Miaka 60 ya Uhuru: Tanzania tuna laana?

Miaka 60 ya Uhuru: Tanzania tuna laana?

Satoh Hirosh

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2021
Posts
7,235
Reaction score
29,524
Leo ni siku ya Uhuru, nimefungulia redio nikatune Wasafi FM nikasikia wanapiga nyimbo ya miaka ya 60-80. Vijana wa sasa huziita zilipendwa. Sijui jina la nyimbo wala aliyeimba simjui lakini nikawa nasikiliza Kwa makini maana ujumbe wa nyimbo ulinivutia sana.

Mwimbaji wa hii nyimbo alikuwa analalamika juu ya ugumu wa maisha Kwa wakati huo. Anasema alioa wanawake wawili lakini inabidi amuache mmoja Kwa sababu maisha yamegekuwa magumu Sana.

Anataja ulanguzi wa bidhaa, akiitaka na sukari jinsi ulivyosababisha ugumu wa maisha wakati huo.

Baada ya hii nyimbo kuisha nikawa nawaza tunasherekea sikukuu ya Uhuru wa Tanzania bara,ni Uhuru wa nini, mbona matatizo yaleyale ambayo huyu muimbaji wa enzi hizo aliyoyaimba bado tunayo tena makubwa sana.

Mkulima bado anatumia jembe la mkono,na inatajwa afrika ndiyo bara linaloongoza kwa kilimo duni kuliko bara lolote, Tanzania ikiwemo.

Tangu nakua tunaambiwa Tanzania ni nchi ya pili Kwa vivutio duniani ikitanguliwa na Brazil lakini tunapokea watalii chini ya milioni mbili Kwa mwaka.

Leo watanzania wanakamuliwa na Kodi za kila Aina.Juzi Tu hapo wametuongezea mzigo wa Kodi isiyo rasmi, wameibatiza jina tozo.Niliwahi kumsikia mtu mmoja akisema endapo Tanzania ingepata asilimia 10 Tu ya watalii wanaotembelea Paris Ufaransa ambao hupokea watalii zaidi ya milioni 80 Kwa mwaka basi tungepiga hatua kubwa Sana Kama taifa,na masuala ya tozo tusingeyazungumzia.

Tuna madini ya kila Aina lakini yamekuwa Kama laana kwwtu.Kila siku yunasikia Stori za kutoroshwa.Juzi tukajenga ukuta mererani lakini tunaambiwa Kasi ya utoroshaji imekuwa kubwa kuliko awali.

Kwenye michezo bado tunaendelea kupeperusha bendera ya 'kichwa cha mwendawazimu'
Miaka 60 ya Uhuru viwanja Bora vyenye hadhi ya FIFA ni viwili tena vyote vipo Dar
Tunatajwa kuwa na ligi Bora ya 8 Africa lakini serikali haifanyi maboresho yoyote kwenye viwanja vya mikoani, viwanja vya CCM ndiyo vibovu kuliko. Azam TV anashindwa kufunga camera za kutosha Kwa sababu viwanja vingi vya mikoani havisupport, hadi wakati mwingine analazimika kufunga majukwa Kwa ajili ya studio ya kurushia matangazo Kwa gharama yake binafsi.

Serikali inalalamika ajira hakuna lakini ingeboresha sekta ya michezo vijana wengi wangejiajiri huko Ila imelala fofofo.Ila wakina mwakinyo wakishinda Kwa juhudi zao binafsi ndiyo wanawakumbuka Kwa kuwaita ikulu na bungeni kuwapongeza.

Nakumbuka wiki kadhaa zilizopita Rais wa Uganda alikuja kufanya ziara Tanzania.Kwenye hotuba yake Rais wa Tanzania Mama Samia aliongelea swala la sukari,akamwambia Rais wa Uganda wafanyabkashara wa Uganda waingize sukari nchini na kuiita kauli ya waziri wake ya kuzuia sukari kutoka nje ni 'nonsense'.

Niliposikia hii nyimbo ya kale hasa hiki kipande cha ulanguzi wa sukari enzi hizo niikaishia kucheka Tu maana miaka mingi baadae bado tatizo la sukari aliloliimba enzi hizo liko pale pale.Tumekwama mahali Kama taifa.

