Miaka 10 ya Dr Shein madarakani Zanzibar pamekuwa mahali penye amani

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
92,426
161,001
Kiukweli Rais wa Zanzibar Dr Shein ameifanya Zanzibar pawe mahali pa amani na salama kuishi.

Zanzibar ya Dr Shein utegemezi wa bajeti ya serikali kwa wahisani umepungua.

Miundo mbinu imeimarishwa ukiwemo ununuzi wa meli mpya ya mafuta

Wazee wote wanalipwa posho ya kila mwezi ili kujikimu kimaisha

Niishie hapo kwa kuipongeza CCM
Maendeleo hayana vyama!
 
.... Bali palipojaa njaa na dhiki ya kutupwa , kwa kadiri ya ufahamu wangu Dr Sheini amekuwa kiongozi aliyefeli kabisa kuilinda heshima ya Zanzibar ndani ya Muungano
 
Chanzo cha utulivu wa Z'bar ni kelele na harakati za Kibaharia za Mzee baba a.k.a Jiwe a.k.a Kiongozi wa Malaika.
 
MiCCM mijitu mihabithi kweli, eti kujengewa vibarabara vibovu na vimeli vya mitumba ndio wanaona maendeleo.

Hakuna hata mzanzibari mmoja anaefurahia visiwa vile vilivyo sasa, kama si punguani wa kisonge huwezi kukubali kuwa zanzibar ina amani na utulivu, wazanzibari wenye akili zilizosalimika wanasikitishwa na aina ya uongozi ambao CCM Dodoma inawaletea kila baada ya miaka kumi.

Zanzibar siasa imeshindwa kuleta maendeleo na mshikamano, wanasiasa sio wa upinzani wala hawa wanaojiita walatawala, wote ni wachumia matumbo yao na kujinufaisha na familia zao.

Mashehe na viongozi wa uamsho wamewekwa ndani, baada ya kudhihirika kuwa wanawaumini wingi wanaowakubali na kuwafuata kuliko siasa na vyama vya siasa vyote, vyama vya siasa ndivyo vinavyoleta mgawanyiko katika jamii ya wazanzibari, na laiti mungewaacha waendelee na shughuli za kufanya mihadhara ya uamsho na kushajihisha kuipigania zanzibar iliyohuru, hakuna hata chama kimoja kingebaki na wanachama wenye msisimko katika kusimamia sera za chama husika.

Wazanzibari wanaijua ajenda wanayoitaka, na popote walipo huwa wanajisikia kuitetea ajenda ya "Zanzibar yenye mamlaka kamili kisiasa, kijamii na hasa kiuchumi", na hii ni baada ya serikali ya kitanganyika kupitia ccm na mawakala wao wenye hisia mbaya za kuiweka zanzibar chini ya mamlaka ya kitanganyika kuzidisha njama na matendo yao ya kuidhalilisha zanzibar kiuchumi kitendo kinachoamsha hisia za kiharakati kwa wazanzibari.

Laanatullah CCM
 
Hayo mambo yalianza kuwekwa mizizi na Rais Abeid Amani Karume katika awamu iliyopita kwa kuwaleta Wazanzibar karibu
Kiukweli Rais wa Zanzibar Dr Shein ameifanya Zanzibar pawe mahali pa amani na salama kuishi.

Zanzibar ya Dr Shein utegemezi wa bajeti ya serikali kwa wahisani umepungua.

Miundo mbinu imeimarishwa ukiwemo ununuzi wa meli mpya ya mafuta

Wazee wote wanalipwa posho ya kila mwezi ili kujikimu kimaisha

Niishie hapo kwa kuipongeza CCM
Maendeleo hayana vyama!
 
Sijamsikia mda kwa kweli ila kwenye gazeti moja wameandika anataka waanze kufukia bahari ili kutanua ardhi
Kwa hili nampa heko sana ingawa hatakuwa wa kwanza katika hili lakini ni uamuzi mzuri sana
IMG_1188.JPG
 
Kiukweli Rais wa Zanzibar Dr Shein ameifanya Zanzibar pawe mahali pa amani na salama kuishi.

Zanzibar ya Dr Shein utegemezi wa bajeti ya serikali kwa wahisani umepungua.

Miundo mbinu imeimarishwa ukiwemo ununuzi wa meli mpya ya mafuta

Wazee wote wanalipwa posho ya kila mwezi ili kujikimu kimaisha

Niishie hapo kwa kuipongeza CCM
Maendeleo hayana vyama!
mhimili wa amani Zanzibar ni maalim Seif.

baada ya kuporwa urais 2010 & 2015, mara zote Wazanzibari walimshinikiza aafikiane nao kuhusu kuingia mtaani/msituni but alitumia hekma kubwa kuwatuliza munkari.

ingekuwa ni mwana CCM mwenzangu ndiyo kafanyiwa hivi, sasa hivi Zanzibar ingekuwa kama Syria!!
 
Bwashee wala urojo na kuingia msituni wapi na wapi?!
 
Kama maalim seif angeona mbali kisha asingejitoa kwenye serikali ya umoja wa kitaifa, zanzibar inge paa zaidi kimaendeleo
 
Back
Top Bottom