Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Mwaka 1980 wakati Mzee Robert Mugabe anaanza kuongoza Zimbabwe mimi nilikuwa nasoma chekechea iliyokuwepo katika majengo ya Forodhani Primary School.
Leo hii kidevu changu kimeanza kujaa nywele nyeupe na nikienda kwa kinyozi naziona nywele nyeupe zidondoka kutoka kichwani, bado Mzee Mugabe anatukanana na Wazungu akiwa kama rais wa Zimbabwe!.
Mwaka 1986 wakati nipo darasa la sita pale pale Forodhani, Mzee Museveni ndipo alipokuwa akiingia madarakani kule Uganda akiwa ameipata nchi kwa mtutu wa bunduki, leo hii Museveni huyo huyo anagombea urais kwa maana ya kutaka kuendelea kubakia madarakani?.
Freeman Mbowe aliingia kwenye uongozi wa juu wa CHADEMA mwaka 2004, kwa matarajio kwamba ikifika mwaka 2014 awe ameachia madaraka baada ya vipindi viwili vya uongozi kumalizika.
Lakini wakati muda wake wa kukaa kwenye uongozi ukiwa unakaribia kuisha, katiba ya CHADEMA ikabadilishwa na mpaka sasa bwana mkubwa bado ni kiongozi mkuu.
Tayari ana miaka 12 kwenye uongozi, na taratibu anaelekea kule kule kwa kina Mugabe na Museveni. Muda huwa unakimbia kwa kasi sana. Bwana mkubwa huyo anaweza kutimiza miaka 20 akiwa kiongozi mkuu halafu ikaja miaka 30 akiwa kiongozi. Time passes so fast.
Sifa mojawapo ya demokrasia ni ule uwezo wa kuandaa mrithi wa uongozi, ili aje aendeleze yale ambayo tayari yameshafanyika.
CHADEMA wasipokuwa waangalifu wanaweza kujikuta wanatumia neno demokrasia bila ya kuwa na mfano hai wenye kuonyesha kuliheshimu, kuanzia ngazi ya juu kabisa.