Miaka 36 ya Mugabe Zimbabwe na 12 ya Mbowe CHADEMA

Miaka 36 ya Mugabe Zimbabwe na 12 ya Mbowe CHADEMA

hahahaaaaaaaaa! sasa mnakereka nini yeye kuwepo kwa matakwa ya wana CDM? nyie mna lichama lenu? komaeni nalo kwa sana japo linaumwa ule ugonjwa mbaya kabisa!
 
Its matter of tym mkuu soon atafall huko hata mugabe alikuwa 12 kama mbowe
i mean huyu mbowe ni mkuu wa chama mkuu but wale ni wakuu wa nchi ,maana sasa tusije tukamu include kwajima mkuu wa ufufue na uzima church then tukafika hadi mpk kwa kadinali pengo kama isuue ni tym,so naona kama hawa kina museveni kagame wapo kwe category yao,afu mkuu hapa kwa akina mugabe naomba tumuongeze na putin
 
Shikamoo mkuu
 
Ila nawaambia kuwa kamwe ccm haiwezi kuokolewa na mtu 1 ambae ni makufuli! huu ni mchezo wa mtu mmoja (one man show) hao wengine (mawaziri) ni washehereshaji tu.
Haiwezekani mtu 1 ndio aokoe lichama tena ambalo liko hoi bin taabani bin Mwaisela!
 
I see kaka Zitto hapo ndipo alipoanza kuonekana msaliti, hahahaha siasa bado Africa
Zitto ana bahati. Ule mkwara wake kwamba kaaga kwao na atakayejaribu kumdhuru kwake mpaka panya watateketea naona ulimsaidia. Otherwise huyu mwenyekiti wa maisha angekuwa amesham-Chacha Wangwe!
 
kweli nyani haoni kundu lake, vipi kuhusu nyie Chama cha Makaburu lini mtaacha kuifanya zenji km koloni? Lini mtaachia wengine waitawale Tanganyika,
Lini mtaachia? Kwenye siasa kuna kuachia? Ulishaona wapi chama kinaachia tu? May be siku wakipatikana wapinzani wa maana na siyo hawa wababaishaji vingunge wa ufisadi na gia zao feki za angani.
 
Mugabe - Raisi (1980 ........
Museveni - Raisi (1986 .......
Mbowe - Mwenyekiti wa Chama (2004 .....
Jk - Mwenyekiti wa chama (2005 ......

Tafakari
JK anajulikana lini ataachia ngazi, huyo Mbowe upo uwezekano ukifika wakati mwingine wa uchaguzi katiba ikabadilishwa tena. 2014 ulikuwa ndio uwe mwisho wa vipindi vyake viwili vya uongozi. JK hajawahi kushinikiza katiba ya CCM iguswe eti kwa sababu ya yeye kuendelea kuwa mwenyekiti wa CCM.
 
Kwa hiyo tulia mpaka JK atoke madarakani ndio uje na hoja yako. Usiwe mtabiri wa kwa upande wa Mbowe. Je Mbowe asipogombea tena utasema nini ?
 
Kwa hiyo tulia mpaka JK atoke madarakani ndio uje na hoja yako. Usiwe mtabiri wa kwa upande wa Mbowe. Je Mbowe asipogombea tena utasema nini ?
Sihitaji kutulia mpaka JK atoke madarakani. Utaratibu wa CCM siku zote haukiukwi kwa sababu eti ya matakwa ya kiongozi wa juu. Mbowe keshapitiliza muda wake kwa miaka miwili, ndio maana nimetoa onyo yasijekuwa kama yale ya kina Mugabe na Museveni. Mbowe asipogombea tena utakuwa ni ushindi wa dhana nzima ya demokrasia, na actually neno CHADEMA litakuwa limeheshimiwa kwa sababu ile DE inawakilisha demokrasia.
 
Ni kweli ulichosema ila usisahau na ccm imekaa madarakani muda mrefu sana nayo inatakiwa kupumzika 1977- 2016
Mbowe ndoto zake ni Kuikabidhi TZ chini ya CHADEMA basi na ataachia nafasi ya uenyekiti bila shida.
Inachotakiwa ni ninyi ccm kukabidhi madaraka kwa CHADEMA Tanganyika na CUF kule Zanzibar over!
 
