Mhudumu wa Mochuari "amchimba mkwara" waziri

Mhudumu wa Mochuari "amchimba mkwara" waziri

Sasa ww jamaa unauliza waziri atafiaje mbeyaunaakili kweli ww?waedhmiwa wanafia mpak choon kifohakichagui

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Hawa watu (wahudumu wa mortuary) huwa vichwa vyao havipo vizuri. They care less!! Wana-guts sana!

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
huwa nasikia hawa watu wa mortuary , spirit za waliokufa ndiyo zinakuwa zinawatesa sana eti kutokana na tabia zao chafu mfano ukiwa mortuary watu wengi sana huwa wanahitaji vitu kutoka huko kwa ajili ya ushirikina kama maji ya maiti , nywele , kucha , ulimi, nk.hasa kama marehemu ni mwehu . sasa spirit zingine hazipendezwi na ndiyo maana wanakuwa mazwazwa spirit zinawatokea , wengi wao.
 
Mhudumu wa kitengo cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa Mbeya,Eugene Vurugu amemtishia naibu waziri wa afya,Dr.Saif Rashid kuwa ikitokea amefariki akiwa mkoani Mbeya,basi maiti yake italazwa sakafuni kutokana na uhaba wa majokufu ya kuhifadhi maiti katika kitengo hicho.

Mhudumu huyo alisema kitengo hicho kina majokofu sita na hulazimika kuhifadhi maiti kwa zamu ili angalau maiti zisiharibike.

"Hata wewe Waziri ukifa leo,hakuna pa kukuweka.Utawekwa sakafuni kusubiri maiti nyingine zipoe halafu utaingizwa ndani kwa kuingizwa maiti mbili kwenye eneo la mtu mmoja"alisema Vurugu.

CHANZO:Mwananchi

MY TAKE:
Mfanyakazi huyu atasalimika kweli kwa kumwambia waziri ukweli huu hadharani?

Huyu mtumishi anastahili kupandishwa cheo kwa ujasiri wake wa kutetea mazingira mazuri ya kazi.

Aisee ingekuwa Nyerere angempandisha..cheo...sema mhudumu Hana Elimu kubwa na wanajulikana kuwa ni fuse ...huwezi Kumpa cheo Zaidi ya hichoooo ...labda apelekwe Magereza akawe Mnyongaji Mkuu wa Serikali
 
Namtambua vema muhudumu huyu.......anapga maji ile mbaya halaf kuna sku akaniomba bia pale central police nkamjibu sna hela akanambia .....utanikuta tu kwenye anga zangu... ukweli nlicheka sana
Haahaaa huyo jamaa kweli kadata!
 
Alikuwa na ujumbe maridhawa,ila jinsi alivyouwakilisha ujumbe huo ndo shida ilipo,lakini pia viongozi wetu itabidi watishwe kidogo maana wanajisahau mno,pengine bajeti ya matengenezo ya hapo hospitari ilipangwa ila wakubwa walifanya kinyume chake.
 
Hata kama hatafia Mby ujumbe ameupata na ikatokea kwa mwingine mwenye hadhi ya juu.
 
Ukweli mchungu huo, safi sana. Hapo kwenye pendekezo lako hapo kidogo ndio pamenitatiza, hivi muhudumu wa Mochwari akipandishwa cheo atakua NANI sasa!?
 
Waziri atafiaje Mbeya?!!!!

kwani haiwzekani mkuu?anaweza pata ajali au presha ikampanda akavuta akiwa huko! huyu mtumishi kawakilisha ujumbe wake mahali sahihi and believe me huyo mh hatasahau jambo hilo hasa kila atakapokuwa anaenda mbeya kikazi au binafsi akiwa waziri au raia wa kawaida!
 
Anajifariji labda itokee bahati mbayaa afie hapoo
 
Ukweli mchungu huo, safi sana. Hapo kwenye pendekezo lako hapo kidogo ndio pamenitatiza, hivi muhudumu wa Mochwari akipandishwa cheo atakua NANI sasa!?

Anaweza kuwa mhudumu mwandamizi n.k kama alikuwa hajafikia ngazi husika.
 
Back
Top Bottom