Miaka mitatu ya ndoa, kipimo cha ndoa kuendelea au kuvunjika…!

Miaka mitatu ya ndoa, kipimo cha ndoa kuendelea au kuvunjika…!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443
black-couple-wedding.jpg

Kuna msemo katika Kiswahili kwamba, kipya ni kinyemi. Msemo huu una maana kwamba, kitu kikiwa kipya huvutia sana na wakati mwingine inakuwa kama vile tunaamini kwamba, hatutaweza kamwe kupunguza hisia zetu dhidi ya kitu hicho. Lakini kadiri siku zinavyoenda, mazoea hutufikisha mahali ambapo hatuwezi tena kuendelea na kiwango kilekile cha kupenda.

Tunapooana, kwa sehemu kubwa ni kwa sababu tunapendana, yaani tumevutana. Katika hatua za awali, tunatokea kuoneshana upendo wa dhati sana. Mara nyingi hi inatokana na haja yetu kuwaonesha wenzetu kwamba, sisi ni watu wa upendo, sisi ni waadilifu na wema. Tunachotafuta ni kukubaliwa nao kwa sababu, wakati huo hamu yetu kwao ni kubwa.

black-african-american-couple-dating.jpg

Kadiri tunavyokaa pamoja, ile hamu yetu kwao inapungua. Ni vigumu kukuta watu ambao wanaweza kudai kwamba, wameishi kwa muda mrefu na hamu ya kila mmoja kwa mwenzake iko palepale au imeongezeka. Kuna tofauti tu ya viwango vya kushuka kwa hamu, lakini huwa inashuka.

Lakini huku kushuka kwa hisia hakuna maana ya kushuka kwa upendo, hapana. Kushuka kwa hisia kuna maana ya akili na baadaye hisia, kujenga mazoea kiasi cha kumchukulia mwingine kwamba ni wa kawaida, pamoja na kumpenda kuliopo.

resolution4_newyear.jpg

Kuna wakati wapenzi hulalamika kwamba, mwenzake alikuwa akipenda kukaa naye kwa muda mrefu, siku hizi hakai kwa muda mrefu tena. Kuna kulalamika kwingi hususan kwa wanawake kwamba, mwenzake haonyeshi ukaribu kama zamani na mengine ya aina hiyo, ingawa bado anaweza kukiri kwamba, anajua anapendwa na huyo mwenzake.

Wataalamu wanadai kwamba, ndoa inapofikia miaka mitatu, mara nyingi ndipo ambapo kama ni kuachana watu huachana au kama ni vurugu, zinakuwa zimefikia mahali pazuri hasa! Katika kipindi cha ile miaka mitatu ya kwanza, ndipo ambapo watu wamefahamiana vema na kama ndoa yao itakuwa ni ndoa ya vurugu, kufikia muda huo inakuwa imeshafahamika.
Black-couple-upset-scaled.jpg

Ndoa nyingi za vurugu zinakuwa zimefahamika kwamba, ni za vurugu kwa kiwango gani kufikia miaka mitatu. Inaelezwa kwamba, katika mwaka wa tatu, mtu anaweza kabisa kutabiri kama ndoa itakuwa ya amani au vita na kama ni ya vita ni kwa kiasi gani. Kama ni ya vurugu kubwa, hata hivyo, mara nyingi haivuki miaka mitatu.

Kama ndoa imeweza kuvuka miaka mitatu, kwa kawaida kipimo kingine ni miaka mitano. Kwenye mwaka wa tano wa ndoa kuna kuachana na kuapizana kwingi pia. Ukichunguza kwa makini, utagundua kwamba wanandoa wengi hufurahishana na kuachana au kuapizana zaidi mwaka wa tatu na wa tano, tangu ndoa yao.

