Miaka 60 ya Uhuru: Tanzania tuna laana?

Miaka 60 ya Uhuru: Tanzania tuna laana?

Laana Kubwa ni hiki chama kinajiita CCM,hicho ndiyo kimepelekea laana kubwa nchi hii.
Nilipoona sherehe za uhuru wa Tanganyika eti zinapewa kauli mbiu ya "Kazi Iendelee" nilizima TV na kuondoka.
 
Kafara la kukimbiza moto linavyoligharimu Taifa
Km vp mwenge ufutwe Tu maana ni km Una laana

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Ni upumbavu kusherekea UHURU hali hatupo huru.
Wanaofaidika na matunda ya UHURU awazidi 10% bora wakoloni wangeendelea tungekuwa mbali sana.
Nchi za Scandinavian norway, sweden, denmark, China, Malasyia, vietnam tulikuwa nao uchumi SAwa,dola moja ilikuwa SAwa na shilingi 60 ya TANZANIA.Ni aibu sana kupewa misaada na vinchi vidogo SAwa na mkoa kama denmark na sweden sababu wao walipata viongozi wanaofikiri huku raslimali tele zimejaa.
Unaambiwa utoroshaji wa madini umerudi Kwa Kasi Sana

Hii nchi keki wanakula wachache sn

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Unaambiwa utoroshaji wa madini umerudi Kwa Kasi Sana

Hii nchi keki wanakula wachache sn

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Yanatoroshwa then watakuja kutupa misaada na mikopo na sisi hatuna uwezo wa kulipa mikopo yao so wanajilipa.Kila mwenye nafasi ya kutafuna keki anatafuna hasa kwa hofu ya akijitokeza magu mwingine washajilipa vya kutosha.Ila Magu mwingine ni hadi kipite kizazi hiki miaka 40 ijayo,ndivyo huwa.
 
Ni aibu sana kutumia gharama kubwa kusherekea birthday huku una matatizo lukuku.
Choo unategemea kwa jirani, watoto hawana ada, uhakika wa matibabu ni mgogoro.
 
Ni aibu sana kutumia gharama kubwa kusherekea birthday huku una matatizo lukuku.
Choo unategemea kwa jirani, watoto hawana ada, uhakika wa matibabu ni mgogoro.
Kuna katuni kwenye replies za huko juu kapost mshana ya DW huyo birthday boy Tz Hadi stick za meno zimekuwa imported.Hakuna haja ya kusherekea Kwa kweli

3028072_IMG-20211209-WA0273 (1).jpg
 
Dar ndio capital city hii haipingiki na sio Dodoma thus sherehe hazikufanyika Dodoma
 
Umeandika vizuri sana.

Pamoja na changamoto nyingi za kisera na kimkakati kama taifa kukwama. Pia, vijana bado tumelala kusubiri serikali utukwamue.

Vijana tunaopambana pia hatujui tunapambania nini maana hatuna malengo yanayozidi mwaka mmoja.

Binafsi kwa sasa pamoja na kuwa mwajiriwa wa serikali ila nimeamua kulima kwa spidi ya hatari. Naamka saa kumi za alfajiri kila siku kabla ya kwenda kazini saa mbili.

Nimejiwekea malengo ya miaka mitano hadi 2026 niwe mtu wa tofauti kiuchumi. Kwa sasa nimeanza na malengo kuvuna gunia 10 za maharage kwa msimu. Baadaye nitaongeza malengo.

Umasikini wetu kwa kiasi kikubwa unaanzia kichwani.
(Umaskini wetu una anzia kichwani)
 
Leo ni siku ya Uhuru, nimefungulia redio nikatune Wasafi FM nikasikia wanapiga nyimbo ya miaka ya 60-80. Vijana wa sasa huziita zilipendwa. Sijui jina la nyimbo wala aliyeimba simjui lakini nikawa nasikiliza Kwa makini maana ujumbe wa nyimbo ulinivutia sana.

Mwimbaji wa hii nyimbo alikuwa analalamika juu ya ugumu wa maisha Kwa wakati huo. Anasema alioa wanawake wawili lakini inabidi amuache mmoja Kwa sababu maisha yamegekuwa magumu Sana.

Anataja ulanguzi wa bidhaa, akiitaka na sukari jinsi ulivyosababisha ugumu wa maisha wakati huo

Baada ya hii nyimbo kuisha nikawa nawaza tunasherekea sikukuu ya Uhuru wa Tanzania bara,ni Uhuru wa nini, mbona matatizo yaleyale ambayo huyu muimbaji wa enzi hizo aliyoyaimba bado tunayo tena makubwa sana.

