MIAKA 35 ya CCM na changamoto za kiutawala LIVE ON Star TV

Dogo hapo kwenye TV amenichekesha kusema Nape Kalegea ni Chifu mangungu Mbwa asiye na Meno ..

Inamaana anabweka tu bwa bwa bwa jiondoe mwenyewe.. nani ajiondoe wewe nape... fukuzeni mafisadi tuanze kuwapenda tena msimamie nchi vyema...

Hiyo ndiyo hali halisi mkuu!
 
Bana wewe ni Muongo hizo takwini na za Zamani sana huwezi kuzitumia kuelezea hali ya CCM ya sasa! Hausemi imeshuka kwa kiasi gani na vyama vya upinzani vimepanda kwa kiasi gani!
 
...Dr Bana ...umeaibisha wasomi na usomi....,jibu ulilotoa lime base ..kwenye matokeo ya uchaguzi wa 2010..,,,

Mimi nilidhani umeongea "sasa",ukiwa na Ripoti ya kiutafiri ya sasa......

Je kwa sasa kwa wimbi la uongozii uliopo Sasa hakuna chama mbadala?
Kwa mfumko mkubwa huu asilimia ishirini wa bei hakuna chama mbadala...
Kwa uwezo wa hoja na kiongozi na hata kwa ushauri wanaoutoa kwa serikali ...hakuna chama mbadala...?
Kwa uchumi huu mbovu?? Kwa migomo hii ??
Unaongelea nguvu ndogo ya upinzania.....kwenye katiba ya sasa? Tume ya uchaguzi ?

Nadhani tuna haja ya kuwa na Shaka na maoni ya daktari Bana,,...
 
Mzee mangula unajitambua kweli?unakumbuka ulipokosa uenyekiti mkoa wa iringa ulisemaje?mimi naona mzee mangula njaa imekushika umeamua kujitokeza ili mkono uende kinywani!
 
Mmefanya nini miaka hiyo yote 35 nyie CCM! Kubwa mlilolifanya ni kuiba mali za watanzania na kufisadi nchi kwa kudhurumu haki na utu wa Mtanzania! 2015 bye bye CCM.
 
Dr.bana unatumia takwimu za nec?wakati watu hawana imani na nec?endelea kuchakachua redet!
 
Mzee mangula unajitambua kweli?unakumbuka ulipokosa uenyekiti mkoa wa iringa ulisemaje?mimi naona mzee mangula njaa imekushika umeamua kujitokeza ili mkono uende kinywani!
anarudi taratibu kwenye mtandao wa JK
 
Swali kwa mzee Mangula,
Wakati uliposhindwa kupata nafasi ya uenyekiti mkoa wa Iringa ulikaririwa ukisema nafasi za uongozi zimefika hatua ya kupigwa mnada na mwenye pesa ndo anaupata. Je CCM unayoitetea leo ndo ileile inayonadi nafasi za uongozi?tunajua kwa sasa kuna ccm kama tatu hivi,yeye yupo ccm ipi kwa sasa?

Yahya uliza hili swali
 
Steven maurice kweli,nape ni legelege,hana meno anabweka tu kama the dog!
 
yahya kilio chetu hatupati Star tv kwenye sattelite''ni zaidi ya mwezi sasa'mna mpango gani??
 
Steven Maurice, anajua hali ya sasa ya CCM ni mbaya sana, Nape anapiga propaganda tu! Nakushauri Maurice ukimbie mapema kabla jumba bovu halijakuandikia!
 
Yahya M: ni bora ukaandaa kipindi kingine kama hiki ( CCM NA CHANGAMOTO ZA KIUTAWALA) ikiwezekana na washiriki wawe hawahawa ili wa-Tanzania wamalize kiu yao kwa kuuliza maswali
 
Dr Bana una maana gani Kama msomi kusema hakuna chama mbadala cha kushika dola kwa sasa...fafanua?
Takwimu alizotoa Dr. Bana kulijibu swali hili hazina uhalisia kwani hajazungumzia wizi mkubwa wa kura na hujuma za watu wa usalama wa Taifa dhidi ya wagombea wa vyama vya upinzani. Lakini kwa kuwa Bana ni miongoni mwa wanufaika wa huu mfumo dharimu sikumshangaa. Ukweli utabakia kuwa CCM ina shinda sio kwa ridhaa ya wananchi bali kwa ujanjaujanja na wizi wa kura.
 
Mapendekezo: Nape ni vizuri chama kuunda commission maalum ya kufatilia utendaji wa watendaji wa kisiasa wa chama (wabunge,Wakuu wa Wilaya,Wakuu wa Mikoa na ngazi za serikali za mitaa).Takwimu zinaonyesha kutowajibika kwingi kwa viongozi hawa aidha kwa malengo binafsi ama uwezo finyu.Hasa wabunge wengi hujisahau sana kutimiza wajibu wao hivyo kukipa wakati mgumu chama kumnadi mgombea hasa katika kipindi cha uchaguzi.

Athari hizi usababisha chama kupoteza mvuto,kupata ushindi finyu ama kupoteza jimbo kabisa.

Kazi kubwa ya Commission hii ni kuanalyze mapungufu ya viongozi wake, ilani za chama kisha kushauri nini kifanyike na kuwasilisha taarifa zake katika Secretariate ya chama kwa utekelezaji.
 
Naomba watuhakikishie kuwa ccm wameshindwa kuiongoza hii nchi na wapo teyayari kuiachia ili wakajipange upya
 
Back
Top Bottom