Waziri Ndubalo usijitumbukize kwenye mgogoro na mashabiki Bali jikite katika kuwapa uraia wachezaji wenye kipaji walipambanie taifa letu

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,206
12,723
Mh waziri (Ndubalo) huu siyo muda wa kutishia mashabiki wa Simba na Yanga Sc katika utani wao wa Jadi ulioota mizizi kwa miaka 80+ mpaka kwani utaonekena Kama Unawapangia namna ya kuishi.

NALIA NGWENA niliposikia kauli yako nilipatwa na ukakasi mpaka nikajiuliza kuwa Mh waziri amekosa Cha maana katika ukuaji wa mpira wetu huu?! Mpaka anaanza kuingilia Kati ushabiki wa Simba sc na Yanga Sc?!

Katika ligi yetu hii Kuna wachezaji wazuri wengi mno ambao mataifa Yao hayawatambui (hayawaiti katika kikosi Cha taifa) wachezaji kutoka Kongo, wachezaji kutoka Ivory coast tunawachezaji kutoka mataifa mbali mbali ambao hata ukipiga hesabu katika kikosi Chao Cha taifa ni ngumu kuitwa.

Kwa nini waziri Ndubalo usichangamke kuokoteza wachezaji wazuri (wenye TALANTA) na unafanya mpango wapate uraia watusaidie AFCON 2027?

Kama alipewa Kibu denisi Kuna wachezaji wazuri Kama Max Nzengeli n.k Hawa ukiwapa uraia hawatokuangusha katika kulipambania taifa letu maan nchi Kama ya Kongo Ina wachezaji wengi sana kuitwa Katika kikosi ni ndoto.

Ushauri wangu kwa Waziri wa michezo : Mashabiki wa Simba sc na Yanga Sc ni watani wa Jadi kuwapangia wafanye nini katika utani wao ni kuwaingilia uhuru wa furaha Yao unapaswa kufanya Jambo litakalo acha legacy katika uongozi wako lakini siyo kuingilia uhuru wa mashabiki wa kariakoo.
 
Yani uhangaike kumpa urai mchezaji kama Max Nzengeli? Ni kuja,a wachezaji mizigo kwenye taifa, wachezaji wa level za nzegeli bongo wapo wengi tu
 
Yani uhangaike kumpa urai mchezaji kama Max Nzengeli? Ni kuja,a wachezaji mizigo kwenye taifa, wachezaji wa level za nzegeli bongo wapo wengi tu
Wataje majina
Halafu siku nyingine uelewe maana ya neno N.K
 
Naona bora watowe uraia pacha kuliko kutoa uraia kwa mchezaji anaetaka kuendelea kuwa na uraia wa alipo zaliwa.

Pamoja na wazaliwa wanao ishi nje ya Tanzania(Diaspora’s)nao wafaidike na uraia wa nchi walio zaliwa.
 
Huyu na yule mwenzake wa mchele wa msaada kiukweli kauli zao mbele ya waandishi hazisadifu vyeo na wasifu wao, sijajua ni siasa au ndo mama yao anapenda vitu kama hivo
 
Waziri kama huyu anaweza kuwapa watu sababu ya ku entertain conspiracy theories kuwa serikali huwa inatoa habari za vituko kwa makusudi ili kuondoa mazungumzo kwenye mambo ya msingi.

Wapenda conspiracy theory wanaweza kukuambia baada ya movie ya Mabeyo kuonekqna imezaa maswali mengi kuliko majibu, na inataka kufujua moto kuliko ilivyotarajiwa, serikali inataka kuifunika movie hiyo kwa movie nyingine ya maneno yasiyo kichwa wala miguu kuteka akili za watu.

Mimi siamini hizi conspiracy theories, lakini naweza kuona inakuwaje mpaka watu wakaamini.
 
Mleta Uzi mjinga sana inamana taifa limekosa watu wenye vipaji mpaka tuanze kuwapa watu uraia, unaacha kuleta mbinu za taifa kuinua vipaji wewe unaleta ushauri wa kijinga , yani kama kweli wewe mwalimu nazani watoto unaowafundisha wanabwela bwela. SPECIALIST IN FAILURE
 
KAMA MLIVUNJA MICHUANO YA MPIRA MASHULENI

NA SHIRKISHO LENU LIMELALA UNADHANI UNATAPATA WAPI VIPAJI?!

ACADEMIC YA BALL MTIBWA NA ZINGINEZO HAZIPEWI KIPAO MBELE UNADHANI UTAPATA VIPAJI WAZAWA?!

KAMA MNAWAWAPIGIA KURA VIONGOZI WAZEE NA WASIOJUA CHOCHOTE KIHUSU MPIRA MNADHANI MTAPATA WAPI VIPAJI WAZAWA?!

KAMA WAZAWA HAWAPATI NAFASI KWENYE TIMU ZA TAIFA MPAKA WATOE TEN % UNADHANI UTAPATA VIPAJI?!
 
Mleta Uzi mjinga sana inamana taifa limekosa watu wenye vipaji mpaka tuanze kuwapa watu uraia, unaacha kuleta mbinu za taifa kuinua vipaji wewe unaleta ushauri wa kijinga , yani kama kweli wewe mwalimu nazani watoto unaowafundisha wanabwela bwela. SPECIALIST IN FAILURE
Hii mbinu ya kutoa uraia imetumika nchi zote zilizo endelea unazo zijua wewe
 
Waziri kama huyu anaweza kuwapa watu sababu ya ku entertain conspiracy theories kuwa serikali huwa inatoa habari za vituko kwa makusudi ili kuondoa mazungumzo kwenye mambo ya msingi.

Wapenda conspiracy theory wanaweza kukuambia baada ya movie ya Mabeyo kuonekqna imezaa maswali mengi kuliko majibu, na inataka kufujua moto kuliko ilivyotarajiwa, serikali inataka kuifunika movie hiyo kwa movie nyingine ya maneno yasiyo kichwa wala miguu kuteka akili za watu.

Mimi siamini hizi conspiracy theories, lakini naweza kuona inakuwaje mpaka watu wakaamini.
Bro ngurumo naona mabeyo ametoa episode2 kupitia link ile ya mwanzo pitia
 
Back
Top Bottom