Mkulima bado anatumia jembe la mkono,na inatajwa afrika ndiyo bara linaloongoza kwa kilimo duni kuliko bara lolote, Tanzania ikiwemo.

Tangu nakua tunaambiwa Tanzania ni nchi ya pili Kwa vivutio duniani ikitanguliwa na Brazil lakini tunapokea watalii chini ya milioni mbili Kwa mwaka

Leo watanzania wanakamuliwa na Kodi za kila Aina.Juzi Tu hapo wametuongezea mzigo wa Kodi isiyo rasmi, wameibatiza jina tozo.Niliwahi kumsikia mtu mmoja akisema endapo Tanzania ingepata asilimia 10 Tu ya watalii wanaotembelea Paris Ufaransa ambao hupokea watalii zaidi ya milioni 80 Kwa mwaka basi tungepiga hatua kubwa Sana Kama taifa,na masuala ya tozo tusingeyazungumzia

Tuna madini ya kila Aina lakini yamekuwa Kama laana kwwtu.Kila siku yunasikia Stori za kutoroshwa.Juzi tukajenga ukuta mererani lakini tunaambiwa Kasi ya utoroshaji imekuwa kubwa kuliko awali

Kwenye michezo bado tunaendelea kupeperusha bendera ya 'kichwa cha mwendawazimu'
Miaka 60 ya Uhuru viwanja Bora vyenye hadhi ya FIFA ni viwili tena vyote vipo Dar
Tunatajwa kuwa na ligi Bora ya 8 Africa lakini serikali haifanyi maboresho yoyote kwenye viwanja vya mikoani, viwanja vya CCM ndiyo vibovu kuliko. Azam TV anashindwa kufunga camera za kutosha Kwa sababu viwanja vingi vya mikoani havisupport, hadi wakati mwingine analazimika kufunga majukwa Kwa ajili ya studio ya kurushia matangazo Kwa gharama yake binafsi.

Serikali inalalamika ajira hakuna lakini ingeboresha sekta ya michezo vijana wengi wangejiajiri huko Ila imelala fofofo.Ila wakina mwakinyo wakishinda Kwa juhudi zao binafsi ndiyo wanawakumbuka Kwa kuwaita ikulu na bungeni kuwapongeza

Nakumbuka wiki kadhaa zilizopita Rais wa Uganda alikuja kufanya ziara Tanzania.Kwenye hotuba yake Rais wa Tanzania Mama Samia aliongelea swala la sukari,akamwambia Rais wa Uganda wafanyabkashara wa Uganda waingize sukari nchini na kuiita kauli ya waziri wake ya kuzuia sukari kutoka nje ni 'nonsense'

Niliposikia hii nyimbo ya kale hasa hiki kipande cha ulanguzi wa sukari enzi hizo niikaishia kucheka Tu maana miaka mingi baadae bado tatizo la sukari aliloliimba enzi hizo liko pale pale.Tumekwama mahali Kama taifa

Miaka ya 2013/2014 kulikuwa na makala kwenye gazeti la Tazama yenye kichwa cha habari POVERTY IN THE MIDST OF PLENTIFUL (UMASIKINI KATIKATI YA UTAJIRI)

Tumejaaliwa na mwenyezi MUNGU kila Aina ya utajiri lakini tuna umasikini wa kutupwa.Je,Tanzania tumelaaniwa?

Happy independence Day
Aisee umeandika kwa uchungu kila kitu ni kweli
 
Tatizo kubwa la nchi hii viongozi wanapenda shortcut kwenye maisha,hawana uvumilivu na utulivu wa akili,hii kauli ya nonsense ya juz daah,imeniacha hoi . Tangu enzi za mwal. et bado tunalalamika matatizo yale Yale ya 1950's Hadi leo,mi nadhani Kuna haja ya kuwapima akili na tabia zao, hawa viongozi wetu kabla hatujawapa madaraka.zanzbar wako nyuma kimaendeleo kwa sababu ya yetu tz bara,hawa wangeachwa huru ninaamini wangekuwa mbali Sana kimaendeleo. tz bara viongoz wetu ni matatizo !!!
 