Miaka ya 2013/2014 kulikuwa na makala kwenye gazeti la Tazama yenye kichwa cha habari POVERTY IN THE MIDST OF PLENTIFUL (UMASIKINI KATIKATI YA UTAJIRI).

Tumejaaliwa na mwenyezi MUNGU kila Aina ya utajiri lakini tuna umasikini wa kutupwa.Je,Tanzania tumelaaniwa?

Happy independence Day.
 
Umeandika vizuri sana.

Pamoja na changamoto nyingi za kisera na kimkakati kama taifa kukwama. Pia, vijana bado tumelala kusubiri serikali utukwamue.

Vijana tunaopambana pia hatujui tunapambania nini maana hatuna malengo yanayozidi mwaka mmoja.

Binafsi kwa sasa pamoja na kuwa mwajiriwa wa serikali ila nimeamua kulima kwa spidi ya hatari. Naamka saa kumi za alfajiri kila siku kabla ya kwenda kazini saa mbili.

Nimejiwekea malengo ya miaka mitano hadi 2026 niwe mtu wa tofauti kiuchumi. Kwa sasa nimeanza na malengo kuvuna gunia 10 za maharage kwa msimu. Baadaye nitaongeza malengo.

Umasikini wetu kwa kiasi kikubwa unaanzia kichwani.
 
Umeandika vizuri sana.

Pamoja na changamoto nyingi za kisera na kimkakati kama taifa kukwama. Pia, vijana bado tumelala kusubiri serikali utukwamue...
Halafu umeamka asubuhi na gunia zako 10 unataka kuuza unaambiwa kilo moja ni 600, wewe gharama ya kilo moja kuizalisha umetumia 1200 sababu ya mbolea kuwa juu,viuatilifu juu,ushuru wa mazao,mbegu kuwa juu.

Utakuwa bado umelala wewe au imelala serikali!
 
Tatizo kundi kubwa la vijana linaendelea kuwalinda na kuwakumbatia viongozi wapuuzi katika nchi hii. Ndyo maana inakuwa ngumu vijana kusimama na kuexplore fursa mbalimbali. Mfano kuanzia mwaka 2015 - 2021 ilikuwa imeshakuwa kwamba ili kijana upate fursa serikalini lazima uwe mfuasi wa chama tawala. Ili mfanyabiashara ufanye biashara kwa amani lazima uwe mfuasi wa chama tawala plus upuuzi mwingi tu.

Resources nyingi tulizonazo zinawafaidisha wanasiasa kuliko wananchi [emoji119]. Tunalalamika sasa hivi na kuonesha tuko serious kwa kutambua tulikosea kuchagua viongozi lakini ikifika wakati wa uchaguzi watu wakipewa elfu 5,10, 50 wanasimama kidete ili waliowahonga wapate nafasi za uongozi halafu baada ya hapo ndyo maumivu haya tunayoyapata. Kila kitu bei juu na hakuna kiongozi imara wa kututetea
 
Leo ni siku ya Uhuru, nimefungulia redio nikatune Wasafi FM nikasikia wanapiga nyimbo ya miaka ya 60-80. Vijana wa sasa huziita zilipendwa. Sijui jina la nyimbo wala aliyeimba simjui lakini nikawa nasikiliza Kwa makini maana ujumbe wa nyimbo ulinivutia sana...
Hatukulaaniwa, lakini tumenyimwa uwezo wa maarifa, Ikiwa hii ndiyo tafsiri sanifu ya laana basi na iwe hivyo.

Afrika Nzima inafanana, yatupasa tujitambue na tuukubali ukweli.

Hakuna aliye na unafuu, Waafrika huwa tunarohombaya na kukabiana wenyewe kwa wenyewe. Mimi najiuluza, kwa nini serikali isitowe fursa kwa Matajiriwa Tanzania amabo wanaonekana kufanya vizuri katika uwekezaji kama vile Bakhresa,Wapewe jukumu la kuchimba Madini ? au kujishughulisha na viwanda vya sukari?, na wengine wawape jukumu la Kulima mazao ya chakula na biashara?

