Miaka 50 ya Taifa letu, Muda na mafanikio, nini Changamoto

sekulu

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
988
157
Wana JF ebu naomba tujitathmini kidogo,

Tuangalie Muda ulio pita tangu tupate Uhuru, Tujilinganishe na Mataifa mengine ambayo yamepata uhuru baada yetu sisi, Nini tunawashinda au Nini wanatushinda,

Tusiangalie nchi za Ulaya Tuangalie humu humu africa,

Nini Tanzania Tunajivunia ukilinganisha na nchi zingine za Africa??
 
Cha kujivunia? -utulivu (siyo amani)

Tatizo letu? -wavivu (wa kufikiri na kufanya kazi), viongozi wabadhirifu (tunda la jamii vivu)

Tufanye nini? -Tujenge utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii na kufikiri kwa mapana, tubadili uongozi wa magamba hauwezi kuongoza mabadiliko, watakaoongoza baada ya magamba wajenge na kuhimiza kila mtu kwa nafasi yake afanye kazi (siyo kutegemea muujiza wa serikali au chama tawala kama ilivyo sasa, elimu iwe ya kumwandaa raia kujitegemea na kufit mazingira yeyote siyo kukariri mambo.

Kilio changu: Sijasikia chama cha siasa kinachosiistiza na kutoa mikakati ya kila mtu kuchapa kazi. Ni ahadi, ahadi, ahadi zaidi!!!!
 
Tuko katika dimbwi lile lile la umaskini, ujinga na maradhi. Tumehitimu katika usanii. Hatujafikia sehemu ya kujilinganisaha na wengine
 
Kwanza nianze kusema Tanzania itatimiza miaka 50 mwaka 2014.
Tanganyika ndiyo ilipasa kutimiza miaka 50 lakini haipo.

Yalikuwepo mengi ya kujivunia lakini kwa jinsi yalivyoharibiwa ni aibu hata kuyataja.

Kuhusu kufanya kazi naomba ukaisome vizuri ilani ya uchaguzi ya CHADEMA ya 2010-2015.
 
Naona kama badala ya kupiga hatua kwenda mbele tunapiga hatua za kurudi nyuma. Maendeleo yaliyotarajiwa naona kama yanafifishwa na viongozi wetu wasiokuwa na vipaumbele vya nini kifanyike na nini kipewe kipaumbele. Ufisadi unalimaliza taifa na wanaokuwa viongozi wanajali zaidi maendeleo yao badala ya maendeleo ya wote
 
Back
Top Bottom