Miaka 50: Tumethubutu, Tumeweza na Tunasonga Mbele...

Miaka 50: Tumethubutu, Tumeweza na Tunasonga Mbele...

Uhuru wa miaka 50 tunaosheherekea mwaka huu ni uhuru wa nchi ya Tanganyika; naomba kusaidiwa hapa, kwa nini tunausherekea watanzania wote kama vile ndo uhuru wa Tanzania? Au ndo mapungufu ya muungano?
 
Huu ndo muda muafaka wa kuchambua uhalisia na ukweli wa kauli-mbiu hii. Kwa sheria za UK, kutengeneza kauli mbiu yenye kukinzana na ukweli kama hii, serikali ingepigwa fine kubwa.
 
Tumedhubutu kwa kupata rais anayezunguka kutafuta wawekezaji.
 
Mimi nikiwa kama mlipa kodi halali wa nchi yangu Tanzania tukiwa tunakwenda kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa taifa langu mimi najivunia haya:
  1. Umeme wa mgao.
  2. Uhaba wa mafuta.
  3. Ufisadi.
  4. Raisi kuwa muongo kwa ahadi zisizotekelezeka.
  5. Uhaba wa ajira kwa vijana.
  6. Hali ngumu ya maisha! Bora ya jana kuliko ya leo.
  7. Mikataba feki na hewa kwa wawekezaji.
  8. Mafisadi kutochukuliwa hatua za kisheria na huku wanajulikana.
  9. Serikali kua Legelege.
  10. Ndani ya serikali ya CCM kila mtu ni mwizi. Sijui wewe mwenzangu unajivunia nini ndani ya miaka hii 50 ya uhuru......!!!!!
 
viongozi wetu bana. Wamejaribu kuiba, wameweza na wanatutaarifu wanasonga mbele.
 
Huu ndo muda muafaka wa kuchambua uhalisia na ukweli wa kauli-mbiu hii. Kwa sheria za UK, kutengeneza kauli mbiu yenye kukinzana na ukweli kama hii, serikali ingepigwa fine kubwa.
misemo ya wanaofikiria kwa makalio.
Kazi kwelikweli
 
Kwa kutunga kauli mbiu tamu tamu kwa viongozi wa Tanzania mbona wanaweza sana,tatizo lipo ktk uhalisia wa kauli hizo.Mfano "kilimo kwanza"Tanzania bila ukimwi inawezekana"na mingine mingi nisaidieni kuijazia hapa
 
Kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru imetolewa leo,ambayo ni 'Tumethubutu,Tumeweza na tunasonga mbele' Je iko relevant na Tanzania ya leo miaka 50 baada ya Uhuru?
Kwa kauli hizo wanaziweza tatizo utekelezaji ndio ziro,akili za wanaofikiri kwa kutumia makalio
 
Mimi nikiwa kama mlipa kodi halali wa nchi yangu Tanzania tukiwa tunakwenda kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa taifa langu mimi najivunia haya:
  1. Umeme wa mgao.
  2. Uhaba wa mafuta.
  3. Ufisadi.
  4. Raisi kuwa muongo kwa ahadi zisizotekelezeka.
  5. Uhaba wa ajira kwa vijana.
  6. Hali ngumu ya maisha! Bora ya jana kuliko ya leo.
  7. Mikataba feki na hewa kwa wawekezaji.
  8. Mafisadi kutochukuliwa hatua za kisheria na huku wanajulikana.
  9. Serikali kua Legelege.
  10. Ndani ya serikali ya CCM kila mtu ni mwizi. Sijui wewe mwenzangu unajivunia nini ndani ya miaka hii 50 ya uhuru......!!!!!
11. Kupiga Machinga na kuwanyanganya vitu vyao.
12. Kupokea mgawo asilimia 3% ya mrahaba wa Dhahabu.
 
Ni kauli mbiu nzuri kabisa.Tumethubutu kujitawala na tumeweza. tumeweza kupunguza umasikini kwa hali ya juu sana na hili nalo tumeweza ingawa jitihada bado zinafanyika maana kutokomeza umasikini ni mchakato na mwisho tunasongambele katika kujiletea maendeleo na hili tumeliona chini ya serikali ya Rais Kikwete kwa kuwekeza sana katika elimu mfano Chuo Kikuu Cha Dodoma, na katika kilimo kwani ni hivi karibuni benki ya wakulima inaanzishwa ukiachilia mbali benki ya wanawake ambayo imekwisha anza kazi.Hakika tunasongambele.
.