Huko ulaya na marekani ukisikia wanamazao ya kutosha na kuuz nje ,huwa hayatokani na wakulima uchwara, bali wakulima wakubwa mabepari ndio wanaolinda uchumi wa mataifa yao.

Hata viwanda vya silaha, mashine na bidhaa ni mali za Matajiri. Serikali kazi yake ni kusimamia na kukusanya Kodi tuu.

Masikini hawezi kulima,
Masikini hachimbi madini,
Masikini hawi mjasiria mali.
Bali masikini huajiriwa na kulipwa mshahara.
Hata Biashara , haiwezekani kila mtu afanye biashara, ndio maana nchi hii wamachinga wamekuwa wengi na hawawezi kudhubitiwa ngo.
 
Umeandika vizuri sana.

Pamoja na changamoto nyingi za kisera na kimkakati kama taifa kukwama. Pia, vijana bado tumelala kusubiri serikali utukwamue..
Ni Jambo zuri sana Ila serikali iliaribhlu mfumo WA kilimo nchini na ilishindwa kutengeneza mazingira mazuri Kwa wakulima serikali haipo kutupa pesa wananchi Ila ni mara ngapi umesikia wakulima wakilalama wanakosa masomo ya mazao Yao na waziri anazuia ata mazao kupelekwa nje ya nchi ili watu wajipatie vipato vya jasho Lao tukumbuke mdau WA Kwanza Kwa mazao ya chakula nchini ni serikali Ila haikununua mazao ya wakulima na kufanya bei iporomoke.

Huku nje ya nchi wamezuia kuuza, kilimo ni kizuri Ila nishasema sitakuja kulima labda niwekeze na mtu Ila kutafuta shamba Bora nifuge mara bilioni siyo kuteseka na viongozi wapumbavu wa nchii hii kila siku wanasema kilimo kimeajiri watu wengi kuliko sekta yoyote Ila haijawai kuja na mpango mzuri WA kumkomboa mkulima zaidi ya blabla Tu mdomoni.

Hawa kila mwaka nyanya zinaaribika shambani hawajawai kuja na plan ya vp tufanye vp mkulima afaidike na jasho lake waliona wakulima WA korosho wanafaidi sana wakaenda kuaribu soko Lao watu wakalia na kuumia ata fidia hawajalipwa upumbavu Tu hii nchii mbaazi ilikuwa imefiika kilo 2000 na zaidi Kwa ujinga WA wanasisia wapumbavu mbaazi ikafika Hadi kilo miambili ivi kweli hii nchii si inaviongozi takataka kabisaa alafu mtu mnashangalia Tu hii nchi kuanzia viongozi na wananchi wake ni wapumbavu kabisa
 
Hatuwezi kupiga hatua kubwa yakimaendeleo kwasababu uwezo wetu wakufikiri na kutenda umeshaisha nguvu.Uko serikalini wanaobadilika ni watu na majina yao ila mifumo ya utendaji na mindset zao ni vile vile.kwahiyo kamwe usitegemee jambo jipya kwa akili na mawazo haya haya.
 
Halafu umeamka asubuhi na gunia zako 10 unataka kuuza unaambiwa kilo moja ni 600, wewe gharama ya kilo moja kuizalisha umetumia 1200 sababu ya mbolea kuwa juu,viuatilifu juu,ushuru wa mazao,mbegu kuwa juu!
Utakuwa bado umelala wewe au imelala serikali!
Hiyo ni kweli kabisa mkuu.....ila nature ya kazi yangu na mazingira nilipo kwa sasa vinanisaidia kupata mbolea bure kabisa na ardhi ina rutuba ya kutosha. Nguvu kazi ni mimi mwenyewe.

Kuhusu bei hiyo changamoto ya karibia kila bidhaa na nafaka zinazozalishwa au kuingizwa hapa nchini.

Vijana tupambane maana inazidi kuwa tete.
 
Ni Jambo zuri sana Ila serikali iliaribhlu mfumo WA kilimo nchini na ilishindwa kutengeneza mazingira mazuri Kwa wakulima serikali haipo kutupa pesa wananchi Ila ni mara ngapi umesikia wakulima...
Mkuu hutakiwi kujata tamaa kwa changamoto za bei. Mfano mdogo tu waliolima mpunga msimu wa 2019-2020 walipata hasara.

