CCM imetimiza miaka 31 tangu kuanzishwa kwake. Pengine sherehe hizi mwaka huu ndio zitazokuwa za kimya kabisa kupita miaka mingine yote.
Hongera sana CCM
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
CCM imetimiza miaka 31 tangu kuanzishwa kwake. Pengine sherehe hizi mwaka huu ndio zitazokuwa za kimya kabisa kupita miaka mingine yote.
Hongera sana CCM
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Nakumbuka sana, CCM ikiwa inazaliwa, nilikuwa mdogo sana shule ya msingi lakini tayari nilikuwa mwumini wa siasa za TANU, ujamaa na Nyerere.
Nilikuwa na imani kubwa sana CCM. Sasa ni mtu mzima, nimesoma, nimetembea dunia na kuona kwanini wenzetu wanaendelea wakati sisi tuko pale pale.
Malengo ya CCM yalikuwa mazuri tu, hata leo bado ni mazuri tu. Bahati mbaya viongozi wetu ambao wengi walizaliwa kabla ya uhuru, hawakushiriki mapambano ya kudai uhuru, ilitakiwa ndio waendeleza mapambano ya kudai uhuru wa kiuchumi. Bahati mbaya sana wametusaliti wananchi na wamegeuka wakoloni weusi.
Kosa kubwa la Nyerere lilikuwa kuifanya CCM ishike hatamu (monopoly). Kushika hatamu huko ndiko mpaka sasa kunawafanya viongozi wetu washindwe kutofautisha kati ya kilicho cha CCM na kile cha wananchi. Hatamu hiyo hiyo ndio inavifanya vyombo kama PCCB, polisi, mahakama, nk. vitumike kama vyombo vya kulinda maslahi ya CCM na viongozi wake.
Binafsi bado nina imani na ile CCM ya Nyerere, kinachotakiwa ni kuirudisha CCM kwa wananchi. Ningependa CCM ishindwe ili iwe nafasi ya kujisafisha na kujijenga upya kama vilivyofanya vyama vya Kikomunisti kule Ulaya Mashariki.
Wakati tuna akina Malecela ambao wanailinda CCM kwa mazuri na mabaya, kuna haja ya kupata akina Gorbachev ambao wataiua au kuivunja CCM kwa faida ya ya nchi yetu na CCM yenyewe huko mbeleni.
Hali ya CCM ya leo inasikitisha sana, inaua matumaini yote ambayo kama kijana, nilikuwa tayari kuitumikia na kuilinda. Leo imegeuka kuwa chombo cha matajiri na majizi ambayo hayana visions zozote za kumkomboa Mtanzania kutoka kwenye umaskini wa ajabu. Miaka karibu 50 ya kuwa huru bado hali za wananchi wengi ni mbaya kuliko miaka ya 70. Sera za mwalimu kama mtu ni afya, kilimo bora, kujitegemea nk vyote vimekufa na sasa hatuna sera zozote za maana zaidi ya majigambo majukwaani.
Nimezaliwa kijijini, pamoja na kutokuwa na vitu muhimu kama viatu na nguo nyingi lakini miaka yote ya utoto wangu sikuwahi kushinda njaa. Tulikuwa na vyakula vya kutosha, sikuwahi kumwona mtoto wa jirani au wa ndugu anashinda njaa. Kulikuwa na zahanati ambako hata kama mtu aliumwa ghafla usiku, basi kulikuwa na uwezekano wa kwenda kumwamsha daktari na kupata matibabu bila ulalamishi wala kuombwa pesa. Kulikuwa na shule nzuri tu, shule zilizokuwa zinaendeshwa na walimu wenye nia na lengo la kuwaendeleza watanzania wenzao, shule ambazo ubora wake haukuwa tofauti na ubora wa shule walizosoma watoto wa mawaziri mijini.
Leo nikirudi kijijini naona watu wazima wamegeuka ombaomba, watoto wanakufa kwa malaria ambayo madawa yake yanajulikana miaka na miaka, shule za umma ni za maskini, viongozi wetu wanapeleka watoto wao majuu na kwenye shule za bei mbaya. Hivi kweli huu ndio uhuru na maendeleo ambayo TANU na kisha CCM walituahidi?
