Miaka 60 ya Uhuru: Tanzania tuna laana?

Miaka 60 ya Uhuru: Tanzania tuna laana?

Umeandika vizuri. Turudi kwenye chanzo, chanzo cha yote aya ni chama cha mapinduzi wameshindwa kua na dira kama taifa kwa kipindi cha muda mrefu kila anayeingia anakua anamatakwa yake binafsi.

Dunia iko 2021 ila sisi tunatamani kuishi early 80s.

Hovyo hovyo tuu
Nini kifanyike.Viongozi Tupo taifa sasa hivi tunaadhimisha miaka 60 ya uhuru
 
Nipo Jiji la Dar Jimbo la Ukonga naamka nijiandae kusherekea uhuru Tanesco wamekata umeme, nimejiuliza maswali mengi sijapata jibu tatizo ni Ccm au sisi Watanzania?
 
Umeandika vizuri sana.

Pamoja na changamoto nyingi za kisera na kimkakati kama taifa kukwama. Pia, vijana bado tumelala kusubiri serikali utukwamue.

Vijana tunaopambana pia hatujui tunapambania nini maana hatuna malengo yanayozidi mwaka mmoja.

Binafsi kwa sasa pamoja na kuwa mwajiriwa wa serikali ila nimeamua kulima kwa spidi ya hatari. Naamka saa kumi za alfajiri kila siku kabla ya kwenda kazini saa mbili.

Nimejiwekea malengo ya miaka mitano hadi 2026 niwe mtu wa tofauti kiuchumi. Kwa sasa nimeanza na malengo kuvuna gunia 10 za maharage kwa msimu. Baadaye nitaongeza malengo.

Umasikini wetu kwa kiasi kikubwa unaanzia kichwani.
You got it to my brain
JamiiForums-638410352.gif
 
Umeandika vizuri sana.

Pamoja na changamoto nyingi za kisera na kimkakati kama taifa kukwama. Pia, vijana bado tumelala kusubiri serikali utukwamue.

Vijana tunaopambana pia hatujui tunapambania nini maana hatuna malengo yanayozidi mwaka mmoja.

Binafsi kwa sasa pamoja na kuwa mwajiriwa wa serikali ila nimeamua kulima kwa spidi ya hatari. Naamka saa kumi za alfajiri kila siku kabla ya kwenda kazini saa mbili.

Nimejiwekea malengo ya miaka mitano hadi 2026 niwe mtu wa tofauti kiuchumi. Kwa sasa nimeanza na malengo kuvuna gunia 10 za maharage kwa msimu. Baadaye nitaongeza malengo.

Umasikini wetu kwa kiasi kikubwa unaanzia kichwani.
Umasikini wetu Kwa kiasi kikubwa unaanzia kichwani
 
Mkuu vipi kuhusu Singapore,pia wao Walikuwa km Sisi enzi hizo.Mimi naona matatizo ya mtanzania ni zaidi ya ulivyotafsiri.Umejibu kiwepesi sn
Kwani vipi kuhusu jirani zako ambao walisoma na kucheza na babu zako mnalingana maendeleo?
 
Nini kifanyike.Viongozi Tupo taifa sasa hivi tunaadhimisha miaka 60 ya uhuru

Tuwe na utawala bora wenye uwazi, katiba ni muhimu hapa. Kila mtanzania akumbuke wajibu wake kufanya kazi, kulipa kodi ( uwazi utafanya kila mtu atamani kulip)

Kama taifa tuvipe kipaumbele sekta muhimu kwanza na sekta shikizi kwa uchache. Tuwekeze kwenye elimu, afya, huduma za kijamii mfano maji, naamini miaka 5 inatosha kufikia malengo
 
Halafu umeamka asubuhi na gunia zako 10 unataka kuuza unaambiwa kilo moja ni 600, wewe gharama ya kilo moja kuizalisha umetumia 1200 sababu ya mbolea kuwa juu,viuatilifu juu,ushuru wa mazao,mbegu kuwa juu!
Utakuwa bado umelala wewe au imelala serikali!
Mnunuzi, mlaji na muuzaji wote watalalamika.

Mkulima = bei ya mazao imeporomoka.

Mlaji = Serikali imeshindwa kudhibiti mfumko wa bei!

Hapa tatizo ni nini, na nani ana haki ya kulalamika?
 