Ila waliolima mpunga msimu wa 2020-2021 wanakula maisha. Vipi bei ya mchele ulipo sasa hivi, msimu huu pamba imeuzwa kwa kilo 1300( hiyo haijawahi kuwepo toka uhuru) msimu huu maharage kilo imeanzia 1500.
 
Hatukulaaniwa, lakini tumenyimwa uwezo wa aarifa, Ikiwa hii ndiyo tafsiri sanifu ya laana basi na iwe hivyo.
Afrika Nzima inafanana, yatupasa tujitambue na tuukubali ukweli...
True boss nchii hii ni ina viongozi wajinga sana na yote ni sababu ya roho zao mbaya ata Mimi sidhani kama bakhresa au matajiri wote nchii hii wameshindwa kuwekeza kwenye madini Ata Kwa njia ya joint venture na makampuni ya nje China makampuni ya nje yanayokuja kuwekeza China lazima yawe na share na wazawa lazima tukumbuke hawa wwawekezaji WA nje wakimaliza shughuli zao wanaondoka na mzawa ata bakisha pesa na ata fanya uwekezaji mwingine apa apa ndani ya nchi kama wazawa wangewekezaga kwenye madini Hadi saivi ingekuwa rahisi ata kupata kampuni ya ndani ya nchi kwenye uwekezaji wa gesi asilia kule mtwara dah tunasafari ndefu sana kwenye hii nchi
 
Mkuu hutakiwi kujata tamaa kwa changamoto za bei. Mfano mdogo tu waliolima mpunga msimu wa 2019-2020 walipata hasara.

Ila waliolima mpunga msimu wa 2020-2021 wanakula maisha. Vipi bei ya mchele ulipo sasa hivi, msimu huu pamba imeuzwa kwa kilo 1300( hiyo haijawahi kuwepo toka uhuru) msimu huu maharage kilo imeanzia 1500.
Mpunga bado upo chini sana labda miezi hui mitatu ijayoo kupanda lazima Ila kiuhalisia biashara ya kulima ninhasara tupu labda uwe na biashara nyingine pembeni
 
Mpunga bado upo chini sana labda miezi hui mitatu ijayoo kupanda lazima Ila kiuhalisia biashara ya kulima ninhasara tupu labda uwe na biashara nyingine pembeni
Ni kweli mkuu ila katika maisha ya sasa usifanye kazi moja tu ukategemea utatoboa maisha.

Lazima uchanganye kazi nyingi ili upate makusanyo mengi kila siku.

Binafsi nafanya kilimo kama mpango wa kando ila nategemea kufuga kuku na bata kwa wingi yote hayo ni kuziba mianya upotevu wa mapato yangu binafsi.

Pia vijana tupunguze usharo unaotupelekea kuitwa ma-handsome wa vijijini ambapo unaishia kuwa videmu vingi vinavyotumalizia hela zetu.
 
Umeandika vizuri sana.

Pamoja na changamoto nyingi za kisera na kimkakati kama taifa kukwama. Pia, vijana bado tumelala kusubiri serikali utukwamue...
Wewe umesema sawia
KICHAWANI ndio tatizo la msingi.
Tanzania ni nchiya kiholela sana, mtu yeyote anaweza kuanza na kupanda hadi kufikia kuwa tajiri.
Kichwa kitulie na kujitahidi kukuza mtaji.
nimesha waona vijana wmeanza kuunza Njugu na muda tuu wakabadili maisha yao nakufungua biashara za maduka au kununua bodaboda na bajaji.
 
Maendeleo ya nchi ni mkusanyiko mdogo mdogo wa maendeleo ya watu wake.

Sasa tuanze na babu zako, na baba zako.

Mmeshayamaliza matatizo yenu ya tangu enzi hizo?
Mkuu vipi kuhusu Singapore,pia wao Walikuwa km Sisi enzi hizo.Mimi naona matatizo ya mtanzania ni zaidi ya ulivyotafsiri.Umejibu kiwepesi sn
 
Back
Top Bottom