Miaka 3 ya Hayati Magufuli vs Miaka 3 Rais Samia madarakani

Miaka 3 ya Hayati Magufuli vs Miaka 3 Rais Samia madarakani

Matapeli yasiyo na maono yoyote yaliyojificha kwenye koti la uongozi yameumbuliwa mchana kweupe na Hayati Magufuli akiwa kaburini

Kila Kona ya nchi Sasa ni mtetemo na mtikisiko ikienda sambamba na tabasamu la kumalizika Kwa miradi iliyoanzishwa wakati wa utawala wa Hayati Magufuli. Ni juzi tumeambiwa mtambo namba 8 wa kuzalisha umeme katika bwawa la JNHPP umewashwa na kuwashwa huko tatizo la umeme litapungua Kwa 85% ,hii ni habari njema na ya matumaini makubwa. Hamu inaendelea kuwa kubwa endapo mitambo yote 9 ikiwashwa na kuanza kuzalisha umeme ,Je matokeo yake yatakuwaje?

Hilo likiwa halijakauka ,habari njema zaidi ni kuanza Kwa majaribio ya SGR kutoka Dar mpaka Moro, majaribio ambayo yamefanyika Kwa mafanikio. Kuanza kufanya kazi Kwa SGR uchumi wa Tanzania utafunguka Kwa kiwango kikubwa.

Miradi hii ,wa kufua umeme na SGR ni pigo litakaloikumba upinzani na Kwa sababu hawaoni wataendelea kuona watanzania wanataka maandamano. Watanzania wanataka maendeleo na maendeleo yanayoletwa na Serikali ya CCM ni ya vizazi Kwa vizazi.

Miradi mikubwa yote ambayo hapo kabla ili " white elephant projects" na wapinzani Sasa imekuwa miradi yenye matokeo mazuri kwenye uchumi. Miradi hiyo itautesa upinzani Kwa miaka mingi sana na kama upinzani wataendelea kuzurura bila ajenda ,sioni mwisho kwao.

Mwenyezi Mungu mpe pumziko jema mja wako , matokeo ya kazi ngumu Kwa nchi hii tumeanza kuyaona Sasa.
T 2025 JPM.....[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] sasa umefurahi?
 
JamiiForums

Miaka mitatu ya Rais Samia;Kila kitu kimepanda bei.​

Unwatch
•••
[IMG alt="Mwande na Mndewa"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/625/625561.jpg?1615621280[/IMG]

Mwande na Mndewa​

JF-Expert Member​

Serikali yote ni ya CCM,walisema wapinzani wanawachelewesha lakini tunajionea wenyewe miaka mitatu ya Rais Samia vitu vyote vimepanda bei mara mbili toka utawala wa Hayati Rais Magufuli,petroli imepanda bei,sukari imepanda bei,unga umepanda bei,Mchele umepanda bei, maharage yamepanda bei,nyama imepanda bei,n.k

-Tatizo ni nini!?
Magufuli angekuwepo mambo yangekuwa kama alivyotaka yaani bila wapinzani Maendeleo tungeyaona,ila amefariki na project yake hakuna wa kuiendeleza,aliyekuja Mama Samia yeye anaamini uwepo wa Wapinzani wampigie kelele ndio afanye lakini pia yeye ni Mama wakitaka kumpigia kelele anawapa tabasamu wanakaa kimya,hili ndio tatizo letu,tumekwama.
 
Ndiyo maana Chadema ni mazwazwa mnapinga hadi ujenzi wa bwawa la umeme ambao ni kwa ajili yenu wenyewe.

Kucha kuombaomba tu walichofanyia kazi wanaume wenzenu,
. Lema na Lisu Familia zao wanalishwa na wazungu.
 
Rais Samia ametimiza miaka 3 tangu achukue madaraka ya urais lakini ukilinganisha na miaka 3 ya hayati Magufuli akiwa madarakani ni kama mlima na kichuguu kwa matokeo.

Rais Samia amefanya semina nyingi kwa mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi na wakuu wa mikoa lakini bado utendaji wa serikali yake uko duni sana! Matokeo baada ya semina hizo hayaonekani kabisa.

Rushwa, uzembe, mfumuko wa bei, kupandisha gharama za miradi, kuchelewesha miradi imekuwa ndiyo sifa kuu ya serikali ya Rais Samia.

