Miaka hiyo wakati Mr II alipokuwa II Proud Hii Ngoma ilikuwa ya Kimapinduzi hasa.

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,651
14,314
"...ni wapi tuna kwenda?'
Ni wapi tunakwenda?
Shule namaliza nabaki najiuliza nitafanya kazi gani?
kwenye kila kampuni kazi hazipatikani
heri kwa watoto wa wakuu
wanaopata kazi kupitia wazazi
hii siyo sawa, kwao hii ni sawa
Mungu awape nini labda gunia la chawa
na sasa nareport natafuta passport nasafiri kikafili
popote nitafika hata south afrika
nyumban nimechoka, nazidi nyanyasika
polisi wanisaka, naonekana kibaka
sababu sina kazi au sababu ya mavazi
ni wapi tunakwenda?

.....Shauritanga tukabaki na Matanga
waliua wasichana vijana wenzetu
walikosa nini maskini
mapema kama vile kuwapeleka kaburini
ni wapi tunakwenda....

...mambo yameharibika namkumbuka sokoine
hii 95 nani mwingine afanane?
alipinga rushwa na ubadhilifu

Miaka hiyo wengi humu walikuwa hawajazaliwa au walikuwa bado wanatoa kamasi kwa ngumi. wakikimbizwa jioni wakaoge na wazazi wao wakiwa wamevaa chupi. sisi miaka hiyo tunasikiliza hip pop toka watu kama II Proud kabla hajabadili jina kuwa Mr II Sugu. jamaa alikuwa mwanaharakati mzuri sana.
 
Kama hujui Unako toka
Hujui Unako kwenda
Fikiri kabla ya Kutenda
Fanya unachopenda
Iliandikwa haikusemwa
Fanya Mapema sasa nasema
Vitabu vilisha Chomwa
Sitorudia tena
Kama unajua
We utaona (oooyeeh)x2
 
Kuna ngoma moja ya Mr.2 inaitw Hali Halisi ni ilipigwa marufuku na serikali ngoma ilikuwa ya kmapunduzi kutetea wanyonge
 
Back
Top Bottom