 
Tokea kufanyika kile kilichoitwa uchaguzi wa marudio mwezi Machi, 2016, sasa ni takribani miaka miwili na miezi miwili ya uongozi wa DR Shein kule Zanzibar. Muda unaenda kwa kasi sana.
Kuna masuali mengi ya kujiuliza hapa.

IPI HATMA YA CUF ?

Kwanza ipi hatma ya CUF ambayo baada ya kumaliza uchaguzi ule waliousisia waliwaaminisha wazanzibari kwamba haki yao ya uchaguzi wa 2015 uliofutwa na Jecha itapatikana na wenyewe walielekeza nguvu zao kupitia jumuiya ya kimataifa hasa kwa kujiweka karibu na taasisi za kimarekani na Uengereza. Jee kwa kile kinachoendelea kuna uwezekano wa kutokea mabadiliko yoyote ya kurejheshwa haki hiyo ? na jee ikiwa hilo halikufanikiwa na mazingira ya uchaguzi ya 2020 yakafanyika bila kutokea mabadiliko ya kimfumo kwenye ZEC na Serikali nini itakuwa hatma ya CUF ?

JEE JUMUIYA YA KIMATAIFA IMEITUPA MKONO ZANZIBAR NA CUF ?
Hili ni suali muhimu, wadau wa uchaguzi wa kimataifa ni UN, kupitia taasisi yake ya UNDP, mataifa makubwa na mashirika yao ya kutetea demokrasia na haki, nchi moja moja na washirika wa maendeleo na marafiki. Zanzibar imekumbwa na tufani ya kisiasa kwa muda mrefu na hakujawa na usawa wa mazingira ya ushindani ya uchaguzi huru na haki kwa wadau , kiasi kwamba kumetokezea mitafaruku na hata mauaji na uvunjifu wa haki za binadamu.

Tuliona jitihada za awali za jumuiya ya Madola baada ya uchaguzi wa 1995 kupitia msuluhishi Chief Ameka Anyauku, ikifuatiwa na miafaka iliyofeli ya 1995, 2000 n.k. Miafaka hii bila shaka ilitiliwa nguvu na Jumuiya za kimataifa mbali mbali.

Hata hivyo, wadau wa demokrasia walidhani SULUHU ya kuingiza maridhiano Kwenye KATIBA YA ZANZIBAR, kupitia mabadiliko ya katiba ya mwaka 2009 chini ya Utawala wa Dr Karume itakuwa Muarubaini wa Matatizo ya Zanzibar kwa washindani kushirikiana kuongoza nchi kwa ulingano wa kuchaguliwa jambo ambalo lilifanya kazi kwa miaka mitano tu 2010 - 2015.

Kinachoshuhudiwa ni kurudi kwa migogoro kama awali huku kukiwa na malalamiko ya chama Dola (CCM ) kutokubali kufuata misingi ya umoja wa kitaifa kwenye Chaguzi na hatimae migogoro kuendelea licha ya JITIHADA KUBWA ZA NDANI NA KIMATAIFA.

Kwa sasa ni zaidi ya miaka miwili ya uongozi wa Dr Shein, Hatusikii masindikizo wala hatuoni jitihada za wazi za jumuiya ya kimataifa kuhusu hali ya Zanzibar. Muda umekwenda kuna ukimya . Jee kwa muhtasari huo tunaweza kusema Jumuiya ya Kimataifa imeshindwa na kuamua kuitupa mkono Zanzibar ?

Tunahitaji wataalamu na wajuzi wa siasa na diplomasia watusaidie maana ikiwa hali itakuwa hivi ilivyo nini itakuwa hatma ya Zanzibar huko mbele ?

Kishada.

Juhudi zinaendelea ata kama imebaki wiki 1

32207703_1670145586437709_8895590616839225344_n.jpg

31969853_1859870760713602_537994647243325440_o.jpg

31960942_1859868957380449_1019846328101896192_o.jpg

31960495_1859873380713340_5359816471818010624_o.jpg
 
Panapokuwa na uongozi usioridhisha katika nchi moja, Serikali za mataifa makubwa uiwekea vikwazo nchi husika. Mashirika mengine ya kimataifa uwezo wao ni kupiga domo kaya tu.
 
