Miaka 20 Ya Kipanya kuwatetea wanyonge

Miaka 20 Ya Kipanya kuwatetea wanyonge

Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
14,593
Reaction score
5,582
kipanya.jpg

Dar es Salaam. Miongoni mwa Watanzania wengi, kuna vijana wachache walioamua kutumia maarifa na vipaji vyao ili kujiletea maendeleo na kuondokana na tatizo la kukosa ajira, wakijiajiri kwa kazi mbalimbali kisanaa kwa mikono yao.

Ali Masuod maarufu ‘Kipanya', ni mmoja wa vijana hao. Yeye anajihusisha na harakati mbalimbali za kuleta mapinduzi ya fikra kwa kundi la vijana na Watanzania kutumia fursa, uwezo na kipaji chake katika uchoraji katuni maarufu kwa jina la Kipanya.

Mbali na uchoraji wa katuni, Masoud ambaye pia ni maarufu kwa jina la katuni anayoichora ya Kipanya ni mtangazaji, mshereheshaji, mwandaaji na mwongozaji wa vipindi kikiwamo cha Maisha Plus.

Katika mahojiano na mwandishi wa makala haya, msanii huyo anaeleza mengi ikiwamo safari ya maisha ya Katuni ya Kipanya, malengo na matarajio yake.

Masoud anabainisha kuwa alianza kazi ya uchoraji katika mazingira magumu yaliyosababisha kutembea umbali mrefu akitafuta ajira kabla ya kutambulika rasmi katika sanaa ya uchoraji katuni na mwaka huu ametimiza miaka 20 ya uchoraji wa Katuni ya Kipanya.

"Nafikiria mambo zaidi ya milioni moja katika kipindi cha nusu saa, lakini natumaini na kuamini inawezekana na siku moja nitafanikiwa," anasema.

Swali: Katuni ya Kipanya imekuwa ikibadilika kadiri siku zinavyokwenda, anatafsiri nini katika maisha ya kila siku kwa Mtanzania?

Jibuu: Ni kweli, mwanzoni Kipanya alikuwa akionekana bila mavazi, akitembea kwa miguu minne, lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda Kipanya akawa anabadilika kulingana na mazingira anayopitia au anayoingia.

Alianza akiwa hana mtoto kwa mwaka huo, lakini kwa sasa Kipanya ana mke na wakati mwingine anaonekana akitembea na mtoto wake. Kwa hiyo, kadri anavyoendelea kuishi, ipo siku atapata mjukuu.

Napenda Watanzania watambue kwamba, Kipanya ni mtetezi wa shida zao. Anatafsiri mambo mengi. Mara nyingi hufatilia mfumo wa siasa na utawala bora kwa sababu ndiyo mhilimili unaotoa majibu ya umaskini wa Mtanzania.

Unaweza kumwona akiwa bungeni, kwenye kamati ya kuibua maovu ndani ya vyama vya siasa. Kipanya ni Mtanzania anayehoji na kupigania matumizi ya rasilimali zake kumletea maendeleo. Huwezi kumwita mwanasiasa au mwanaharakati tu bali ni zaidi ya hayo.

Swali: Wazo la kutumia Mchoro wa Kipanya lilitokana na mtazamo gani uliokuwa nao kwa wakati huo?

Jibu: Mchoro wa Kipanya ni wazo lililokuja akilini baada ya kupata nafasi ya gazeti hilo la Majira, ambalo lilianza kuandika habari za siasa kwa uhuru zaidi, ikabidi nifikirie aina gani ya mchoro utakaokuwa ukiwakilisha mawazo yangu kwa njia ya katuni.

Ilikuwa ni ghafla Mchoro wa Kipanya ukanijia akilini na kuona unakidhi vigezo vya sanaa yangu.

Swali: Unaonekana kuanza kitambo uchoraji, ilikuwaje safari yako ya kielimu?