Ambaye bado hana uwezo hawezi kukabidhiwa nchi kirahisi tu. CCM ina succession plan kubwa sana, imelea wanasiasa wengi ambao hurithishana nafasi za uongozi kadri kizazi kimoja kinavyoonyesha kupevuka kisiasa. CHADEMA inapaswa kujenga misingi ya uwezo wa chama kuwa na uwezo wa kurithishana uongozi. Majina ya Lowassa na Membe yanakatwa halafu bado anakuwepo mtu mwenye uwezo kama JPM, Lowassa kaenda CHADEMA na kupata kura milioni 6, naamini hata Membe kama angeenda upinzani angeweza kupata kura nyingi tu. Yaani CCM kwa sababu ya ubora wake katika kuandaa vizazi vya viongozi, haitetereki hata wanachama wenye ushawishi wanapoondoka.

Ili CHADEMA muweze kufikiriwa kupewa uongozi wa nchi inabidi mjijenge ili ndani ya chama muwe na watu walioandaliwa kwa miaka mingi. Miaka 39 ya CCM huwezi kulinganisha na ukongwe wa kina Republican na Democrat
 
Mtoa mada hujamtendea haki Mbowe kwa kumlinganisha na viongozi hao uliowataja maana vigezo havilinganishiki.. Haki ingekuwa kumlinganisha na Mrema, Cheyo, au basi wenyeviti wa vyama vyote vilivyoanzishwa 1992-2000, nani bado anashikilia uenyeviti. Namshauri mtoa mada aitendee haki akili aliyopewa na mwenye enzi Mungu.
 
Ili CHADEMA muweze kufikiriwa kupewa uongozi wa nchi inabidi mjijenge ili ndani ya chama muwe na watu walioandaliwa kwa miaka mingi. Miaka 39 ya CCM huwezi kulinganisha na ukongwe wa kina Republican na Democrat[/QUOTE]

Siasa za Afrika zinatofautiana na nchi za ulaya na marekani Mapinduzi ya kuvitoa vyama vikonge vinafanyika na viongozi waliotoka kwenye vyama Tawala na kuhamia Upinzani mfano. Bingwa mutharika-Malawi, Somebody pale Kenya alitoka KANU, Zambia, Ghana na nyinginezo. Sababu moja kubwa ninayokubalianan na wewe na kuiboresha ni Kwamba kutokana na Upeo mdogo wa wananchi wa Nchi za Afrika wanafikiri Rais ni lazima awe ameshika angalau madaraka ya Uwaziri au mamlaka makubwa serikalini. Ndio maana Dr.Slaa kwa kipindi chake alikuwa anajaribu sana kuwaelimisha Wananchi kwamba hakuna Elimu ya Urais duniani bali kuna sifa za mtu kuwa Rais.
Membe asingeweza kupokelewa UKAWA kwa kupewa Cheo cha kugombea Urais na angepewa asingevuka hata KURA millioni 2. Lowasa sijui JPM hawana hadhi ya viongozi waliotukuka kama unavyotanabasiha hapo. JPM ni sehemu ya hayo Majipu kama umechukulia ndio mfano wa kiongozi bora. kwenye serikali iliyopita kuna majipu mengi sana pale wizara yaujenzi na yaliibuliwa na PPRA na yeye ni sehemu ya zao la majipu ndio maana kuna majipu mengi hatoyagusa
 
Mtoa mada hujamtendea haki Mbowe kwa kumlinganisha na viongozi hao uliowataja maana vigezo havilinganishiki.. Haki ingekuwa kumlinganisha na Mrema, Cheyo, au basi wenyeviti wa vyama vyote vilivyoanzishwa 1992-2000, nani bado anashikilia uenyeviti. Namshauri mtoa mada aitendee haki akili aliyopewa na mwenye enzi Mungu.
Nimemlinganisha na hao viongozi wa nchi kwa sababu wote wamefanya dhambi ile ile moja. Kutengeneza mazingira ambayo yanawafanya wanabakia kwenye madaraka. Mbowe alipaswa kuachia uongozi mwaka 2014, ukiwa ni mwaka wa kumi tangu akabidhiwe chama. Yeye katengeneza mazingira ya kubadili kifungu cha katiba ili aendelee kuwa mwenyekiti. Akili yangu ninaitendea haki siku zote, ndio maana nipo tayari kujenga hoja kwa kuulinganisha ujanja wa CHADEMA katika kumuongezea muda mwenyekiti wao na ujanja wa madikteta wa Afrika kina Mugabe na Museveni.
 