Ndio nikauliza Jumuiya ya kimataifa imeiacha mkono Zanzibar au kuna kitu gani kinaendelea na jee kwa hali hii nini hatma ya CUF ?
 
Jibu ni kwamba CUF wasubiri uchaguzi 2019 hilo ni jibu sahihi kutoka kwa raisi Shein

Bado hujajibu swali. Labda nifafanuwe kidogo. Nini hatma ya CUF ?ikiwa ZEC ni ile ile na mazingira ni yale yale ? Halafu jee jumuiya ya kimataifa imeiacha mkono Zanzibar kwa kutofanya jitihada za kutatua mgogoro ?

Majibu ya dr shein ni kuhusu uchaguzi tu kuwa utakuwa 2020.
 
Ndio Mkuu. Kwa hio kama nchi hakuna tatizo lolte la kidiplomasia kwa yaliyotokea 2015 ? tuseme sawa. Ndio kusema jumuiya ya kimataifa imeshindwa na mgogoro wa Zanzibar ? na ipi hatma ya Zanzibar kwa migogoro hii ya chaguzi ?
Zanzibar hamna mgogoro.. amekuambia nani kama upo mgogoro?
 
Tunachokiona kwa upande wa CCM kupitia Dr Shein ni kama kwamba hawana wasi wasi wowote na ndio kwanza wanaendelea na mipango yao, Aidha kwa upande wa jamuhuri ya muungano ndio kwanza unaendelea kumuahidi Kumpa support zaidi Dr Shein . Dr Shein ana confidnce zote na ndio wanajipanga na 2020. Sasa kwa mnasaba wa kilichotokea 2015 na ukimya uliopo unatia shaka zaidi kwa CUF, Kwanza wanachama wao wengi wamekatas tamaa, lakini lengine hivi jumuiya ya kimataifa ina mchango gani haswa ? maana ukiwauliza wana CUf ni kama kwamba wao wamegogna mwamba na kile wanachokiita vitimbi vya CCM na serikali zake na kwamba hawana ubavu wa kupambana na Dola, ndio nikauliza hivyo.
 
Zanzibar hamna mgogoro.. amekuambia nani kama upo mgogoro?

Pengine wewe huoni kuwa kule kuna mgogoro. Hujiulizi jitihada zote za kimataifa kufanikisha miafaka hadi 2009 kufikiwa uwepo wa GNU kikatiba kwamba hakuna mgogoro ? Mbona Tanzania Bara hakuna mambo hayo hadi leo ?
 
Ukiangali kwa jicho la karibu utagundua ni kweli Zanzibar utengemano wa kijamii na kisiasa umepotea kwa asilimia kubwa. Kwa sasa Zanzibar ni kikundi kidogo tu cha watu ndio wanaiendesha nchi, sheni amebaki tu mtu wa kutoa matamko jukwaani ili aonekane yupo kama raisi. Ipi hatma ya CUF? cuf ni moja kati ya Chama ambacho wanapita katika njia ngumu mnoo, wanapita katika njia yenye mabomu mengi ya kutegwa ardhini, miiba na kila aina ya hatari, wanasonga mbele kwa mwendo wa kobe lakini kwa uhakika sana (slow but sure). Na yote hii ni kwa sababu wako na chief strategist mzuri mnoo. CUF wanajua kuwa CCM itaendelea kuharibu uchaguzi kwa kutumia vikosi vya ulinzi vya zanzibar na Tanganyika lakini ipo siku wataifikia ikulu. Hatma ya CUF ni kufikia malengo yao hata kama itachukua mda gani, na kama unaangalia wana progress vizuri mnoo ndani na nje ya nchi. Salama ya CCM ni kuiripua kwa mabomu Pemba yato ipotee kabisa katika uso wa dunia kwa sababu katika chaguzi zote za Zanzibar aneshinda Pemba ndio mshindi na hapo ndipo moyo wa cuf na jeuri ya kutokukataa tamaa kwa CUF inapoanzia. CUF hawapambani na Shein wa Zanzibar, CUF wanapambana na Tanganyika pamoja na vyombo vyake vyote vya ulinzi na usalama tena vita kali na isiyoisha, inahitaji kichwa kilichotulia sana na kisicho na tamaa na madaraka ama fedha. Jee Jumuiya ya Kimataifa imeitupa mkono Zanzibar? Hata kidogo. CUF wamechagua njia za kidiplomasia katika kupigania wanachokiamini na njia hii siku zote inachukua muda mrefu katika kuwashawishi mataifa kuwa dhulma imefanyika na kuhitaji haki itendeke. Na ndio maana wamekuwa wakizunguka kila pembe ya dunia kuhakikisha lengo lao linatimia, sio rahisi. Kitu ambacho kinaviumiza vyama vya upinzani ni mapandikizi yaliopandikizwa kwa ustadi mkubwa na CCM pamoja na kitengo. Rejea kesi za Mapalala, Hamad Rashid, aliekuwa kiongozi wa kwanza mwanamke bungeni Bi Fatma Maghimbi, Salum Msabah, Khalifa ali, Lipumba na wengineo. Na ndio maana strategies za kuipata haki Zanzibar zinakwenda kimya kimya na kwa mwendo wa uhakika kwa sababu ya mapandikizi haya. let me remand you yanayoitokea Zanzibar baadae yanahamia Tanganyika, nauona mkinzano wa kisiasa na baadae kuundwa kwa serikali ya kitaifa tanganyika kama ilivyotokea zanzibar, lakini kama ilivyotokea Zanzibar nayo haitadumu. CCM tunaipenda lakini itafika muda lazima na wao waondoke hakuna kinachodumu kwenye uso wa dunia. Thats a bitter truth.
 