Hapa kwenye mwaka wa tano, ndipo ambapo wanandoa hujiuliza kama walifanya uamuzi sahihi, ndipo ambapo hutaka kujua kama waendelee na ndoa ngumu kama hiyo au hapana hujihoji kuhusu udhaifu wao (wale wenye hekima). Hapa unaweza kukuta mtu anabadilika tu na kuwa ama mkorofi sana au mwadilifu sana kwa ndoa yake.

i-always-wanted-to-ask-ep4-600x337.jpg

Inaelezwa kwamba, baada ya hapo, yaani ukiona watu wamevuka mwaka wa tano salama, kimbuka kinaweza kutokea kwenye mwaka wa tisa. Kwenye mwaka wa saba yale ambayo yalikuwa ni siri ya wanandoa yanaweza kusemwa nje. Inawezekana mume alikuwa ni mzinzi mke akawa anaficha, mke hajui kutunza familia, mume akaficha, yote hayo yanaweza kusemwa hadharani au kwa watu wengine inapofikia mwaka wa tisa.

Kama wanandoa wakivuka salama au wakivuka pamoja na misukosuko yao kwenye mwaka wa tisa, hatua ya mwisho ni mwaka wa 13 wa ndoa. Hapa ndipo ambapo wanandoa wengi wanaamua kwamba, ngoja maisha yaende kama yalivyo au tufikie ukomo. Hebu jaribu kuvuta kumbukumbu na uone kama hakuna wanandoa wengi ambao unawajua, waliovunja ndoa zao kwenye mwaka wa 13! Kama sio mwaka wa 13 palepale inaweza kuwa mwaka wa 12 au wa 14 wa ndoa yao. Lakini kipimo mara nyingi ni mwaka wa 13.

LHHATL-1338403796.jpg

Ukiona ndoa imevuka hapo, watu wakiwa pamoja hata kama kuna vurugu za namna gani za kindoa, huenda wataishi hivyohivyo hadi kifo kiwatengenishe au mmoja amdhuru mwingine…….

Copy to: Nivea, Lisa, King'asti, AshaDii, MwanajamiiOne, afrodenzi, Kongosho, BADILI TABIA, Paloma, mwaJ, Swts, Madame B, MadameX, Mamndenyi, Preta, marejesho, snowhite, Angel Msoffe, sweetlady, FirstLady1, FirstLady, Remmy, Zion Daughter, Kipipi, Roulette, Smile, Asnam, Binti.com, lara 1, Mrembo by Nature, Raiza, cacico, gfsonwin, Asprin, Kiranga, Nyani Ngabu, Mwita Maranya, Don Mangi, Mungi, Erickb52, Mr Rocky, jouneGwalu, SnowBall, HorsePower, Mzee mwenzangu Babu DC Dark City, Jeska, Lusile, Thomas Odera, Arushaone, Bujibuji, Blaine
 
copy :kalou
hapa kuna mambo mawili ya kuyatazama kwenye jamii tuliyonayo sasa
1. Ndoa kuvunjika na wanandoa kutengana
2.Ndoa kuvunjika ila wanandoa wanaendelea kuishi nyumba moja
asilimia kubwa ya ndoa za siku hizi huwa zinavunjika ila wanandoa wanaishi nyumba 1,yaani utakuta mtu anakuambia kuwa ameachana na mme/mke wake,yupo na mtu mwingine na mwenza wake pia anajua ila bado wanaishi nyumba moja,
hebu Mtambuzi dadavua kwa upande huu.
 
nashindwa kusoma nina mambo mengi kichwani kwa leo ntasoma bdae
 
NAKUBALIANA NA WEWE KABISA NIMEYAONA MENGI KWENYE MIAKA 9 YA NDOA YANGI ILA KWA SISI KUAMUA KUWA ACHA MAMBOYAENDE KAMA YALIVYO NAONA IMEKUJA KABLA YA MWAKA WA 13.

Hizi ndoa za siku hizi nazo hazitabiriki yaani mtu anawezaingia kwenye ndoa keshamchoka mwenzie hata mwaka wa tatu hazifiki.

Nimemwona dada mmoja alikuwa anaanda harusi yao huku nje anasema hili li mwanaume hili mi nitakuja tu kuachana nalo nikamuuliza kwanini unaolewa akasema ati anaolewa kutoa Nuksi huuu nilishanagaa sana na kweli baada ya ndoa mwaka haukwisha kila mtu yuko kwake.