Wana CCM amkeni, tambueni kwamba nyie ndio mumeuza chama kwa kuchagua watu wasio na mwelekeo wala uwezo wa kutuongoza, watu ambao wanatuacha wananchi kwenye shule hoi zisizo na walimu, wao wanapeleka watoto wao Ulaya, viongozi ambao wanatumia mabilioni kwenda kufanya checkups Ulaya huku watoto na akina mama wanakufa kwa kukosa dawa ya malaria. Viongozi ambao wanawaacha vijana wetu wanahaha barabarani kwa kukosa kazi, huku wanaruhusu wageni kuajiriwa hata kwenye kazi ambazo Watanzania wanaweza kufanya bila matatizo. Viongozi ambao wanaruhusu kila takataka iagizwe toka nje, huku mananasi na matunda yetu mengine yanaoza kwa kukosa soko.
Sina cha kufurahia kuhusu uhai wa CCM na badala yake hiyo sherehe itakuja fanyika siku CCM itakapo pelekwa theatre na kufanyiwa operation ili kuondoa cancer iliyotapakaa kila sehemu. Siku ambapo CCM itakubali kuachia madaraka japo kwa muda ili ifanyiwe matibabu makubwa kwa faida yake na Watanzania wote.
Pole sana kwa wana CCM wote, huyo mwaneno ni taahira!
Hilo jina lisiwapumbaze naweza kulibadilisha hata kesho.
La muhimu leo hii ni kwamba Watanzania woote popote waliopo tufurahie Chama chetu kitukufu CCM kuadhimisha miaka 31 ya kuzaliwa! Ni furaha iliyoje!! CCM Hoyee!! JK juu!! Juuu!! Juuu!! Juu zaidi!!
wanaumiwa na wataumia sana,ukweli CCM imefikisha miaka 31.
........
CCM imepita katika mengi na mengi hayo yamechangiwa na siasa za kimataifa. Wakati wa vita baridi ulikuwa ni wakati ambao kulikuwa na umuhimu mkubwa wa kuwa na chama kimoja cha kisiasa kuliko wakati mwingine wowote ule. Hivyo wazo la Mwl.Nyerere na wasaidizi wake halikuwa baya, zaidi lilirenga kwenye maslahi ya taifa, ambayo hadi leo tunaendelea kufaidika. Misingi iliyojengwa katika kipindi cha vita baridi, itachukua muda kubomaoka mna kutoweka kabisa. Katika mfumo wa sasa ambapo ni taifa moja tu lenye nguvu na kauli ya mwisho, tumeendelea kuona machafuko katika tawala za ndani katika nchi zinazoendelea. Hali hii kwa sasa inainyemelea nchi yetu.Nilikuwa na imani kubwa sana CCM. Sasa ni mtu mzima, nimesoma, nimetembea dunia na kuona kwanini wenzetu wanaendelea wakati sisi tuko pale pale.
Malengo ya CCM yalikuwa mazuri tu, hata leo bado ni mazuri tu. Bahati mbaya viongozi wetu ambao wengi walizaliwa kabla ya uhuru, hawakushiriki mapambano ya kudai uhuru, ilitakiwa ndio waendeleza mapambano ya kudai uhuru wa kiuchumi. Bahati mbaya sana wametusaliti wananchi na wamegeuka wakoloni weusi.
Kosa kubwa la Nyerere lilikuwa kuifanya CCM ishike hatamu (monopoly). Kushika hatamu huko ndiko mpaka sasa kunawafanya viongozi wetu washindwe kutofautisha kati ya kilicho cha CCM na kile cha wananchi. Hatamu hiyo hiyo ndio inavifanya vyombo kama PCCB, polisi, mahakama, nk. vitumike kama vyombo vya kulinda maslahi ya CCM na viongozi wake.
Kipindi cha Mzee wa Ruska hapana shaka ndio kilikuwa kipindi ambacho ni sawa na kipindi cha Urusi na Gorbachev. Mabadiliko makubwa yalitokea katika kipindi hicho nchini, hata hivyo yaliweza kuwanufaisha wachache tu. Aidha baada ya Kipindi hicho kupita, Chama cha Mapinduzi kilifanikiwa kubadilisha mwelekeo wake na kwenda na wakati zaidi. Mafanikio katika hilo yaliweza kuonekana katika kipindi cha Mkapa. Tathimini nzuri itatokea mara baada ya Mwenyekiti wa sasa wa CCM kumaliza ngwe ya kwanza ya Uprez.Wakati tuna akina Malecela ambao wanailinda CCM kwa mazuri na mabaya, kuna haja ya kupata akina Gorbachev ambao wataiua au kuivunja CCM kwa faida ya ya nchi yetu na CCM yenyewe huko mbeleni.