Hayati Magufuli alijenga majengo ya wizara na kuhamishia serikali yote Dodoma ndani ya miaka 3 lakini Rais Samia kwa miaka 3 hakuna jengo hata moja lililokamilika kiasi cha kuanza kukaliwa na watu.

Kwenye serikali ya Samia hamna mradi hata mmoja ulioanzishwa unaoweza kusema kwamba angalau hapa Kuna watu walikaa na kutumia akili.

Rais Samia amefanya vizuri sana kwenye ujenzi wa madarasa kwa kutumia mkopo wa fedha za Uviko.
Miradi iliyoanzishwa mingi kwa mara moja na huyo unayemsifia upi ulikuwa umekamilika?
Yote ilikuwa kwenye hatua za awali.
Kwa sasa mingi kati ya hiyo inakamilika; je hiyo pesa ya kuikamilisha aliitafuta baba'ko JPM.
Ingelikuwa unafikiri kidogo tu; ungempongeza mama kwa kazi kubwa anayoifanya ya kumalizia viporo vingi na vigumu.
Utaanzishaje miradi mipya ilhali kuna miradi mingi ya kuimalizia?
 
Ilani ya ccm 2020 - 2025 inasemaje?
 
Wapinzani wa Senegal siyo wasaliti wa nchi kama hawa wa Tanzania.

# Lisu tutashitakiwa MIGA tukidai kodi kwenye madini yetu.

# tukichimba bwawa la umeme mvua haitanyesha tena na miti millioni 3 itakatwa hivyo tutatengwa kimataifa.
 
Samia aliikuta nchi imefilisika, watu wameporwa pesa zao, wengine wamewekwa ndani kiuonevu, bureaus wamenyang'anywa dollars zao, wafadhili wamekataa kutoa misaada na nchi inetengwa. Tulijazwa propaganda eti tunajenga kwa pesa zetu kumbe mikopo umiza. Anitajie mtu mradi uliojengwa kwa pesa zetu kama jiwe alivokuwa anatupanga
 
Nadhan ni muhimu wakati mnafanya hizo comparisons,pia angalieni mazingira ambayo kila mmoja wao alipopokea kijiti nchi ilikua katika Hali ipi...kiuchumi,kitamaduni na kisiasa.
 
Nadhan ni muhimu wakati mnafanya hizo comparisons,pia angalieni mazingira ambayo kila mmoja wao alipopokea kijiti nchi ilikua katika Hali ipi...kiuchumi,kitamaduni na kisiasa.
Magufuli alipokea Nchi wakati mzuri kushinda Samia ila amezidiwa.

Anaebisha aniletee takwimu hizi hapa 👇
20240420_124314.jpg
20240420_124306.jpg
 
Rais Samia ametimiza miaka 3 tangu achukue madaraka ya urais lakini ukilinganisha na miaka 3 ya hayati Magufuli akiwa madarakani ni kama mlima na kichuguu kwa matokeo.

Rais Samia amefanya semina nyingi kwa mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi na wakuu wa mikoa lakini bado utendaji wa serikali yake uko duni sana! Matokeo baada ya semina hizo hayaonekani kabisa.

Rushwa, uzembe, mfumuko wa bei, kupandisha gharama za miradi, kuchelewesha miradi imekuwa ndiyo sifa kuu ya serikali ya Rais Samia.

Hayati Magufuli alijenga majengo ya wizara na kuhamishia serikali yote Dodoma ndani ya miaka 3 lakini Rais Samia kwa miaka 3 hakuna jengo hata moja lililokamilika kiasi cha kuanza kukaliwa na watu.

Kwenye serikali ya Samia hamna mradi hata mmoja ulioanzishwa unaoweza kusema kwamba angalau hapa Kuna watu walikaa na kutumia akili.

Rais Samia amefanya vizuri sana kwenye ujenzi wa madarasa kwa kutumia mkopo wa fedha za Uviko.
CHAWA lazima wakuwashe!!! Walivyogundua pale hakuna kiongozi sasa lile gap limeamriwa lifunikwe kwa SIFA na MAPAMBIO.

RIP JPM ulikuwa kiongozi kwelikweli
 
Nonsense. Nilidhani utakuja kwa takwimu kumbe ni maelezo ya jumla. Tutajie kukua kwa pato la Taifa ongezeko la ajira miundombinu FDI . Mapato ya nchi. Demokrasia nk. Twende kwenye hizo parameters na njoo tena na ulinganishi mzuri
CHADEMA mna hasira sana na JPM
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom