Miaka 58 baada ya ajali ya Kilwa Airport, Taifa limedhalilika

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Tukio la ajali ya ndege Bukoba la jana linafanana sana na tukio la ndege aina ya Douglas DC-3C iliyotokea katika uwanja wa Kilwa Masoko Airport (KIY) mwaka 1964. Ndege hiyo ilikuwa ikitokea Lindi-Kikwet Airport. Enzi viwanja hivyo vikiwa na sifa ya kimataifa.

Ndege hiyo iliyokuwa mali ya Shirika la ndege la mkoloni la East African Airways ilipata hitilafu wakati ikitua katika uwanja huo bada ya propellar ya ndege hiyo kuchomoka na kuukata mlango wa rubani, Ndege ilikuwa ikiendeshwa na Captain Gene Brokensha ambae alipoteza maisha hapo hapo katika ajali hiyo.

Ndege ilikuwa na abiria 22 na watumishi wa ndege 3 akiwemo rubani. Katika ajali hiyo mbaya zaidi alifariki rubani pekee huku abiria na wengine wote wakisalimika baada ya huduma za uokoaji za uwanja huo kuwahi kwa wakati kuzima viashiria vya moto nk.

Miaka 58 baadae katika dunia mpya ya teknolojia, taifa linapata ajali ya ndege baada ya rubani kushindwa kutua na kuipeleka ndege ziwani ufukweni, lakini katika hali ya kushangaza baada ya masaa zaidi ya 6 ndio huduma za uokoaji tena za kienyeji ndio zinafika. Hata Mizimu yangu ya Mbutu Block E, Kigamboni inashangaa tu. Nchi haina helkopta ya kuweza kunyenyua mizigo hata ya tani 5 tu? Nchi yenye maziwa makuu zaidi ya matatu haina boti kubwa za uokoaji "tags". Sasa sisi Watz tunaweza nini ikiwa hata kujiokoa tu hatuwezi kwa ajali nyepesi kama hii?

Kwa muda mrefu, video za mwanzo na picha za ndege hii zilionyesha ndege ikiwa imezama kidogo tu kichwani, kiasi kwamba timu kamili ya uokoaji ingewahi ingeweza kuivuta haraka isizame, lakini hadi uokoaji wa raia wema wavuvi walipoanza kuivuta tayari ilikuwa imezama yote... Ni uzembe wa hali ya juu sana wa serikali. Hakuna lugha unayoweza kuitumia kuelezea hili jambo zaidi ya kusema ni uzembe wa serikali umepelekea kupoteza maisha ya watu wengi, Rubani alijitahidi amefanya kazi yake ipasavyo, ametoa taarifa mapema, lakini response ya kiserikali ni dhaifu.

Poleni sana wahanga wa ajali hii, kuna watu wanahitaji kuwajibika na kuwajibishwa. Tukio hili limetoa taswira ya uzembe katika taifa. Kitengo cha Maafa chini ya ofisi ya Waziri Mkuu, hakijawajibika kwa wakati kuokoa roho za watu ipasavyo, naamini wangewahi mapema eneo la tukio, idadi ya maafa ingepungua. Uzembe huu tulianza kuuona kwenye ajali ya moto Mlimani Kilimanjaro

Soma link hii ASN Aircraft accident Douglas DC-3C VP-KJP Kilwa Masoko Airport (KIY) Kujua ajali hii ya mwaka 1964 na namna wenye akili wa enzi hizo walivyofanya kuokoa maisha ya watu.

Ok, Haujachelewa, Pata Kitabu cha Ujasusi kwa ofa ya 25,000 tu badala ya bei halisi 80,000/=

Nunua kwa:

Tigopesa 0715865544
M-Pesa. 0755865544
LIPA NAMBA TIGO 7489022
LIPA NAMBA VODA 5352627

(YERICKO NYERERE)

CRDB BANK AC No 0152241955000 (YERICKO YOHANESY NYERERE)

(Dar ni free delivery)
Nje ya Dar nauli 8,000/=
Kwamaelezo zaidi piga 0715865544

Kwa watumiaji wa ANDROID nenda Play Store Download sasa Application yetu ya YerickoNyerereApp uweze kujisomea vitabu vyote kwa wiki 5,000/=, Mwezi 10,000/=, Mwaka 30,000/= tu. Link kwenye BIO:
IMG_20221107_100047_511.jpg
 
Ivi Ile Uzi wa bwana maharage ya ukweni Alie tabiri ajali ya ndege Bado upo atakae uona anitag
 
Tukio la ajali ya ndege Bukoba la jana linafanana sana na tukio la ndege aina ya Douglas DC-3C iliyotokea katika uwanja wa Kilwa Masoko Airport (KIY) mwaka 1964. Ndege hiyo ilikuwa ikitokea Lindi-Kikwet Airport. Enzi viwanja hivyo vikiwa na sifa ya kimataifa...
Sina comment, sijui kwanini ccm bwana
 
Back
Top Bottom