Hapa umeongeza chumvi Kamanda, Hakuna sehemu yoyote yenye uhakika wa kuishi kibinadamu zaidi katika Tanzania kama vijijini. Ukiondoa mabadiliko ya kiuchumi duniani, mabadiliko ya hali ya hewa na mashinikizo ya vyombo vikubwa vya fedha duniani, kijijini bado ni sehemu ambayo mtu anaweza kuishi kwa amani na kupata huduma muhimu vilevile.Nimezaliwa kijijini, pamoja na kutokuwa na vitu muhimu kama viatu na nguo nyingi lakini miaka yote ya utoto wangu sikuwahi kushinda njaa. Tulikuwa na vyakula vya kutosha, sikuwahi kumwona mtoto wa jirani au wa ndugu anashinda njaa. Kulikuwa na zahanati ambako hata kama mtu aliumwa ghafla usiku, basi kulikuwa na uwezekano wa kwenda kumwamsha daktari na kupata matibabu bila ulalamishi wala kuombwa pesa. Kulikuwa na shule nzuri tu, shule zilizokuwa zinaendeshwa na walimu wenye nia na lengo la kuwaendeleza watanzania wenzao, shule ambazo ubora wake haukuwa tofauti na ubora wa shule walizosoma watoto wa mawaziri mijini.
Haupo peke yako katika hili wapo wengi na wengi wanaingia. Lakini ukweli ni kuwa CCM imefanya mengi na itaendelea kufanya mengi.Sina cha kufurahia kuhusu uhai wa CCM na badala yake hiyo sherehe itakuja fanyika siku CCM itakapo pelekwa theatre na kufanyiwa operation ili kuondoa cancer iliyotapakaa kila sehemu. Siku ambapo CCM itakubali kuachia madaraka japo kwa muda ili ifanyiwe matibabu makubwa kwa faida yake na Watanzania wote
Tusiongelee ushabiki tu, huduma za afya nchini zinazidi kuwa bora kila siku. Aidha kumekuwepo na matatizo ya watu binafsi katika kulinda afya zao na kufuata taratibu za kiafya katika kuhakikisha wanajifungua salama. Tatizo la watoto wengi kufa kabla ya kufikisha miaka 5, lipo kwa ukanda mzima wa kusini mwa jangwa la Sahara. Kwa upande wa serikali ya CCM inaendelea vema katika kupunguza na hatimae kuondoa tatizo hilo.1. Kina mama wajawazito wanaokufa bila huduma nzuri
2. Watoto wachanga wanaokufa kwa magonjwa yanayotibika
MMhm CCM haiwezi kutimua wananchi katika eneo lao pasipo kuwepo na sababu ya msingi ya kufanya hivyo. Na inapotokea kuwa watu wanaondolewa katika ardhi wanayomiliki kisheria basi taratibu zote hufuatwa.3. Wananchi wa Buzwagi na Bulyanhulu waliotimuliwa na ccm
4. Wananchi wa kanda ya ziwa ambayo ardhi yao imeuzwa kwa Barick
Mambo mengine ni vichekesho, eti umeme wa kuruka? sijapta kusikia hilo! Ina maana kuwa Tanzania sasa kuna umeme wa magendo?5. Watanzania wanaolipia umeme kwa bei ya kuruka
6. Watanzania wa Kigoma ambao wametengwa na Tanzania
7. Wananchi wa vijijini wasio na barabara nzuri
8. Watoto wa shule wanaokaa kwenye mavumbi kusoma
9. Mamilioni ya watanzania wanaishi kwa mulo mmoja
CCM imetimiza miaka 31 tangu kuanzishwa kwake. Pengine sherehe hizi mwaka huu ndio zitazokuwa za kimya kabisa kupita miaka mingine yote.
Hongera sana CCM
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Hivi huyo Avenue M hamjamjua tu? Come on....
Kwani CCM kama Chama imewakosea nini? Why can't you join CCM to clean the house.