Mimi hua sio mwendaji wa bar, juzi kati hapa nilikua naendesha kikao cha harusi, kama kawaida hua kuna zile pesa za uchakavu, tuliletewa vinywaji vyetu na kuanza kunywa pole pole, mhudumu wa bar ile alikuja na glass (tunafahamiana vizuri nae na baadhi ya staff wa hapo kwenye hiyo bar/hotel) alinambia hivi; kaka yangu usipende kutumia glass za kwenye ma bar please; sikumuuliza sababu cause alining'oneza tu so nikamwambia nenda na glass yako nitakunywa kwa kupiga tarumbeta, hapa nilitoa sauti ya juu na wengine wakinisikia. Nahisi ipo namna na hizo glass za kwenye ma bar.