Dr.Dimwa ataka Katiba ya Zanzibar ibadilishwe Ili Dr Mwinyi atawale vipindi viwili vya miaka Saba badala ya mitano

dega

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
3,138
3,042
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr.Dimwa amesema kwamba CHAMA hicho kimeanza mchakato wakipeleka mapendekezo hayo baada wananchi wengi wa Visiwa hivyo kumtaka Dr Mwinyi aongezewe muda badala miaka mitano atawale miaka Saba.

Hii nikutokana na MAFANIKIO makubwa aliyoleta katika Visiwa hivyo Kwa kipindi Cha miaka mitatu aliyokaa Madarakani miongoni mwa MAFANIKIO hayo ni kuvuka sera za CHAMA hicho katika ujenzi wa Madarasa Kwa asilimia mia Moja na hamsini. Ujenzi wa hospital za kisasa Kwa Kila Wilaya ya Visiwa hivyo kizifanyia ukarabati barabara zote kuu na za ndani visiwani humo . Ujenzi wa flaiova

Na hivi karibu anatarajia kuanza ujenzi vituo vya TAXI za bahari kurejesha usafiri wa Treni ZANZIBAR mradi wa mabasi ya kisasa ya abiria yatakayokua yanatumia mfumo wa gesi

Kama haitoshi amejenga viwanja vya kisasa vya michezo ya ndani kuukarabati Uwanja wa Amani KUJENGA Parking ya kisasa katika Mji wa ZANZIBAR

Na mengine mengi
Hivyo Hilo likipita uchaguzi Mkuu wa ZANZIBAR utakua mwaka 2027 na Muhula wa pili atamaliza 2034

ZANZIBAR Yangaraaa
 
Atake Asitake
Umenikumbusha mbunge mmoja mwenye kitambi akisema mwendazake atake asitake ataongezewa muda. Wakati huo hajaongea na mamlaka za Mbinguni ambayo ndio yenye uamuzi wa mwisho.

Huyu waziri anataka kumjengea Dr maadui wasio wa lazima.
 
Huyu Dr. Dmbwa Ni Dokta wa mifugo, hospitali au wa PhD?
Kama Ni wa PhD...........
 
Umenikumbusha mbunge mmoja mwenye kitambi akisema mwendazake atake asitake ataongezewa muda. Wakati huo hajaongea na mamlaka za Mbinguni ambayo ndio yenye uamuzi wa mwisho.

Huyu waziri anataka kumjengea Dr maadui wasio wa lazima.
Ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM ZANZIBAR
si Waziri
 
Huyu Jamaa Naona Amevimbiwa,Akajisahauu.Ajikumbushe yaliyomkuta Komandoo Dr.Salmin Amour.Alitolewa Nduki huko Dodoma,Mpaka Leo alinyamazishwa mazimaa.
 
Back
Top Bottom