Ili CHADEMA muweze kufikiriwa kupewa uongozi wa nchi inabidi mjijenge ili ndani ya chama muwe na watu walioandaliwa kwa miaka mingi. Miaka 39 ya CCM huwezi kulinganisha na ukongwe wa kina Republican na Democrat

Siasa za Afrika zinatofautiana na nchi za ulaya na marekani Mapinduzi ya kuvitoa vyama vikonge vinafanyika na viongozi waliotoka kwenye vyama Tawala na kuhamia Upinzani mfano. Bingwa mutharika-Malawi, Somebody pale Kenya alitoka KANU, Zambia, Ghana na nyinginezo. Sababu moja kubwa ninayokubalianan na wewe na kuiboresha ni Kwamba kutokana na Upeo mdogo wa wananchi wa Nchi za Afrika wanafikiri Rais ni lazima awe ameshika angalau madaraka ya Uwaziri au mamlaka makubwa serikalini. Ndio maana Dr.Slaa kwa kipindi chake alikuwa anajaribu sana kuwaelimisha Wananchi kwamba hakuna Elimu ya Urais duniani bali kuna sifa za mtu kuwa Rais.
Membe asingeweza kupokelewa UKAWA kwa kupewa Cheo cha kugombea Urais na angepewa asingevuka hata KURA millioni 2. Lowasa sijui JPM hawana hadhi ya viongozi waliotukuka kama unavyotanabasiha hapo. JPM ni sehemu ya hayo Majipu kama umechukulia ndio mfano wa kiongozi bora. kwenye serikali iliyopita kuna majipu mengi sana pale wizara yaujenzi na yaliibuliwa na PPRA na yeye ni sehemu ya zao la majipu ndio maana kuna majipu mengi hatoyagusa[/QUOTE]
Umeongea mengi lakini pointi yangu ni moja. CHADEMA wamebadili katiba ili mwenyekiti aendelee kubaki madarakani sawa sawa na madikteta wa Afrika. Uzoefu unaonyesha kuwa bado hatujawa na watu wengi ambao kwa uwezo wao wenyewe bila ya kupitia mifumo ya chama wanaweza kuwa marais wazuri. Nchi zilizoendelea zinao mabilionea wenye uwezo huo, sisi bado sana. JPM sio jipu kama unavyotaka kuaminisha watu, angekuwa ni jipu asingekuwa na jeuri ya kuwaambia walio chini yake wasipande ndege kwenda nje ya nchi. Nafsi yake isingekuwa na ujasiri wa kufikia maamuzi hayo. Magufuli ni binadamu kama mimi na wewe lakini angalau kawazidi wagombea wote waliogombea mwaka jana.
 
Kusema ukweli pamoja na mapenzi yangu kwa CHADEMA kama chama makini na chenye malengo makubwa lakini hili la kupindua katiba ili mtu aendelee kubaki madarakani linatia kichefu chefu na kubadilisha kabisa taswira ya CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO....kwenye demokrasia ya kweli ni lazima kunakuwa na ukomo wa uongozi.....
Hii inaweza kuleta tafsiri ya undumilakuwiri kwa viongozi wa CHADEMA kwa kuhubiri kile wasicho kitenda......

Hakuna ubishi kuwa Mbowe ni kiongozi makini na kwa uongozi wake mzuri amekikuza chama...lakini hii haimaanishi kuwa hakuna mwingine mwenye uwezo wa kuongoza isipokuwa Mbowe tu.....

CHADEMA imejaaliwa vijana wengi wazalendo na wenye elimu kubwa bila ya kusahau uelewa mkubwa wa mambo....hao wote wana sifa za kuongoza chama na kikafikia mafanikio makubwa tu.....

Kuedelea kubakia mtu mmoja kwenye uongozi kwa muda mrefu kiasi cha kupindua katiba ya chama kunaleta picha mbaya kwa wapiga kura na hali ya wasi wasi....ikiwa mtu amethubutu kuipindisha katiba ya chama chake ili aendelee kuwa kiongozi je kiongozi kama huyo atashindwaje kubadili katiba ya nchi ili aendelee kutawala milele au atashindwaje kuvigandamiza vyama vingine vya upinzani ili chama chake kiendelee kubaki madarakani.....?? Huo nao ni udikteta katika sura nyingine.....

Mheshimiwa Mbowe hana budi kujipima kama anastahili kuendelea kuwepo katika ngazi hiyo ya uongozi....na ingekuwa vyema kama angeirudisha kama zamani.....

Nawasilisha....
 
Back
Top Bottom