Hahahahaa umeshasema 2009, hiyo GNU mlitaka kujipa umaarufu tu. hivi sasa si unaona mambo yanaenda kama kawaida nyinyi endeleeni kuweweseka kwenye social media. lakini nakupongezeni bila ya hizo picha mnazopiga na wazungu zinawapa furaha misukule yenu...
 
unazungumza dunia ipi wewe ? Point yako ni nini ?
 
Ukiangali kwa jicho la karibu utagundua ni kweli Zanzibar utengemano wa kijamii na kisiasa umepotea kwa asilimia kubwa. Kwa sasa Zanzibar ni kikundi kidogo tu cha watu ndio wanaiendesha nchi, sheni amebaki tu mtu wa kutoa matamko jukwaani ili aonekane yupo kama raisi. Ipi hatma ya CUF? cuf ni moja kati ya Chama ambacho wanapita katika njia ngumu mnoo, wanapita katika njia yenye mabomu mengi ya kutegwa ardhini, miiba na kila aina ya hatari, wanasonga mbele kwa mwendo wa kobe lakini kwa uhakika sana (slow but sure). Na yote hii ni kwa sababu wako na chief strategist mzuri mnoo. CUF wanajua kuwa CCM itaendelea kuharibu uchaguzi kwa kutumia vikosi vya ulinzi vya zanzibar na Tanganyika lakini ipo siku wataifikia ikulu. Hatma ya CUF ni kufikia malengo yao hata kama itachukua mda gani, na kama unaangalia wana progress vizuri mnoo ndani na nje ya nchi. Salama ya CCM ni kuiripua kwa mabomu Pemba yato ipotee kabisa katika uso wa dunia kwa sababu katika chaguzi zote za Zanzibar aneshinda Pemba ndio mshindi na hapo ndipo moyo wa cuf na jeuri ya kutokukataa tamaa kwa CUF inapoanzia. CUF hawapambani na Shein wa Zanzibar, CUF wanapambana na Tanganyika pamoja na vyombo vyake vyote vya ulinzi na usalama tena vita kali na isiyoisha, inahitaji kichwa kilichotulia sana na kisicho na tamaa na madaraka ama fedha. Jee Jumuiya ya Kimataifa imeitupa mkono Zanzibar? Hata kidogo. CUF wamechagua njia za kidiplomasia katika kupigania wanachokiamini na njia hii siku zote inachukua muda mrefu katika kuwashawishi mataifa kuwa dhulma imefanyika na kuhitaji haki itendeke. Na ndio maana wamekuwa wakizunguka kila pembe ya dunia kuhakikisha lengo lao linatimia, sio rahisi. Kitu ambacho kinaviumiza vyama vya upinzani ni mapandikizi yaliopandikizwa kwa ustadi mkubwa na CCM pamoja na kitengo. Rejea kesi za Mapalala, Hamad Rashid, aliekuwa kiongozi wa kwanza mwanamke bungeni Bi Fatma Maghimbi, Salum Msabah, Khalifa ali, Lipumba na wengineo. Na ndio maana strategies za kuipata haki Zanzibar zinakwenda kimya kimya na kwa mwendo wa uhakika kwa sababu ya mapandikizi haya. let me remand you yanayoitokea Zanzibar baadae yanahamia Tanganyika, nauona mkinzano wa kisiasa na baadae kuundwa kwa serikali ya kitaifa tanganyika kama ilivyotokea zanzibar, lakini kama ilivyotokea Zanzibar nayo haitadumu. CCM tunaipenda lakini itafika muda lazima na wao waondoke hakuna kinachodumu kwenye uso wa dunia. Thats a bitter truth.