Ndoa nyingi za siku hizi zinaendana na hali ya uchumi hivyo matatizo ya kiuchumi unayoyasikia huko bara ulaya jua ndio myumbo wa ndoa huku Afrika na duniani kwa ujumla watu wamekuwa na tamaa za hali ya juu siku hizi pia kuachwa kwa mwanamke nayeye kuweza kuendesha maisha yake kumeonekana kama sifa flani hivo na zaidi wameanzisha mpaka vyama vya wanawake walioachwa na wamekuwa wakiwashawishi wanawake waliokwenye ndoa kutoka hii ni hatari wakati enzi za wazazi wetu kuachwa kwa mwanamke ilikuwa ni aibu ya ukoo na kabila kwa ujumla watu walijitahidi kuzilinda ndoa zao ili wasiletee familia, ukoo, kabila na taifa aibu. ilisemekana usioe familia ile au ukoo ule au kabila lile kwakuwa tu walikuwa na sifa ya kutokukaa kwenye ndoa zao siku hizi hakuna cha familia, ukoo wala kabila mambo yamekwenda mrama.
 
Hili sio kwa ndoa tu, ni relationship zote kati ya binadam nadhani... Asante sana kwa uzi huu.
 
copy :kalou
hapa kuna mambo mawili ya kuyatazama kwenye jamii tuliyonayo sasa
1. Ndoa kuvunjika na wanandoa kutengana
2.Ndoa kuvunjika ila wanandoa wanaendelea kuishi nyumba moja
asilimia kubwa ya ndoa za siku hizi huwa zinavunjika ila wanandoa wanaishi nyumba 1,yaani utakuta mtu anakuambia kuwa ameachana na mme/mke wake,yupo na mtu mwingine na mwenza wake pia anajua ila bado wanaishi nyumba moja,
hebu Mtambuzi dadavua kwa upande huu.
kalou nakubaliana na wewe kuhusu watu kutengana, lakini hilo la kutengana na kuendelea kuishi nyumba moja, lipo kwa kiwango kidogo sana. Mara nyingi inatokea mwanamke kuondoka na kwenda kuanza maisha au mwanaume kuitelekeza familia na kwenda kuanza maisha upya hasa kama ndoa ina watoto (Hii ipo sana).

Wanaume kwa asilimia kubwa wameonekana kushindwa kuhimili kukaa kwenye ndoa zenye vurugu na kukimbia kwa sababu hawana cha kupoteza wakati wanawake ni waoga kuanza maisha wakiwa peke yao kutokana na kuwa tegemezi. Lakini pia swala la wanawake kuogopa kunangwa na jamii kunawafanya wavumilie ndoa ngumu hata kama zinatishia maisha yao.

Labda pia ule utamaduni wa kuwatumia wataalamu wa ushauri kwa wanandoa haupo sana ukilinganisha na wenzetu. Mara nyingi wanandoa wanatumia taasisi za kidini na vikao vya familia kutatua migogoro ya ndoa ambapo navyo vimeonekana kushindwa. Na hii imetokana na mkengeuko mkubwa katika swala zima la kuchagua wenza. Kwani watu wamekuwa waongo kupindukia linapokuja swala la kuchagua mwenza.

Tumefika mahali ambapo watu wanaishai maisha ya bandia na si halisi, wanawake kwa wanaume wamekuwa wakidanganyana sana pale wanapoanzisha mahusiano. Wanawake kwa upande wao wamekuwa na ndoto za Alinacha jambo ambalo limewafanya wanaume kuwa waongo kupindukia. Inaonekana kama vile ni lazima mwanamke adanganywe ndipo aingie kwenye uhusiano kwa sababu mwanaume kumweleza mwanamke ukweli kuhusu hali yake ya kipato hasa kama si cha uhakika ni sawa na kumkimbiza huyo mwanamke na ndio maana hivi sasa wanadanganywa.