Halafu umeamka asubuhi na gunia zako 10 unataka kuuza unaambiwa kilo moja ni 600, wewe gharama ya kilo moja kuizalisha umetumia 1200 sababu ya mbolea kuwa juu,viuatilifu juu,ushuru wa mazao,mbegu kuwa juu!
Utakuwa bado umelala wewe au imelala serikali!
Hapo ndipo kwenye tatizo la msingi.Mtu unaweza kuamka kwenda kupambana lkn serikali imelala sn ktk kumwinua huyu raia

Kuna siku nilikuwa Morogoro Kwa mshikaji,tukaenda sokoni kununua zaga tupike msosi.Asee bei ya nyanya ilikuwa chini sn,kisado kidogo cha Lita kumi tulinunua buku 2..sasa huyu mkulima anapataje faida ktk Hali km hii
 
Tatizo kundi kubwa la vijana linaendelea kuwalinda na kuwakumbatia viongozi wapuuzi katika nchi hii. Ndyo maana inakuwa ngumu vijana kusimama na kuexplore fursa mbalimbali. Mfano kuanzia mwaka 2015 - 2021 ilikuwa imeshakuwa kwamba ili kijana upate fursa serikalini lazima uwe mfuasi wa chama tawala. Ili mfanyabiashara ufanye biashara kwa amani lazima uwe mfuasi wa chama tawala plus upuuzi mwingi tu.


Resources nyingi tulizonazo zinawafaidisha wanasiasa kuliko wananchi [emoji119]. Tunalalamika sasa hivi na kuonesha tuko serious kwa kutambua tulikosea kuchagua viongozi lakini ikifika wakati wa uchaguzi watu wakipewa elfu 5,10, 50 wanasimama kidete ili waliowahonga wapate nafasi za uongozi halafu baada ya hapo ndyo maumivu haya tunayoyapata. Kila kitu bei juu na hakuna kiongozi imara wa kututetea
Kwa taarifa yako viongozi hawatakuja jubadilika nchi hii.

Ondoa hizo fantasy za kupata malaika wa kuja kutawala nchi hii.

Hata kama viatakuja kubadioika vyama, watu watabaki kuwa wale wale.

Jaribu kufikiri kwa kutumia akili.

Uhuru aligombea kupitia KANU hakupata, leo Uhuru huyo huyo wa KANU ndie mtawala kupitia Jubilee.

Hata hapa kwetu, Lowassa yule yule wa CCM ndiye huyo huyo alikuwa wa CHADEMA.

Narudia tena TUMIA AKILI.
 
Leo ni siku ya Uhuru, nimefungulia redio nikatune Wasafi FM nikasikia wanapiga nyimbo ya miaka ya 60-80. Vijana wa sasa huziita zilipendwa. Sijui jina la nyimbo wala aliyeimba simjui lakini nikawa nasikiliza Kwa makini maana ujumbe wa nyimbo ulinivutia sana.

Mwimbaji wa hii nyimbo alikuwa analalamika juu ya ugumu wa maisha Kwa wakati huo. Anasema alioa wanawake wawili lakini inabidi amuache mmoja Kwa sababu maisha yamegekuwa magumu Sana.

Anataja ulanguzi wa bidhaa, akiitaka na sukari jinsi ulivyosababisha ugumu wa maisha wakati huo

Baada ya hii nyimbo kuisha nikawa nawaza tunasherekea sikukuu ya Uhuru wa Tanzania bara,ni Uhuru wa nini, mbona matatizo yaleyale ambayo huyu muimbaji wa enzi hizo aliyoyaimba bado tunayo tena makubwa sana.

Mkulima bado anatumia jembe la mkono,na inatajwa afrika ndiyo bara linaloongoza kwa kilimo duni kuliko bara lolote, Tanzania ikiwemo.

Tangu nakua tunaambiwa Tanzania ni nchi ya pili Kwa vivutio duniani ikitanguliwa na Brazil lakini tunapokea watalii chini ya milioni mbili Kwa mwaka

Leo watanzania wanakamuliwa na Kodi za kila Aina.Juzi Tu hapo wametuongezea mzigo wa Kodi isiyo rasmi, wameibatiza jina tozo.Niliwahi kumsikia mtu mmoja akisema endapo Tanzania ingepata asilimia 10 Tu ya watalii wanaotembelea Paris Ufaransa ambao hupokea watalii zaidi ya milioni 80 Kwa mwaka basi tungepiga hatua kubwa Sana Kama taifa,na masuala ya tozo tusingeyazungumzia

Tuna madini ya kila Aina lakini yamekuwa Kama laana kwwtu.Kila siku yunasikia Stori za kutoroshwa.Juzi tukajenga ukuta mererani lakini tunaambiwa Kasi ya utoroshaji imekuwa kubwa kuliko awali

Kwenye michezo bado tunaendelea kupeperusha bendera ya 'kichwa cha mwendawazimu'
Miaka 60 ya Uhuru viwanja Bora vyenye hadhi ya FIFA ni viwili tena vyote vipo Dar
Tunatajwa kuwa na ligi Bora ya 8 Africa lakini serikali haifanyi maboresho yoyote kwenye viwanja vya mikoani, viwanja vya CCM ndiyo vibovu kuliko. Azam TV anashindwa kufunga camera za kutosha Kwa sababu viwanja vingi vya mikoani havisupport, hadi wakati mwingine analazimika kufunga majukwa Kwa ajili ya studio ya kurushia matangazo Kwa gharama yake binafsi.