Mkuu nimekusoma. Umefafanua vizuri , hata hivyo hebu tujikite kwenye hio hoja ya Hatma ya CUf hasa kuelekea 2020 ikiwa mazingira ya kisiasa yatabaki kama yalivyo. Kwa mfano ushiriki wa CUf kwenye uchaguizi chini ya akina JECHA na mfumo wa serikali ambao wenyewe hawamo kabisa. Kuna serikali ya CCM na wapambe wao vipi kutakuwa na future yoyote.

Haya ni masuali muhimu kwa sasa ingawa hatujui mkakati wa CUF wenyewe, ila hizi juhudi za kimataifa kuna uwezekano kweli wa kuzaa matunda yoyote ?
 
Wadadisi wanajaribu kuhoji upi utakuwa msimamo wa jumuiya ya kimataifa katika hali ya Zanzibar kuelekea uchaguzi wa 2020 ? Hili ni muhimu ikizingatiwa kuwa pamoja na kuwa na GNU Katika uchaguzi wa 2015 na jitihada ya kimataifa kuwa karibu sana na uchaguzi ule bado CCM walitumia mbinu ya kufuta uchaguzi wote baada ya kubaini wameshindwa, Yaani kuanzia sasa fanya ufanyavyo lakini ujuwe mwisho wa siku CCM wanafuta uchaguzi wote wakibaini wameshindwa na kufuata uchaguzi wa maelekezo na mtutu wa bunduki kama ulivyokuwea ule wa Machi, 2016. wanafanya haya wakijuwa Jumuiya za Kimataifa zinafuata Diplomasia na huitisha uchaguzi mwengine ambao dunia haiowajibiki nao tena na hata waangalizi inakuwa wamemaliza muda wao na vibali vyao inakuwa vimeisha. Hivi tuseme hali hii kwa ZANZIBAR ITAKUWEPO HADI LINI ?

Tuseme Dunia imeshindwa mikakati hii ya kudhoofisha HAKI inayofanywa na watawala wa CCM kwa Zamnzibar au kuna nini kimejificha ?
 
Mkuu nimekusoma. Umefafanua vizuri , hata hivyo hebu tujikite kwenye hio hoja ya Hatma ya CUf hasa kuelekea 2020 ikiwa mazingira ya kisiasa yatabaki kama yalivyo. Kwa mfano ushiriki wa CUf kwenye uchaguizi chini ya akina JECHA na mfumo wa serikali ambao wenyewe hawamo kabisa. Kuna serikali ya CCM na wapambe wao vipi kutakuwa na future yoyote.

Haya ni masuali muhimu kwa sasa ingawa hatujui mkakati wa CUF wenyewe, ila hizi juhudi za kimataifa kuna uwezekano kweli wa kuzaa matunda yoyote ?

Kwanza ukiangalia historia ya chama cha cuf mara nyingi utaona ni watu wanaosimamia na wasiotetereka katika misimamo yao. Juhudi unazoziita za kimataifa zipo na hazikuanzia leo ingawa mara hii zimekuwa na kasi ya ajabu na athari kubwa kwa pande zote za muungano kwa sababu aliyoyafanya babu jecha ilikuwa ni ujambazi wa wazi kabisa. Angalia tu kidogo wala sio sana athari yake utaikuta hata Tanganyika kwenyewe. Nikuhakikishie Juhudi hizi za Mataifa zitazaa matunda. Hilo halina shaka kabisa. Diplomasia maamuzi yake huwa yanachelewa sana lakini huwa ni uhakika na jamaa wanaonekana kushinda.
 
Back
Top Bottom