Ni pale tu wanawake watakakuwa na utambuzi na kubadili mitazamo yao na kuwa wao ndipo ndoa zitakapokuwa salama.
 
Last edited by a moderator:
NAKUBALIANA NA WEWE KABISA NIMEYAONA MENGI KWENYE MIAKA 9 YA NDOA YANGI ILA KWA SISI KUAMUA KUWA ACHA MAMBOYAENDE KAMA YALIVYO NAONA IMEKUJA KABLA YA MWAKA WA 13.

Hizi ndoa za siku hizi nazo hazitabiriki yaani mtu anawezaingia kwenye ndoa keshamchoka mwenzie hata mwaka wa tatu hazifiki.

Nimemwona dada mmoja alikuwa anaanda harusi yao huku nje anasema hili li mwanaume hili mi nitakuja tu kuachana nalo nikamuuliza kwanini unaolewa akasema ati anaolewa kutoa Nuksi huuu nilishanagaa sana na kweli baada ya ndoa mwaka haukwisha kila mtu yuko kwake.

Ndoa nyingi za siku hizi zinaendana na hali ya uchumi hivyo matatizo ya kiuchumi unayoyasikia huko bara ulaya jua ndio myumbo wa ndoa huku Afrika na duniani kwa ujumla watu wamekuwa na tamaa za hali ya juu siku hizi pia kuachwa kwa mwanamke nayeye kuweza kuendesha maisha yake kumeonekana kama sifa flani hivo na zaidi wameanzisha mpaka vyama vya wanawake walioachwa na wamekuwa wakiwashawishi wanawake waliokwenye ndoa kutoka hii ni hatari wakati enzi za wazazi wetu kuachwa kwa mwanamke ilikuwa ni aibu ya ukoo na kabila kwa ujumla watu walijitahidi kuzilinda ndoa zao ili wasiletee familia, ukoo, kabila na taifa aibu. ilisemekana usioe familia ile au ukoo ule au kabila lile kwakuwa tu walikuwa na sifa ya kutokukaa kwenye ndoa zao siku hizi hakuna cha familia, ukoo wala kabila mambo yamekwenda mrama.
kitalolo naomba nikupe LIKE.
 
Last edited by a moderator:
Mtambuzi
ina maana basi hakuna muda ndoa inakuwa salama,manake
2nd year kavuka akiwa haamini kama ypo ndani ya mto,
3rd year kavuka hivo hivo,
4th year ah ngoja nivuke tu,
6th an 7th msinione nimevuka nimebeba kibao,
8th,9th na 10th lolote liwe naweza kuvuka mwenyewe
10th,11th nafkir nimemudu kuvuka mwenyewe
12th year na 13 hatuvuki wete endelea mwenyewe!

is this how best we can talk about a marriage?
haijalishi ndoa ni changamoto kiasi gani lakini bado si kiasi hiki!
 
snowhite, hivi umesoma kwa makini kweli...?
Wataalamu wanadai kwamba, ndoa inapofikia miaka mitatu, mara nyingi ndipo ambapo kama ni kuachana watu huachana au kama ni vurugu, zinakuwa zimefikia mahali pazuri hasa! Katika kipindi cha ile miaka mitatu ya kwanza, ndipo ambapo watu wamefahamiana vema na kama ndoa yao itakuwa ni ndoa ya vurugu, kufikia muda huo inakuwa imeshafahamika

Ndoa nyingi za vurugu zinakuwa zimefahamika kwamba, ni za vurugu kwa kiwango gani kufikia miaka mitatu. Inaelezwa kwamba, katika mwaka wa tatu, mtu anaweza kabisa kutabiri kama ndoa itakuwa ya amani au vita na kama ni ya vita ni kwa kiasi gani. Kama ni ya vurugu kubwa, hata hivyo, mara nyingi haivuki miaka mitatu.

Naomba usome tena na nimejaribu kukuonesha kile nilichomaanisha hapo juu....

Shemeji kama uliamka nazo basi kapate supu uondoe mning'inio...
 
Back
Top Bottom