KWELI serikali ya ccm imejitahidi kutufikisha hapa tulipo, hilo hatukatai, BIG UP, LAKINI, maendeleo tuliyo nayo ni aibu kujisifu nayo kwa miaka 50, maendeleo haya tuliyo nayo yangetakiwa yawe miaka 20 iliyopita, sio sasa, kwa taarifa yako UMASIKINI sio kwamba unapungua, kwa miaka hii saba ya kikwete umasiki umeongezeka mara dufu, je unaweza kuamini katika nchi hii kuna watu wanapata mlo mmoja tu tena wako mjini? kunafamilia zinashindwa kupeleka watoto shule kwa kukosa pesa ya sare za shule? chuo kikuu? niwazazi wangapi makabwela ambao wanauwezo wa kumsomesha mtoto kufikia huko, kila siku tunazidi kuweka tofauti kubwa kati ya tabaka la wasomi na wasio soma, walionacho na wasio nacho, tunakwenda wapi? Je ni haki kujisifu, tunatamba na barabara za lami nchi nzima, kabwela kijiji na alie mjini itamsaidia nini, utasema kusafirisha mazao, yapi? jembe la mkono, wanao nufaika na hayo mazao kidogo ni wafanyabiashara wakubwa. HOPELESS, Wanafunzi wangapi wanamaliza hivyo vyuo vikuu wanakosa ajira? hawawezi hata kujiajiri. viwanda vimekufa, wawekezaji wanakimbilia kenya, nani anataka kuwekeza kwenye nchi isiyo kuwa na umeme? kwa hali tuliyonayo hata viwanda vilivyo baki vitakufa. TUMETHUBUTU kujitawala!!! miaka hamsini bado bajeti yetu inategea wahisani kwa asilimia kubwa, nchi hii bado ni watumwa kwa wahisani, wanauwezo wakaamua watakalo wao ndo lifanyike katika nchi hii.
IN SHORT tunaingia miaka hamsini kwa aibu. aibu, aibu

GOD BLESS TANGANYIKA, 50 YRS OF TANGANYIKA (not tanzania).

 
Kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru imetolewa leo,ambayo ni 'Tumethubutu,Tumeweza na tunasonga mbele' Je iko relevant na Tanzania ya leo miaka 50 baada ya Uhuru?
.


Hivi Tanzania ilipata uhuru lini na ilitawaliwa na nani?
 
Kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru imetolewa leo,ambayo ni 'Tumethubutu,Tumeweza na tunasonga mbele' Je iko relevant na Tanzania ya leo miaka 50 baada ya Uhuru?

Nakusaidia tu, tanzania ni miaka 47. Tanganyika the late ndio ingekua hai ingetimiza miaka 50. RIP.
 
Hawa jamaa mimi hata siwaelewi kabisa , yaani wameshakaa madarakani kwa miongo mitano , ni miaka 50 sasa tangu tupate uhuru.

Na kila kukicha kwa mtanzania wa kawaida hali yake ni afadhali ya jana. Sijui watatuambia nini, tukiwaomba mapato na matumizi ya miaka 50 tangu tupate uhuru. Yaani hata hapa Kibaha , Mailimoja hakuna chochote wanachokifanya. Yaani barabara mbovu, huduma za afya mbovu, ajira hakuna na umasikini unaongezeka kila kukicha.

Lakini wenyewe watakuambia nchi inapiga hatua sana , maendeleo yanaongezeka. Lakini ukilinganisha muda waliopewa wa miaka 50 tangu tupate uhuru na maendeleo yaliyofikiwa ni sawa sawa na sifuri kabisa. Muda umetumika mwingi mno na maendeleo yenyewe ni ya kasi ya kobe ! Loooo..!
 
I'm proud of my Tanzania,wus up with this Rwanda crap?...are you serious? At least we can complain when the gas prices goes up,when we gained our independence,most indegeneous kids were running,cheering a woman driving a car....but it could've been better.

