Nkobe
JF-Expert Member
- Feb 17, 2013
- 2,162
- 3,162
Bila shaka Zitto hawezi kusahaulika katika historia ya Mabadiliko ya kifikra katika Bunge. Zitto ndie mbuge wa kwanza alieweza kuhoji au kusema direct bungeni kwamba Waziri kasema uongo, yeye ndie alieondoa zana ya uoga bungeni, pia kwa kujiamini alisimamia hoja zake. Nakumbuka baada ya kufukuzwa bungeni, mimi nilitembea kwa miguu kupokea msafara wako kuelekea jangwani. Lakini mimi nina wasiwasi na wewe kama ifuatavyo.
Baada ya ule mkutano wa Jangwani, kwa muda mfupi Mheshimiwa Zitto alijiondoa katika harakati za kueneza chama. Chadema ilifanya mikutano mingi ya kueneza chama kwa slogan mbali mbali, ikiwemo Operation Sangara, M4C nk, katika harakati zote hizi Zitto Kabwe hakuonekana kabisa. Wakati Viongozi wa Chadema wakiangaika kueneza chama huku wakipigwa mabomu Arusha, Morogoro, Iringa nk, Mheshimiwa Zitto kastarehe tu. Mimi binafsi nilikuwepo katika matukio kadhaa ya kupigwa mabomu, hata pale Soweto Arusha nilikuwepo
Wengi tulijiuliza, kwanini Zitto kapotea ghafla?, je katika mafanikio ya Chadema ya sasa mpaka kuweza kusimamisha wagombea kwa mitaa na vijiji vingi na kufanikiwa kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa, je Zitto umehangia nini? Unaweza ukasimama ukawaambia Watanzania kuwa katika uenezaji wa Chadema hadi vijijini umechangia ukilinganisha na cheo ulichokuwa umepewa ndani ya chama?
Mimi nasema hivi, vijana wengi tunakupenda lakini kwa dalili hizo nilizozielezea, ukitaka ondoka bwana, maisha yanaweza songa mbele bila wewe. Hata ukiwa na mwanamke mzuri wa sura na umbo, kama akiwa na tabia mbaya, kwa roho ngumu utamwambia kwakheri nakutakia maisha mema.