Jibu: Safari yangu ya upande wa elimu ilikuwa ni mwendo wa kuungaunga. Nimemaliza darasa la saba katika Shule ya Msingi Kijitonyama mwaka 1986, lakini kutokana na sababu ambazo hadi leo sizielewi, sikuweza kufaulu katika mtihani wa darasa la sababu ingawa nilishishika nafasi kati ya moja hadi kumi kuanzia darasa la kwanza.

Kwa wakati huo, tayari nilikuwa nina msukumo mkubwa katika sanaa ya uchoraji.

Nikiwa bado njiapanda ya kuendelea na elimu ya sekondari, nikapata fursa adimu ya kusomea masomo ya Sanaa ya uchoraji (Fine Art) kwa miaka miwili, yaliyotolewa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwa kutumia mtalaa wa Chuo Kikuu. Hata hivyo, baada ya sisi kumaliza, darasa lile halikuendelea tena.

Nikiwa shule, nikaanza kuchora katuni zilizochapishwa katika Gazeti la Heko mwaka 1988, hapo nilikiwa na umri wa miaka 16, nilichora michoro ya hadithi za katuni.

Mwaka 1989 mwishoni, familia yetu ilipata ugeni wa mtoto wa mjomba wangu aliyekuwa akiishi Malawi. Kwa bahati nzuri alipoondoka nikaondoka naye kwenda Malawi.

Mazingira ya Malawi ilipokuwa ikiishi familia ya mjomba yalikuwa ni ya kijijini nami nilikuwa nimetokea mjini, hiyo mwaka 1990 nilipotakiwa kuanza masomo ya sekondari Malosa School eneo la Chilema kati ya Lilongwe na Blantyre nilianza kwa shingo upande na nikasoma kwa mbinde sana.

Nadhani utoto nao ulichangia, mwaka 1994 nikarudi Dar es Salaam baada ya kumaliza sekondari. Kwa msingi huo safari ya kielimu ni vizuri, mwaka 2008 nilijiunga na Chuo Kikuu Huria (OUT) kwa masomo ya Shahada ya Sayansi ya Siasa, ingawa miezi michache baadaye niliahirisha masomo na mpaka leo sijapata muda wa kuendelea.

Chanzo: Mwananchi
 

Attachments

  • kipanya.jpg
    kipanya.jpg
    24.7 KB · Views: 806
Kipanya hata alipokuwa power brekfast ya clouds redio alikuwa anakemea sana maovu ya watendeji wa serikali wanaonyanyasa wananchi tofauti na sasa gerad hando paul james babra hassan na mbwiga wao.
 
Kipanya hata alipokuwa power brekfast ya clouds redio alikuwa anakemea sana maovu ya watendeji wa serikali wanaonyanyasa wananchi tofauti na sasa gerad hando paul james babra hassan na mbwiga wao.

Hao wameaidiwa ukuu wa wilaya ndo maana kila kitu ni kuisifia ccm na mafisadi
 
Nsipokomenti apa ntato avatar!! Safi sana kipanya kazi nzuri

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Masoud Kipanya style yake aliyoondokea Clouds FM Inanipaga funzo fulani maishani kila siku.
 
Kipanya "Masoud" ni mtu asiyeyumbishwa na upepo wA Kisiasa.Yupo firm kwa jambo analoamini lina manufaa kwa jamii.

Nakumbuka alichora katuni akimuuliza Mrema kama ung`avu wa uso wake (kama alivyokuwa anajigamba) unatokana na kikombe cha Babu wa Loliondo au ni kwa sababu ya posho bungeni.

Kwa ambao walikuwa wametekwa na Babu hawakumwelewa kabisa Kipanya!!
 
Kazi yake ni nzuri sana maana ni mbunifu na si mwoga katika kuwasilisha ujumbe. Aendelee hivyo ili mtanzania mnyonge aweze kutatuliwa kero zake nyingi ingawa watatuzi wa kero hizo hujifanya hawaoni.
 
Jamaa kitambo katika gani,nakumbuka tangu enzi za gazeti la sanifu alikuwa anatoa nondo za ukweli...
 
Huyu jamaa yuko poa sana na kipaji anacho
 
Back
Top Bottom