1. Why are we not suprised that you are proud of "your" TZ? .. jibu unalo
2. Rwanda .. ? jibu unalo!

Sasa unauliza nini? hujui kitu gani kinaendelea .... au have you become so dense with arrogance na bangi za madaraka and stupidity kiasi kwamba you cannot tell your ass from your elbow!!!!
 
NITAPENDA KUJUZWA:

Matatizo ya mafuta na umeme ukiacha mengine yakiwemo ya kuporomoka thamani ya shilingi tutayatafsiri vipi katika huu muktadha?
Ni matokeo ya kuthubu au ndio kuweza?
 
Ni kauli mbiu nzuri kabisa.Tumethubutu kujitawala na tumeweza. tumeweza kupunguza umasikini kwa hali ya juu sana na hili nalo tumeweza ingawa jitihada bado zinafanyika maana kutokomeza umasikini ni mchakato na mwisho tunasongambele katika kujiletea maendeleo na hili tumeliona chini ya serikali ya Rais Kikwete kwa kuwekeza sana katika elimu mfano Chuo Kikuu Cha Dodoma, na katika kilimo kwani ni hivi karibuni benki ya wakulima inaanzishwa ukiachilia mbali benki ya wanawake ambayo imekwisha anza kazi.Hakika tunasongambele.
Ndiyo, ni kauli mbiu nzuri kabisa kwa wezi, mafisadi na mafisadi papa waliosheheni ndani ya CCM. Ni kweli kabisa mmepunguza umasikini kwenu na familia zenu, mmeongeza saizi za mikanda mnayovaa nyinyi na watoto wenu, mmegawana hadi nyumba za serikali mkazikarabati kwa fedha za kodi tunazolipa na kuzipangisha, tena kwa malipo ya fedha za kigeni, mmeuza ardhi zetu kwa wageni wanaotunyanyasa na kutusambazia sumu huku ardhi tuliyoirithi toka kwa mababu zetu ikifukuliwa na kuachiwa mashimo! Mmeuziana karibu viwanda vyote kiasi cha kujitapa na hiyo kauli mbiu yenu ya kusema mmeweza! Mmewafanya watoto wetu kusoma wakiwa wameketi sakafuni na kuiingiza nchi nzima katika giza totoro - miaka 50 tangu tujitawale! mmeyafanya maisha yetu kuwa magumu na yasiyoelezeka huku ya kwenu ni kama mnaishi Manhattan vile! Ndiyo, mmefaulu vema maana miaka sita tu iliyopita sukari tulikuwa tukiinunua kwa Sh. 400 kwa kilo, sasa ni zaidi ya 2000 na sehemu nyingine kama kwetu Kagera Nkanda, Makere, Herushingo hadi Bukholi, Kasongamile na Bupandwamhela ni Sh. 3,000 kwa kilo. Simenti ilikuwa Sh. 7,000 na sasa inakaribia Sh. 25,000. Hatujui "mafanikio" yenu hayo yatakapotufikisha miaka minne iliyobaki maana hata soda iliyokuwa 200/= sasa ni Sh. 700/=, na barabara alizoziacha mwingereza mwaka 1961 huku kwetu Kasulu, Kibondo na Kigoma zimebaki kama zilivyokuwa na pengine kuharibika zaidi wakati zinazoelekea kwenu zinabanduliwa lami chakavu na kuwekwa mpya!.
Ila mkumbuke kwamba hakuna refu lisilo na ncha na kwamba hata utawala wa Rumi uliokuwa na nguvu za kutisha ulifikia tamati, na mpende msipende mnafikia tamati sawa na iliyomkuta Ben Ally wa Tunisia, Mubaraka wa Misri na El Assad wa Syria. Kumbukeni Mungu ni wetu wote hata sisi mliotugandamiza kwa miango kadhaa sasa. Mungu ibariki Tanzania na tuangamizie fidhuli ya wezi, vibaka, mafisadi na genge la wahalifu walioiteka nyara serikali yetu chini ya dude linalojiita CCM.
 
No no no
1- Hatujathubutu, kwani hadi leo baadhi yetu ni watumwa ndani ya nchi yetu, tunanyanyaswa,
tunaonewa na tunauliwa na hao hao wazungu kupitia sisi wenyewe ( mauaji ya Tarime)
2- Hatujaweza, hadi leo bajeti yetu inategemea wazungu achilia mbali misaada n.k.
3- Hatujasonga mbele ukilinganisha na tulioanza nao au tulio waacha nyuma.(Kenya, Rwanda)
MWL kwakweli umenifurahisha umefanya summary zuri. excellent
 
Hamna kitu hapo, hizo ni kauli kama zile za kwenye uchaguzi ambazo hazina ukweli wowote.Wana maneno mengi sana lakini vitendo vya kiungwana hawana, kwa mtazamo wangu kauli mbiu ingekuwa 'NI WAPI TULIPOJIKWAA' ili siku ya miaka 50 tufungue mjadala wa nini kimetukwaza kwenye maendeleo ya nyanja zote na nini kifanyike ili kuweza kusonga mbele.Hayo maneno pekee hayawezi kutukwamua kwenye lindi la umasikini.
 
Inasikitisha sana kudanganya watoto wetu ati wachange sh 500 kwa ajili ya shere za uhuru ambao wao awajauona na walichokishuhudia zaidi ni utapeli na ufisadi wa serikali za kikwete na mkapa

sasa najiuliza hivi tunawetendeahaki ahwa watoto kweli..na hii miaka 50 ni ya uhuru ama uhuni na ujambazi leo tumeletewa majina mapya ya ufisadi wakina
lowassa edward
chenge andrew
lukaza
mramba na mgonja at least hawa wamjenga barabara na hela za wizi ukiacha tusi la watanzania tule majani sababu ndege ya billion 50 ililetwe

leo tuna kingunge wakilimwingine arusha nae ameona asiwe mkiya kusikia watu wamechota kadhaa nae aakaamua kuhifadhi chake..je wewe ni mtarajiwa waufisadi ???
 
Wakati tukijiandaa kwa maadhimisho ya miaka hamsini tangu kupata uhuru wa kisiasa,
inasikitisha kuona sehemu kubwa ya utajiri na rasilimali ya Tanzania iliyopaswa kuwa ni
kwa ajili ya mafao ya wengi, inaendelea kuwanufaisha wachache ndani ya jamii, kinyume
kabisa na mipango na mikakati iliyowekwa na waasisi wa Taifa hili, wakati wa kupigania
uhuru; misingi ya uadilifu, uzalendo na umoja wa kitaifa inazidi kumong'onyoka siku hadi
siku, hali ambayo inasababisha kustawi kwa ubinafsi, ufisadi na kinzani za kijamii.

Tanzania kadiri ya vigezo vya Mashirika ya Fedha ya Kimataifa ni kati ya nchi masikini zaidi
duniani, lakini imekuwa na mvuto mkubwa kwa wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali za
dunia, wanaokimbilia nchini kutafuta madini.

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Tanzania imefanikiwa kuuza dhahabu yenye thamani
ya zaidi ya dola bilioni mbili nukta tano, lakini, cha kushangaza imeambulia dola milioni mbili
nukta saba, hali inayoonesha kimsingi, ukosefu wa haki na usawa katika soko la kimataifa.




Matajiri wanaendelea kufaidika na mikataba ya madini, wakati kuna mamilioni ya watu wanaokufa
kwa baa la njaa, umasikini na magonjwa, katika maeneo haya yenye rasilimali na utajiri mkubwa
kiasi hiki.

Baadhi ya watu wanaendekeza rushwa na ufisadi; maadui wakuu wa haki na usawa kama
alivyobainisha Mwalimu Nyerere wakati fulani. Masuala haya yameleta mpasuko wa kijamii ambao
kwa sasa ni hatari kubwa kwa ustawi na maendeleo ya Watanzania.

Mikataba ya madini, imeendelea kuwanufaisha wawekezaji kutoka nje ya nchi na wananchi wa
Tanzania kuendelea kuogelea katika umasikini wa kipato, licha ya kuzungukwa na utajiri wa
rasilimali. Uchumi wa Tanzania utaendelea kudidimia, ikiwa kama hatutarudisha uzalendo wa
kuipenda nchi yetu.

Rushwa na ufisadi vinaendelea kuota mizizi katika mioyo ya watu, jambo ambalo itakuwa vigumu
kulifuta kwa kipindi kifupi, kama ilivyo dhana ya udini, iliyoibuliwa na baadhi ya wanasiasa kwa
mafao yao binafsi.




Hivi tufanye nini jamani? Naomba mchango wenu wakuu...
 
Back
Top Bottom