Mdudu halisi
JF-Expert Member
- May 7, 2014
- 2,730
- 4,771
Mimi ni mkulima niko huku kijijini Lusewa. Sina pembejeo za kilimo, mazao yangu yamekosa bei ya uhakika sokoni (nanyang'anywa), wanangu hawapati elimu bora kwani kuna mrundikano madarasani na hawasomi katika mazingira rafiki kwa mtoto, huduma za afya ni mbovu kupita maelezo kwani mara niendapo hospitali natakiwa kununua dawa kwenye maduka ya madawa na sizipati toka hospitalini hapo, usafiri wa kawaida huku kwetu ni wa kutumia "maguta" yaani pikipiki zenye matairi matatu, umeme tunakutana nao pindi tuendapo mjini. Sasa ndugu yangu badala ya kuongelea shida tuzipatazo sisi wakulima wa Lusewa na kuishauri serikali ya CCM na Magufuli watupunguzie ukali wa maisha, wewe unamwongelea Mbowe sijui, ambaye sisi huku Lusewa hatufahamu anakoishi na wala kazi anayofanya. Mbowe ni nani kwenye maslahi yetu sisi wavuja jasho? Wakati mwingine, ukishiba acha kuwadhihaki wenye njaa.