MIAKA 35 ya CCM na changamoto za kiutawala LIVE ON Star TV

Goodmorning studio! Namuliza Nape CHAMA CHAKE KINAFUATA ITIKADI GANI? JE ANAAMINI KUWA RAIS ANANIA YA DHATI NA KUTENGENISHA SIASA NA BIASHARA WAKATI YEYE NDIO WALIOMFADHILI AKAINGIA MADARAKANI?MZEE MANGULA UNALIZISHWA NA NAMNA CHAMA KINAVYOONGOZWA AWAMU YA NNE?MANGULA NA NAPE SUALA LA POSHO KWA NINI SPIKA ANALIPA POSHO BILA IDHINI YA MAMLAKA HUSIKA?MTAMCHUKULIA HATUA GANI SPIKA KAMA CCM?JE MZEE MANGULA UNAKUBALI KUA MAAMUZI YA Z'BAR NDIO YALIASISI UFISADI NDANI YA CHAMA?KAMA MAMUZI YA Z'BAR NDIO YALIUA AZIMIO LA ARUSHA KWA NINI TUSIITE AZIMIO LA Z'BAR?
 
Kutoka Arusha, Je, Nape anakubali kuwa CCM imeshindwa kuithibiti serikali yake? Je, anakubaliana sasa kuwa ni wakati muafaka kutenganisha kofia ya uenyekiti wa CCM na Urais wa nchi?
 
Swali kwa Mzee Phillip Mangula:
Kwanini Mzee Mangula anakanusha kuwa Azimio la Zanzibar halikuwepo?
Mambo yaliyopitishwa kule Zanzibar ni yapi?
 
hili swala la makinda na waziri mkuu kusema posho zimepanda huku rais akipinga mnalichukuliaje kama chama
 
Dr.BANA UNAYUMBISHA MJADALA KWA KUTOONYESHA UPO UPANDE GANI,NANI KAKUAMBIA WANANCHI BADO WANAIMANI NA CCM?WAKATI JK AMEKILI HADHARANI NA MAMA KIKWETE WATU WANAICHUKIA CCM HASA VIJANA,DR.BANA USICHAKACHUE MJADALA HUU UKO LIVE UNAJUA?SIO RIPOTI ZA REDET HIZI!
 
Yahaya naomba uniulizie kwa ndg yangu Nape hivi miaka 35 ya chama chetu WABUNGE WA CHAMA WANAONGOZA KUMGOMEA MKITI WA CHAMA KATIKA MAMBO YENYE MASLAHI KWA NCHI NA WANACHAMA WETU...TUNAMTAKA ATOE TAMKO LA CHAMA.
 
Nape ni kweli hamlipi vijana wasomi wanaoshirikii makongamano,...Yake mabasi yanayokusanyaga wanavyuo kuwapeleka ubungo plaza na diamond ......na zile posho mnazotoa za Tzs 10'000 ...sio rushwa??????????? Huoni aibu kusema uwongoooo...na propaganda zisizokuwa na tija...

Wapinzani ndio kuandaa makongamano bila kutumia sentiii..
 
Habari bwana Yahaya!,swali langu kwa Nape...wewe mvuto kwa wasomi kwako unauchukuliaje? Ni kwa wale ambao wako uongozini au ni idadi ya wasomi walio wanachama wa chama husika pamoja na washabiki Wake.
 
Nape wacha kumwaga mapovu Katibu mkuu wako anasema Chama kimepoteza mvuto kwa vijana na wewe unajifanya unashangaa sababu umeenda india na marekani so kwa akili zako hao vijana wa india na marekani ndio wanaopiga kura? hebu funguka uelewe vijana wanaozungumziwa ni vijana wasomi wa Tanzania..

Hili hlipingiki ccm haina mvuto kwa vijana fanya jitihada za fact na si uchwara kemeeni maovu ndani ya chama na serikalini ikikaa sawa na haki kwa wote mvuto takuja wenyewe .. Huu ushauri nakupa kwa njia nyingine utapotea bila kukumbukwa
 
Kutoka Arusha, Mwenyekiti wa CCM alishakiri kuwa CCM imepoteza mvuto, alisema haya Dodoma hadharani, Nape anapinga nini? Huko ni kujidanganya na kwa style hii watanzania tumejia CCM haina Nia ya kujirekebisha!
 
Naomba yahya urudie swali langu,mi namaanisha CDM,ww umeinclude CCM B na C,CUF na NCCR
 
Swali kwa mzee Mangula,
Wakati uliposhindwa kupata nafasi ya uenyekiti mkoa wa Iringa ulikaririwa ukisema nafasi za uongozi zimefika hatua ya kupigwa mnada na mwenye pesa ndo anaupata. Je CCM unayoitetea leo ndo ileile inayonadi nafasi za uongozi?tunajua kwa sasa kuna ccm kama tatu hivi,yeye yupo ccm ipi kwa sasa?
 
Steven maurice unaongea facts!!,nape hajitambui mwambie ukweli huyo!
 
Dogo hapo kwenye TV amenichekesha kusema Nape Kalegea ni Chifu mangungu Mbwa asiye na Meno ..

Inamaana anabweka tu bwa bwa bwa jiondoe mwenyewe.. nani ajiondoe wewe nape... fukuzeni mafisadi tuanze kuwapenda tena msimamie nchi vyema...
 
Steven maurice,unafunguka kweli,nape hana meno,hajui kuchambua mambo funguka funguka kaka!!!
 
Back
Top Bottom