Umesema kweli kbs mkuu

CCM imekua ikilazimisha kueaka viongozi vilaza kule Zanzibar, bila ya hivo Zanzibar ingekua mbali sana
 
Leo ni siku ya Uhuru, nimefungulia redio nikatune Wasafi FM nikasikia wanapiga nyimbo ya miaka ya 60-80. Vijana wa sasa huziita zilipendwa. Sijui jina la nyimbo wala aliyeimba simjui lakini nikawa nasikiliza Kwa makini maana ujumbe wa nyimbo ulinivutia sana.

Mwimbaji wa hii nyimbo alikuwa analalamika juu ya ugumu wa maisha Kwa wakati huo. Anasema alioa wanawake wawili lakini inabidi amuache mmoja Kwa sababu maisha yamegekuwa magumu Sana.

Anataja ulanguzi wa bidhaa, akiitaka na sukari jinsi ulivyosababisha ugumu wa maisha wakati huo.

Baada ya hii nyimbo kuisha nikawa nawaza tunasherekea sikukuu ya Uhuru wa Tanzania bara,ni Uhuru wa nini, mbona matatizo yaleyale ambayo huyu muimbaji wa enzi hizo aliyoyaimba bado tunayo tena makubwa sana.

Mkulima bado anatumia jembe la mkono,na inatajwa afrika ndiyo bara linaloongoza kwa kilimo duni kuliko bara lolote, Tanzania ikiwemo.

Tangu nakua tunaambiwa Tanzania ni nchi ya pili Kwa vivutio duniani ikitanguliwa na Brazil lakini tunapokea watalii chini ya milioni mbili Kwa mwaka.

Leo watanzania wanakamuliwa na Kodi za kila Aina.Juzi Tu hapo wametuongezea mzigo wa Kodi isiyo rasmi, wameibatiza jina tozo.Niliwahi kumsikia mtu mmoja akisema endapo Tanzania ingepata asilimia 10 Tu ya watalii wanaotembelea Paris Ufaransa ambao hupokea watalii zaidi ya milioni 80 Kwa mwaka basi tungepiga hatua kubwa Sana Kama taifa,na masuala ya tozo tusingeyazungumzia.

Tuna madini ya kila Aina lakini yamekuwa Kama laana kwwtu.Kila siku yunasikia Stori za kutoroshwa.Juzi tukajenga ukuta mererani lakini tunaambiwa Kasi ya utoroshaji imekuwa kubwa kuliko awali.

Kwenye michezo bado tunaendelea kupeperusha bendera ya 'kichwa cha mwendawazimu'
Miaka 60 ya Uhuru viwanja Bora vyenye hadhi ya FIFA ni viwili tena vyote vipo Dar
Tunatajwa kuwa na ligi Bora ya 8 Africa lakini serikali haifanyi maboresho yoyote kwenye viwanja vya mikoani, viwanja vya CCM ndiyo vibovu kuliko. Azam TV anashindwa kufunga camera za kutosha Kwa sababu viwanja vingi vya mikoani havisupport, hadi wakati mwingine analazimika kufunga majukwa Kwa ajili ya studio ya kurushia matangazo Kwa gharama yake binafsi.

Serikali inalalamika ajira hakuna lakini ingeboresha sekta ya michezo vijana wengi wangejiajiri huko Ila imelala fofofo.Ila wakina mwakinyo wakishinda Kwa juhudi zao binafsi ndiyo wanawakumbuka Kwa kuwaita ikulu na bungeni kuwapongeza.

Nakumbuka wiki kadhaa zilizopita Rais wa Uganda alikuja kufanya ziara Tanzania.Kwenye hotuba yake Rais wa Tanzania Mama Samia aliongelea swala la sukari,akamwambia Rais wa Uganda wafanyabkashara wa Uganda waingize sukari nchini na kuiita kauli ya waziri wake ya kuzuia sukari kutoka nje ni 'nonsense'.

Niliposikia hii nyimbo ya kale hasa hiki kipande cha ulanguzi wa sukari enzi hizo niikaishia kucheka Tu maana miaka mingi baadae bado tatizo la sukari aliloliimba enzi hizo liko pale pale.Tumekwama mahali Kama taifa.

Miaka ya 2013/2014 kulikuwa na makala kwenye gazeti la Tazama yenye kichwa cha habari POVERTY IN THE MIDST OF PLENTIFUL (UMASIKINI KATIKATI YA UTAJIRI).

Tumejaaliwa na mwenyezi MUNGU kila Aina ya utajiri lakini tuna umasikini wa kutupwa.Je,Tanzania tumelaaniwa?

Happy independence Day.
Kiini cha laana ni mwaka 1967
 
Back
Top Bottom