PseudoDar186
Senior Member
- Mar 18, 2017
- 104
- 241
Hii chupa ya dripu ina nusu lita ya kimiminika aina ya ‘maji’. Lebo hapo inasema "0.9% w/v" Sodium Chloride (chumvi). Kwa kifupi, maana yake ni kwamba 99.1% ya hii chupa ni maji. Kwenye hii dripu ya 500 ml, kuna gram 4.5 ya chumvi. Kilichobaki 495ml ni maji.
Haya maji yamekuja kutoka India kwa kupitia meli au ndege. Hebu tufikirie, makontena ya maji 99% yanavuka bahari au anga kufika Tanzania kutoka India kisa nchi yetu imeshindwa kukidhi mahitaji yake.
Baada ya miaka 64 ya uhuru, bado tunaagiza maji kutoka nje! Hatuna vikwazo vya kiuchumi kama Iran. Nchi inaliza hii.