Serikali inalalamika ajira hakuna lakini ingeboresha sekta ya michezo vijana wengi wangejiajiri huko Ila imelala fofofo.Ila wakina mwakinyo wakishinda Kwa juhudi zao binafsi ndiyo wanawakumbuka Kwa kuwaita ikulu na bungeni kuwapongeza

Nakumbuka wiki kadhaa zilizopita Rais wa Uganda alikuja kufanya ziara Tanzania.Kwenye hotuba yake Rais wa Tanzania Mama Samia aliongelea swala la sukari,akamwambia Rais wa Uganda wafanyabkashara wa Uganda waingize sukari nchini na kuiita kauli ya waziri wake ya kuzuia sukari kutoka nje ni 'nonsense'

Niliposikia hii nyimbo ya kale hasa hiki kipande cha ulanguzi wa sukari enzi hizo niikaishia kucheka Tu maana miaka mingi baadae bado tatizo la sukari aliloliimba enzi hizo liko pale pale.Tumekwama mahali Kama taifa

Miaka ya 2013/2014 kulikuwa na makala kwenye gazeti la Tazama yenye kichwa cha habari POVERTY IN THE MIDST OF PLENTIFUL (UMASIKINI KATIKATI YA UTAJIRI)

Tumejaaliwa na mwenyezi MUNGU kila Aina ya utajiri lakini tuna umasikini wa kutupwa.Je,Tanzania tumelaaniwa?

Happy independence Day
Niliposikia hii nyimbo ya kale hasa hiki kipande cha ulanguzi wa sukari enzi hizo niikaishia kucheka Tu maana miaka mingi baadae bado tatizo la sukari aliloliimba enzi hizo liko pale pale.Tumekwama mahali Kama taifa[emoji23]
 

Kafara la kukimbiza moto linavyoligharimu Taifa
 
Acha mawazo ya visingizio.
Sawa, endelea kuwa na vivutio vya utalii huku USA anawapa travel alert ya Corona dhidi ya watu wake kutembelea Tanzania, huku akiwaruhusu waende paris kwamba ni salama, na chanjo tumenunua za Trillion 2, sasa sijui hao watalii million 80 utawatoa wapi
 
Ni upumbavu kusherekea UHURU hali hatupo huru.
Wanaofaidika na matunda ya UHURU awazidi 10% bora wakoloni wangeendelea tungekuwa mbali sana.
Nchi za Scandinavian norway, sweden, denmark, China, Malasyia, vietnam tulikuwa nao uchumi SAwa,dola moja ilikuwa SAwa na shilingi 60 ya TANZANIA.Ni aibu sana kupewa misaada na vinchi vidogo SAwa na mkoa kama denmark na sweden sababu wao walipata viongozi wanaofikiri huku raslimali tele zimejaa.
 
Sawa, endelea kuwa na vivutio vya utalii huku USA anawapa travel alert ya Corona dhidi ya watu wake kutembelea Tanzania, huku akiwaruhusu waende paris kwamba ni salama, na chanjo tumenunua za Trillion 2, sasa sijui hao watalii million 80 utawatoa wapi
Tunapaswa tupate akili za kujitegemea wenyewe kwanza ndio tufikirie nje.Ukiona tunafikiria nje kwanza badala ya ndani jua uko ndani hakuna chochote cha maana tulichofanya kwa ajili yetu wenyewe ndio maana tunakimbilia nje kwa wengine ambao walishafanya kwa ajili yao kwanza badae ndo wakatoka nje.
 
Tunapaswa tupate akili za kujitegemea wenyewe kwanza ndio tufikirie nje.Ukiona tunafikiria nje kwanza badala ya ndani jua uko ndani hakuna chochote cha maana tulichofanya kwa ajili yetu wenyewe ndio maana tunakimbilia nje kwa wengine ambao walishafanya kwa ajili yao kwanza badae ndo wakatoka nje.
Yeye kaongelea utalii, watalii wa nje ndio wanaongeza pato la ndani, sio watalii wa ndani
 
Acha kazi ujiajiri. Ajira ni utumwa
Hiyo ni kweli kabisa mkuu.....ila nature ya kazi yangu na mazingira nilipo kwa sasa vinanisaidia kupata mbolea bure kabisa na ardhi ina rutuba ya kutosha. Nguvu kazi ni mimi mwenyewe.

Kuhusu bei hiyo changamoto ya karibia kila bidhaa na nafaka zinazozalishwa au kuingizwa hapa nchini.

Vijana tupambane maana inazidi kuwa tete.
 
Back
Top Bottom